• About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact
Thursday, January 22, 2026
  • Login
Bajeti
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo
No Result
View All Result
Bajeti
No Result
View All Result
Home Mazingira

CCM:Mvomero ni maarufu kwa migogoro ya ardhi

by bajeti
January 30, 2023
in Mazingira
0
CCM:Mvomero ni maarufu kwa migogoro ya ardhi

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM),Daniel Chongolo, akishiriki Ujenzi wa Ofisi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Tawi la Kibaoni Januari 29,2023 lililopo Kata ya Melela wilayani Mvomero Mkoa wa Morogoro wakati wa ziara ya kukagua uhai na utekelezaji wa Ilani ya chama hicho ikiwemo kusikiliza kero za wananchi(Picha na CCM)

Share on FacebookShare on Twitter

NA MWANDISHI WETU,MOROGORO

KATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi(CCM) Daniel Chongolo amesema Wilaya ya Mvomero mkoani Morogoro ni maarufu kwa migogoro ya ardhi na kuwataka viongozi wa ngazi zote kuhakikisha wanatatua hali hiyo kwenye maeneo wanayoyasimamia kiutawala.

Amesema lengo la CCM  na Serikali kwa ujumla ni kuona changamoto za wananchi zinapatiwa majawabu hivyo hawawezi kuwa na viongozi wanaosababisha mgogoro kila siku hivyo lazima wafanye maamuzi na wasimamie wanayoyaamua

Akizungumza  na Wananchi pamoja na Wanachama wa chama hicho Januari 29,2023 katika Kata ya Dakawa wilayani Mvomero Mkoa wa Morogoro, Chongolo amesema Serikali inayoongozwa na CCM inaendelea kuchukua  hatua mbalimbali katika kutatua changamoto zinazowakabili wananchi kwenye maeneo husika huku akieleza changamoto kubwa kwenye wilaya ya Mvomero ni migogoro ya ardhi.

“Mimi na wenzangu tumekuja Mvomero kwa ajili ya kuzungumza na wananchi, kusalimiana na kusikiliza changamoto zao,nimepewa changamoto ya migogoro ya ardhi kati ya Kijiji na Kijiji, Kata na Kata na maeneo ya kiutawala na changamoto hizi mara nyingi zinasababishwa na viongozi ambao wanaongeza maeneo ili kupata kura na baadae anaacha kero kwa wananchi.

“Sisi viongozi ndio wenye jukumu la kutatua changamoto ,Sheria ya nchi iko wazi kwa sababu hakuna kijiji kisicho na mpaka kwani maeneo yote yameanishwa , ukiona kuna shida ya kijiji na kijiji uje viongozi wenyewe ndio wanashida,nimeona nianze na hilo kwasababu Mvomero ni maarufu kwa migogoro ya ardhi.”Amesema Chongolo

Chongolo ameongeza  kuwa ni lazima viongozi waamue  kumaliza changamoto ambazo hazina haja ya kulelewa kwa muda mrefu ikiwemo changamoto ya mipaka ya kiutawala iwe ngazi ya Kijiji Kata,Wilaya  na Mkoa , na linawezekana kama viongozi watakubali.

Aidha amebainisha kuwa kumekuwepo na utaratibu wa kuweka mipango ya matumizi bora ya ardhi kwa kutenga maeneo kwa ajili ya makazi, kilimo na ufugaji lakini bado kumekuwa kukiibuka changamoto na kueleza kuwa wakulima wakipewa eneo wanalima hao hao lakini mfugaji akipewa eneo la mifugo anaalika na wenzake baada ya miezi sita anahangaika kutafuta malisho.

“Sababu mkulima hajaalika wengine kuja kulima kwenye shamba lake lakini mfugaji amealika na wenzake, hii mialiko kuna wanaosaidia kuifanikisha , ng’ombe haruki kama njiwa , lazima atembee anakopita kuna viongozi na wanaona, hatuwezi viongozi tunakuja kila siku tunaambiwa mgogoro wa wakulima , mgogoro wa wafugaji”amesema Chongolo.

Next Post
Serikali yaombwa kupunguza kodi kwenye dawa

Serikali yaombwa kupunguza kodi kwenye dawa

Jafo aipa wiki mbili Kampuni ya SUMA JKT

Jafo aipa wiki mbili Kampuni ya SUMA JKT

Watakaokaidi uchafuzi wa mazingira unaotokana na kelele,mitetemo kufungiwa

Watakaokaidi uchafuzi wa mazingira unaotokana na kelele,mitetemo kufungiwa

Discussion about this post

Contact us:

BAJETI COMMUNICATION

info@bajeti.co.tz
bajetinews@gmail.com
+255718699828
P.o.BOX 18133,
DAR ES SALAAM,
TANZANIA

Category

  • Habari
  • Magazeti
  • Makala
  • Mazingira
  • Michezo
  • Picha
  • Sayansi na Teknolojia
  • Siasa

Our Visitors

  • Today's visitors:17
  • Today's page views 17
  • Total visitors 13,276
  • Total page views 15,024

Kuhusu Tovuti Hii

Hii ni tovuti ya habari iliyojikita katika kuandika  habari za kina   zikiwemo za mazingira kwa lengo la kuelimisha na kuuhabarisha umma.

Subscribe

  • About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact

© 2025 Bajeti

No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo

© 2025 Bajeti

Welcome Back!

Login to your account below

Forgotten Password?

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In