• About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact
Saturday, May 2, 2026
  • Login
Bajeti
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo
No Result
View All Result
Bajeti
No Result
View All Result
Home Mazingira

Jafo aipa wiki mbili Kampuni ya SUMA JKT

by bajeti
February 3, 2023
in Mazingira
0
Jafo aipa wiki mbili Kampuni ya SUMA JKT

Sehemu ya jengo la Ofisi ya Makamu wa Rais ikiwa katika hatua ya ujenzi baada ya kutembelewa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Dkt. Selemani Jafo Februari Mosi, 2023.(Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)

Share on FacebookShare on Twitter

NA MWANDISHI WETU,DODOMA

WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Dkt. Selemani Jafo  ametoa wiki mbili kwa mkandarasi Kampuni ya SUMA JKT  kuhakikisha wanakamilisha kazi katika jengo la Ofisi ya Makamu wa Rais.

Jafo ametoa kauli hiyo Februari Mosi,2023 jijini Dodoma  baada ya kukagua ujenzi wa jengo la Ofisi ya Makamu wa Rais unaoendelea katika eneo la Mtumba .

Jafo ambaye aliambatana na viongozi na wataalamu kutoka Ofisi hiyo ameonesha kutoridhishwa na kasi ya ujenzi wa jengo hilo na kumtaka mkandarasi kuongeza kasi.

Kwa mujibu wa mpango kazi uliowekwa, kazi ya ujenzi huo kwa ujumla iko nyuma kwa siku 41 hali inayotokana na kasi ya ujenzi wa jengo hilo kutokuwa ya kuridhisha.

Kutokana na hali hiyo Dkt. Jafo ametoa wiki mbili kwa mkandarasi Kampuni ya SUMA JKT pamoja Msimamizi Elekezi Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) kuhakikisha wanakamilisha kazi ya kusiliba (plasta) kuta ambayo ilipaswa kuwa imekamilika.

Amesema kuwa pamoja na kuwa wameaminiwa na kupewa dhamana ya ujenzi wa jengo hilo la Serikali lakini haijaonesha umakini katika utekelezaji wa mradi huo.

“Hapa mko nyuma sana wenzenu kule wako mbali sana kuliko ninyi na mara ya mwisho tulipokutana mkaniambia kazi itaenda kwa kasi lakini ndio mkaamua kabisa kusimama na mmeanza tena kufanya baada ya kusikia ninakuja kukagua, hapa naona hakuna userious katika kufanya hii kazi,” ameeleza  Dkt. Jafo.

Aidha amebainisha kuwa Serikali haitavumilia kuona kazi hiyo ya ujenzi wa jengo la Ofisi ya Makamu wa Rais inakwama na kuonya kuwa kama hawataonesha maendeleo mkataba utavunjwa ili apewe mkandarasi mwingine atakayefanya kazi hiyo.

Katika ziara hiyo, Waziri Jafo pia alitembelea majengo mengine yanayojengwa na SUMA JKT na kubaini ujenzi wake unakwenda kwa kasi hivyo akaonya kuchukua hatua ya kuvunja mkataba.

Ofisi ya Makamu wa Rais ilisaini mkataba wa Sh. Bilioni 18.8 na Kampuni ya ujenzi ya SUMA JKT Oktoba 13, 2021  na kutakiwa kukamilisha kazi hiyo Novemba 09, 2023 na kutakiwa kukamilisha ujenzi huo uwe wa haraka kwa kuzingatia ubora, viwango na kasi.

 

Next Post
Watakaokaidi uchafuzi wa mazingira unaotokana na kelele,mitetemo kufungiwa

Watakaokaidi uchafuzi wa mazingira unaotokana na kelele,mitetemo kufungiwa

Kikosi cha KMKM chatakiwa kuongeza nguvu kudhibiti vitendo vya uhalifu baharini

Kikosi cha KMKM chatakiwa kuongeza nguvu kudhibiti vitendo vya uhalifu baharini

Mwaipopo:Rais Samia Suluhu Hassan muda unakuruhusu kutwaa tuzo ya Mo Ibrahim

Mwaipopo:Rais Samia Suluhu Hassan muda unakuruhusu kutwaa tuzo ya Mo Ibrahim

Discussion about this post

Contact us:

BAJETI COMMUNICATION

info@bajeti.co.tz
bajetinews@gmail.com
+255718699828
P.o.BOX 18133,
DAR ES SALAAM,
TANZANIA

Category

  • Habari
  • Magazeti
  • Makala
  • Mazingira
  • Michezo
  • Picha
  • Sayansi na Teknolojia
  • Siasa

Our Visitors

  • Today's visitors:9
  • Today's page views 9
  • Total visitors 16,034
  • Total page views 18,192

Kuhusu Tovuti Hii

Hii ni tovuti ya habari iliyojikita katika kuandika  habari za kina   zikiwemo za mazingira kwa lengo la kuelimisha na kuuhabarisha umma.

Subscribe

  • About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact

© 2025 Bajeti

No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo

© 2025 Bajeti

Welcome Back!

Login to your account below

Forgotten Password?

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In