NA MWANDISHI WETU
RAIS Samia Suluhu Hassan ameshauriwa kuongeza nguvu katika kuboresha maisha ya watanzania ili kujiandaa kupokea tuzo ya Bilionea Mo Ibrahim kwa kuwa muda unamruhusu kutekeleza yanayohitajika.
Hata hivyo Rais Samia amepongezwa kwa maamuzi yake magumu ya kuruhusu mikutano ya vyama vya siasa ambayo ilizuiwa kwa zaidi ya miaka sita.
Tuzo ya Mo Ibrahim hutolewa na Wakfu wa Mfanyabishara raia wa Uingereza mwenye asili ya Sudan Mo Ibrahim aliyeianzisha mwaka 2007 kwa ajili ya kuwatunukia viongozi walioonesha kazi nzuri wakati wa kipindi cha uongozi wao ndani ya Bara la Afrika, ambalo Viongozi wasiofuata utawala bora wamerudisha nyuma maendeleo yake.
Akizungumza Februari 6,2023 jijini Dar es Salaam na waandishi wa habari Februari 5,2023 jijini Dar es Salaam na Mwenyekiti wa Taasisi ya Jai inayojishughulisha na utoaji wa misaada kwa watu wenye matatizo wakiwemo Yatima,Walemavu na Wajane, Juma Mwaipopo wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu tuzo ya Mo Ibrahim kupokelewa Tanzania.
Amesema yeye anamshukuru Rais Samia kwa uamuzi mgumu ambao pengine inawezekana hata chama chake cha Mapinduzi hakikupenda jambo hilo lakini kwa kuwa yeye ni Mwenyekiti wao hawawezi kumpinga.
“Kuna maeneo ambayo kama uboreshaji wa maisha ya wananchi,kupatikana kwa Katiba Mpya,kushughulikia mifumo ya haki kama mahakama,polisi ambapo ikiwa haya atatimiza vizuri bila vikwazo kutoka ndani ya chama chake basi naamini tuzo ya Mo Ibrahim itatua Tanzania.
“Kuruhusu mikutano ya kisiasa pekee imemletea Rais Samia heshima kubwa duniani kwani viongozi wengi wa Afrika hawapendi kukoselewa bali wanataka kusifiwa lakini pia kwa kuruhusu mikutano hiyo kutasaidia zaidi kujua shida zinazowakabiliwa wananchi na kujua wanataka nini”amesema Mwaipopo
Mwaipopo ambaye ni Diwani Mstaafu wa Kata ya Ukonga ameongeza kuwa Rais Samia bado ana muda wa kuyatekeleza mambo muhimu ikiwemo upatikanaji wa Katiba Mpya atasaidia kuongeza idadi ya wanawake watakaopokea Tuzo ya Mo Ibrahim baada ya aliyekuwa Rais wa zamani wa Liberia Hellen Johnson SerLeaf
Marais wengine waliopokea tuzo hiyo ni pamoja na Thabo Mbeki wa Afrika Kusini, Olusegun Obasanja wa Nigeria na John Kufuor wa Ghana.
Wengine ni aliyekuwa Rais wa Botswana Festus Mogae alishinda zawadi hiyo mwaka 2008 baada ya kukaa madarakani kwa mihula miwili katika nchi hiyo yenye matukio machache ya rushwa na yenye maendeleo.
Hata hivyo Rais wa Niger Mahamadou Issoufou alishinda Tuzo ya Wakfu wa Mo Ibrahim ya 2020 kwa Mafanikio katika Uongozi wa Afrika. Na ameingia katika rekodi hiyo kama mshindi wa sita wa tuzo hio inayotambua uongozi bora Afrika.
Kamati ya tuzo hiyo katika taarifa yake iliusifu uongozi wa kipekee wa Rais Issoufou baada ya kurithi taifa lenye uchumi duni zaidi ulimwenguni, unaokabiliwa na changamoto ngumu zinazoonekana.
Katika miaka yake 10 kama Rais, Niger imefanya maendeleo katika maeneo mengi, pamoja na kuboresha sekta zote za Maendeleo ya Binadamu.
Katika uongozi wake Niger ilishika nafasi 28 kati ya nchi 54 katika faharasa ya Mo Ibrahim kuhusu utawala bora Afrika, na ilitajwa kuwa kati ya nchi 10 za Kiafrika zilizoboreshwa zaidi katika kuimarisha fursa za kijamii na kiuchumi kwa wanawake.
Katika kipindi chote cha kazi yake, Issoufa alijikita katika kukuza uchumi, kujitolea bila kutetereka kupigania utulivu wa kikanda na kikatiba pamoja na kupigania demokrasia ya Afrika.
Mwaka 2011, Rais Mtaafu wa Cape VerdePedro Pires kuwa mshindi wa tuzo ya utawala bora ,kutokana na mafanikio yake katika kuleta demokrasia,uimara na neema katika kisiwa cha Cape Verde.
Kamati ya Wakfu wa Mo Ibrahim ilisema katika uongozi wake wa miaka 10 katika kisiwa cha Rasi ya Verde, kwenye Pwani ya Magharibi mwa Afrika ,Pedro Verona Pires aliweka msingi wa kuwaondoa wananchi wake 200,000 kutoka kwenye umasikini.
Kutokana na utawala wake bora Pires alitambulika duniani kwa sera zake za kutekeleza haki za binadamu.
2015 Rais Mstaafu wa Namibia Hifikepunye Pohamba alishinda tuzo ya Mo Ibrahim kwa mwaka 2014 baada ya kipindi cha utawala wake kuwa na vigezo vyote vinavyostahiki
Mshindi wa kwanza wa tuzo hiyo alikuwa Joaquim Chissano, aliyekuwa Rais wa Msumbiji, ambaye tangu wakati huo alikuwa mpatanishi wa migogoro katika nchi mbalimbali za Afrika.
Washindi hupokea dola za kimarekani Milioni tano kwa zaidi ya miaka 10 na kupata dola za kimarekani 200,000 kwa mwaka mpaka atakapoaga dunia.




Discussion about this post