• About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact
Monday, May 25, 2026
  • Login
Bajeti
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo
No Result
View All Result
Bajeti
No Result
View All Result
Home Mazingira

Mtama wapandwa anga za juu kukabili mabadiliko tabianchi.

by bajeti
January 17, 2023
in Mazingira
0
Mtama wapandwa anga za juu kukabili mabadiliko tabianchi.

Zao la mtama

Share on FacebookShare on Twitter

VIENNA,AUSTRALIA

SHIRIKA la Umoja wa Mataifa la Nishati ya Atomiki, (IAEA) limesema mbegu za mazao zilizopelekwa kituo cha anga za juu mwezi Novemba mwaka 2022 zimepandwa kama sehemu ya utafiti wa kuimarisha aina mbalimbali za mbegu zinazohimili mabadiliko ya tabianchi.

Kwa mujibu wa taarifa ya IAEA iliyotolewa Januari 12,2023 imeeleza kuwa tayari mbegu hizo ikiwemo Mtama zimmepandwa eneo la ndani na nje ya kituo hicho na hivyo zinapata miali kamilifu ya anga za juu pamoja na viwango vya juu zaidi vya joto kwenye eneo hilo.

Kwa mujibu wa IAEA yenye Makao yake Makuu, Vienna nchini Australia, mbegu hizo zilipelekwa na shirika hilo pamoja na lile la Chakula na Kilimo Duniani(FAO) kwa lengo la kuchunguza athari za miali ya anga za juu kwenye mbegu kama sehemu ya utafiti wa kuimarisha aina mbalimbali za mbegu zinazohimili mabadiliko ya tabianchi na hivyo kuongeza uhakika wa chakula.

“Lengo ni kubaini iwapo mazingira magumu ya hali ya hewa anga za juu kama vile joto kali kupindukia, miale kutoka anga za juu vinaweza kuchochea mabadiliko kwenye mbegu na hatimaye mabadiliko hayo ya hali ya hewa yanaweza kusaidia mimea kuwa na mnepo zaidi pindi inapokabiliwa na changamoto za ukuaji au kumea duniani,” imesema taarifa hiyo.

Naibu Mkurugenzi Mkuu wa IAEA ambaye pia ni  Mkuu wa Idara ya Sayansi ya Nyuklia na Matumizi yake, Najat Mokhtar amesema wana wajibu wa kuchunguza teknolojia za kinyuklia ambazo zinaweza kuleta tofauti chanya kwa afya ya binadamu na chakula anachokula.

“Jinsi dunia inahaha kuhimili madhara ya mabadiliko ya tabianchi, tunahitaji kuongeza kasi ya tafiti za kuboresha mimea na kupata majawabu yanayotesheleza na fanisi,” amesema Mokthar.

Next Post
JET  yawataka waandishi wa habari kujikita katika uhifadhi wa maliasili,mapito ya wanyamapori(Shoroba)

JET yawataka waandishi wa habari kujikita katika uhifadhi wa maliasili,mapito ya wanyamapori(Shoroba)

Dkt Mpango ataka wezi na wanaochepusha maji kutoka kwenye mito bila vibali kuchukuliwa hatua

Dkt Mpango ataka wezi na wanaochepusha maji kutoka kwenye mito bila vibali kuchukuliwa hatua

Miradi ya kuhamasisha matumizi endelevu ya ardhi yapunguza kuenea kwa jangwa

Miradi ya kuhamasisha matumizi endelevu ya ardhi yapunguza kuenea kwa jangwa

Discussion about this post

Contact us:

BAJETI COMMUNICATION

info@bajeti.co.tz
bajetinews@gmail.com
+255718699828
P.o.BOX 18133,
DAR ES SALAAM,
TANZANIA

Category

  • Habari
  • Magazeti
  • Makala
  • Mazingira
  • Michezo
  • Picha
  • Sayansi na Teknolojia
  • Siasa

Our Visitors

  • Today's visitors:16
  • Today's page views 16
  • Total visitors 16,470
  • Total page views 18,681

Kuhusu Tovuti Hii

Hii ni tovuti ya habari iliyojikita katika kuandika  habari za kina   zikiwemo za mazingira kwa lengo la kuelimisha na kuuhabarisha umma.

Subscribe

  • About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact

© 2025 Bajeti

No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo

© 2025 Bajeti

Welcome Back!

Login to your account below

Forgotten Password?

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In