• About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact
Thursday, May 21, 2026
  • Login
Bajeti
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo
No Result
View All Result
Bajeti
No Result
View All Result
Home Habari

Serikali yabaini matishio 459 ya kiusalama mtandaoni

by bajeti
February 11, 2023
in Habari
0
Serikali yabaini matishio 459 ya kiusalama mtandaoni

Naibu Waziri Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Deogratius Ndejembi

Share on FacebookShare on Twitter

NA MIRIAM SARAKIKYA,ARUSHA

SERIKALI imebaini  matishio 459 ya kiusalama  mtandao ambapo pia imejipanga kuongeza watumiaji wa interneti kutoka asilimia 43 iliyopo sasa hadi kufikia asilimia 80 ifikapo mwaka 2025.

Hayo yamebainishwa jijini Arusha Februari 8,2023 wakati wa kikao kazi cha tatu cha Serikali Mtandao (ega) kilichohudhuriwa na Naibu Waziri Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Deogratius Ndejembi

Akizungumza katika kikao hicho,Ndejembi Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan imejipanga kuongeza watumiaji wa interneti kutoka asilimia 43 iliyopo sasa hadi kufikia asilimia 80 ifikapo mwaka 2025

“Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu mwaka  2021 wakati akihutubia Bunge kwa mara ya kwanza, alieleza bayana kuwa serikali  itatoa kipaumbele kwenye matumizi ya TEHAMA hususani katika masuala ya utafiti na ubunifu Tehama ili kuwawezesha watanzania kupata huduma bora na kwa wakati kupitia mifumo ya TEHAMA”

“Kupitia TEHAMA Dunia hivi sasa imekuwa ni Kijiji hivyo pamoja na wigo huo pia imejipanga kuongeza kasi ya kufikisha miundombinu ya Mkongo wa Taifa kwenye maeneo mengi nchini ikiwemo ngazi za wilaya.

“Tunaitaka Mamlaka ya Serikali Mtandao (ega) kuendelea kufanya tafiti ili kubuni mifumo mipya ya TEHAMA itayoliwezesha taifa kufanikisha kuimarisha sekta ya viwanda na biashara”ameeleza Ndejemi

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Mamlaka  ya Serikali Mtandao(ega)Mhandisi Benedict Ndomba amesema kikao hicho ni cha kipekee kwani ega imetimiza miaka10 na kufanikiwa kutekeleza majukumu mbalimbali ikiwemo kubaini matishio ya kiusalama  mtandao 459.

Mhandisi Ndomba amefafanua kuwa pamoja na kubaini matishio hayo ya kiusalama lakini pia imefanya ukaguzi na tathmini ya usalama wa mifumo kwa Taasisi za Umma.

Aidha ameongeza kuwa mamlaka hiyo imeendelea kusimamia na kuhimiza uzingatiaji Sera, Kanuni , Sheria  na miongozo  ya Serikali Mtandao kwa Taasisi za Umma ili kuhakikisha matumizi ya mfumo wa TEHAMA yanakuwa na tija na ufanisi.

Akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha,Mkuu wa Wilaya ya Arusha Felisia Mtahengerwa amebainisha  kuwa  Mkoa wa Arusha ni moja ya wadau wa Serikali Mtandao kupitia taasisi mbalimbali za umma ambapo wanapata huduma nyingi kwa njia rahisi ,gharama nafuu.

Next Post
CCM yawataka wanasiasa kudumisha amani na mshikamano

CCM yawataka wanasiasa kudumisha amani na mshikamano

Bilioni 120  kutumika miradi ya uhifadhi wa mazingira na mabadiliko ya tabianchi

Bilioni 120 kutumika miradi ya uhifadhi wa mazingira na mabadiliko ya tabianchi

Mtambo achangia ujenzi Zahanati ya Kijiji Dondo

Mhandisi Mtambo:Kuwe na uwazi katika utoaji tenda za ujenzi

Discussion about this post

Contact us:

BAJETI COMMUNICATION

info@bajeti.co.tz
bajetinews@gmail.com
+255718699828
P.o.BOX 18133,
DAR ES SALAAM,
TANZANIA

Category

  • Habari
  • Magazeti
  • Makala
  • Mazingira
  • Michezo
  • Picha
  • Sayansi na Teknolojia
  • Siasa

Our Visitors

  • Today's visitors:18
  • Today's page views 23
  • Total visitors 16,332
  • Total page views 18,522

Kuhusu Tovuti Hii

Hii ni tovuti ya habari iliyojikita katika kuandika  habari za kina   zikiwemo za mazingira kwa lengo la kuelimisha na kuuhabarisha umma.

Subscribe

  • About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact

© 2025 Bajeti

No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo

© 2025 Bajeti

Welcome Back!

Login to your account below

Forgotten Password?

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In