NA MWANDISHI WETU
SERIKALI imeombwa kupunguza kodi katika dawa zinazotibu magonjwa mbalimbali ya binadamu ili kuruhusu wananachi wengi kuzipata gharama nafuu.
Hata hivyo licha ya juhudi kubwa za serikali katika kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora za afya lakini baadhi ya magonjwa yamekuwa na gharama kubwa za matibabu ikiwemo dawa zinazotumika kuyatibu ama kupunguza makali ya magonjwa hayo.
Akizungumza jijini Dar es Salaam Januari 30,2023 wakati wa hafla iliyoandaliwa na Kampuni ya SuperLife na kuwakutanisha Viongozi wa Dini,Serikali na Siasa,Mwenyekiti wa Taasisi ya Jai Juma Mwaipopo amesema pamoja na juhudi za serikali katika kutoa huduma nzuri za kiafya kwa watanzania lakini kuna baadhi ya magonjwa yana gharama kubwa ya dawa katika matibabu yake hivyo ni muhimu kuangalia suala hilo ili kuruhusu watu wengi kupata dawa bora za matibabu.
Mwaipopo amesema anatambua juhudi za serikali katika kuhakikisha huduma bora za afya zinaboreka katika ngazi ya Kituo cha Afya,Zahanati na Hospitali lakini hilo la gharama za dawa ni muhimu kuangaliwa vizuri.
“Maisha mengi ya Jamii yetu kwa asilimia kubwa yanategemea afya hivyo niiombe serikali iangalie jinsi ya kupunguza kodi katika dawa ili watu wengi wapate dawa kwa bei nafuu .
“Mfano kuna wajane,yatima na wengine ambao hata kula yao ya shida lakini wanamaradhi mengi yanayowasumbua ikiwemo kuugua figo hivyo kodi ikipunguzwa itasadia wananchi kupata dawa kwa gharama nafuu kwani kuna magonjwa ambayo dawa zinazotumika kuyatibu ni gharama kubwa hivyo wengine kuishia kukata tama na kubakia nyumbani kusubiri kifo”Amesema Mwaipopo
Mwaipopo ambaye pia ni Diwani Mstaafu wa Kata ya Ukonga ameongeza kuwa kwa hali ya sasa hakuna magonjwa ya kurithi kama zamani bali kila mtu sasa anaweza kuugua saratani,moyo,figo,presha na mengine mengi ikiwemo sukari ambapo zamani mengine waliugua watu wazima pekee.
Kwa upande wake Mshauri Mkuu wa SuperLife Lidia Katura amesema yeye amekuwa akitoa ushauri kwa wagonjwa wengi waliokata tamaa jinsi ya kupambana na magonjwa yanayowasumbua huku wakitumia dawa walizopewa hospitali hali iliyosaidia wengi wao kupona.
“Mimi kazi kubwa ni kushauri na kumfariji mgonjwa yeyote hasa wale wanaougua magonjwa ambayo huwakatisha tamaa ya kupona hivyo huwarudishia matumani na wakati mwingine huku wakipata matibabu ya hospitali nasi huwashauri kama watapenda basi wanaweza kutumia dawa ambazo Kampuni yetu inazo kutumia”Amesema Katura
Awali akizungumza katika hafla hiyo,Mkurugenzi wa SuperLife Emmanuel Oligi amesema wao wamefuata taratibu zote zinazohitajika na Serikali katika kuhakikisha kuwa wanatoa huduma bora kwa jamii kwa kuwa asilimia kubwa ya mwili wa binadamu ni seli hivyo wao wamejikita katika hilo.




Discussion about this post