• About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact
Tuesday, January 13, 2026
  • Login
Bajeti
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo
No Result
View All Result
Bajeti
No Result
View All Result
Home Mazingira

Miradi ya kuhamasisha matumizi endelevu ya ardhi yapunguza kuenea kwa jangwa

by bajeti
January 25, 2023
in Mazingira
0
Miradi ya kuhamasisha matumizi endelevu ya ardhi yapunguza kuenea kwa jangwa

Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Mazingira Ofisi ya Makamu wa Rais Catherine Bamwenzaki (aliyeka katikati) akiwa katika picha ya pamoja na washiriki wa kikao cha wataalamu cha kuhakiki rasimu ya Mpango wa Kitaifa wa Kupambana na Kuenea kwa hali ya Jangwa na Ukame chini ya Mkataba wa Umoja wa Mataifa wa Kupambana na Kuenea kwa hali ya Jangwa na Ukame (UNCCD) Januari 25, 2023 jijini Dodoma(Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)

Share on FacebookShare on Twitter

NA MWANDISHI WETU,DODOMA

TANZANIA imefaidika na miradi ya kuhamasisha matumizi endelevu ya ardhi hivyo kupunguza kuenea kwa hali ya jangwa,ukame na athari zake

Hayo yamesemwa Januari 25,2023 jijini Dododma na Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira) Dkt. Switbert Mkama wakati akifungua kikao cha wataalamu cha kuhakiki rasimu ya Mpango wa Kitaifa wa Kupambana na Kuenea kwa hali ya Jangwa na Ukame chini ya Mkataba wa Umoja wa Mataifa wa Kupambana na Kuenea kwa hali ya Jangwa na Ukame (UNCCD).

Akizungumza kwa niaba ya Naibu Katibu Mkuu, Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Mazingira Ofisi ya Makamu wa Rais Catherine Bamwenzaki amesema Mkoa wa Kilimanjaro unafaidika na mradi wa kuokoa maeneo yaliyoharibibika wakati Tabora na Katavi imefaidika na mradi wa kuhifadhi misitu ya miombo.

Amesema Tanzania inafaidika pia na Mradi wa Kunusuru Vyanzo vya Maji Kupitia Usimamizi Endelevu wa Ardhi Katika Mabonde Madogo ya Ruvu na Zigi, Mradi wa Kurejesha Ardhi Iliyoharibika na Kuongeza Usalama wa Chakula Katika Maeneo Kame ya Tanzania pamoja na Mpango wa kuandaa Shabaha ya kuzuia uharibifu wa ardhi ifikapo mwaka 2030.

“Zipo faida kadhaa ambazo nchi wanachama wananufaika ambazo ni pamoja na kujengewa uwezo kitaalam, kifedha na kupatiwa vitendea kazi kwa ajili ya kupambana na kuenea kwa hali ya jangwa na ukame.

“Hivyo, kwa kuwa mwanachama wa Mkataba huu, Serikali pia kupitia Ofisi ya Makamu wa Rais imefanya tafiti mbalimbali na kuandaa taarifa ambazo zinatoa uelekeo utakaonesha njia ya kupambana na kuenea kwa hali ya jangwa na ukame”amesema Bamwenzeki

Kwa upande wake Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Mitaji (UNCDF) Aine Mushi amesema Mkakati huo utakuja na ripoti ambayo itasaidia katika utekelezaji wake.

 Aidha, amesema kuwa upo umuhimu wa kuona namna gani mkakati unashirikisha wadau kutoka sekta mbalimbali zikiwemo mashirika yasiyo ya kiserikali na wadau wa maendeleo.

 “Tunapowashirikisha wadau hawa tutaweza kujua ni kwa namna gani tunaingia kwenye mfumo wa bajeti ya Serikali na kwa kiwango gani cha fedha tunaweza kutekeleza mkakati huu,” ameongeza  Mushi.

 

 

 

Next Post
Kamati ya Bunge yaishauri serikali changamoto ya kelele

Kamati ya Bunge yaishauri serikali changamoto ya kelele

CCM:Mvomero ni maarufu kwa migogoro ya ardhi

CCM:Mvomero ni maarufu kwa migogoro ya ardhi

Serikali yaombwa kupunguza kodi kwenye dawa

Serikali yaombwa kupunguza kodi kwenye dawa

Discussion about this post

Contact us:

BAJETI COMMUNICATION

info@bajeti.co.tz
bajetinews@gmail.com
+255718699828
P.o.BOX 18133,
DAR ES SALAAM,
TANZANIA

Category

  • Habari
  • Magazeti
  • Makala
  • Mazingira
  • Michezo
  • Picha
  • Sayansi na Teknolojia
  • Siasa

Our Visitors

  • Today's visitors:1
  • Today's page views 1
  • Total visitors 13,057
  • Total page views 14,802

Kuhusu Tovuti Hii

Hii ni tovuti ya habari iliyojikita katika kuandika  habari za kina   zikiwemo za mazingira kwa lengo la kuelimisha na kuuhabarisha umma.

Subscribe

  • About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact

© 2025 Bajeti

No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo

© 2025 Bajeti

Welcome Back!

Login to your account below

Forgotten Password?

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In