• About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact
Thursday, January 22, 2026
  • Login
Bajeti
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo
No Result
View All Result
Bajeti
No Result
View All Result
Home Mazingira

Kamati ya Bunge yaishauri serikali changamoto ya kelele

by bajeti
February 3, 2023
in Mazingira
0
Kamati ya Bunge yaishauri serikali changamoto ya kelele

Mkurugenzi wa Mazingira Ofisi ya Makamu wa Rais Dkt. Andrew Komba akifafanua jambo wakati wa kikao cha kuwasilisha taarifa ya utekelezaji wa majukumu ya Ofisi ya Makamu wa Rais ya kipindi cha Julai 2022 hadi Desemba 2022 kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Sheria Ndogo katika Ofisi za Bunge jijini Dodoma Januari 24, 2023.(Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)

Share on FacebookShare on Twitter

NA MWANDISHI WETU,DODOMA

KAMATI ya Kudumu ya Bunge ya Sheria Ndogo imetoa wito kwa Serikali kutafutia ufumbuzi changamoto ya kelele ambayo imekuwa kero kwa wananchi katika maeneo mbalimbali nchini.

Hayo yamesemwa Januari 24,2023 jijini Dodoma na Makamu Mwenyekiti wa Kamati hiyo Ndogo Kilumbe Ng’enda wakati wa kikao cha kuwasilisha taarifa ya utekelezaji wa majukumu ya Ofisi ya Makamu wa Rais kuanzia Julai 2022 hadi Desemba 2022 mbele ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Sheria Ndogo.

Akitoa ufafanuzi wa hoja hiyo, Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Khamis Hamza Khamis amesema Serikali inaendelea kusimamia na kutoa elimu kuhusu Mwongozo wa Udhibiti wa Uchafuzi wa Mazingira utokanao na Kelele na Mitetemo.

Amesema mwongozo huo unalenga kuboresha usimamizi na udhibiti wa uchafuzi wa mazingira unaotokana na kelele na mitetemo kwa kuanisha namna ambavyo wadau mbalimbali wanatakiwa kushiriki katika kupunguza kero zitokanazo na kelele na mitetemo.

Akitoa ufafanuzi kuhusu malalamiko dhidi ya kelele na mitetemo ambazo zimekuwa zikilalamikiwa na wadau,Khamis amesema Ofisi ya Makamu wa Rais kupitia Baraza la Taifa la Usimamizi wa Mazingira (NEMC) inaendelea kusimamia utekelezaji wa mwongozo huo.

“Mtakumbuka mwaka 2021 tulikutana na wizara mbalimbali zinazohusika tukawa na kikao na tukatoa tamko la la pamoja yote haya ni kuhakikisha tunasimamia ipasavyo mwongozo huu ili wananchi waepuke na adha ya kelele hizo,” amesema Khamis.

Malengo Mahsusi ya Mwongozo huu ni pamoja na  Kuainisha wajibu wa kila mdau katika kudhibiti kelele na mitetemo, Kubainisha na kupendekeza mifumo itakayosaidia kupunguza kero zitokanazo na kelele na mitetemo pamoja na Umuhimu wa Kuandaa Mwongozo

Next Post
CCM:Mvomero ni maarufu kwa migogoro ya ardhi

CCM:Mvomero ni maarufu kwa migogoro ya ardhi

Serikali yaombwa kupunguza kodi kwenye dawa

Serikali yaombwa kupunguza kodi kwenye dawa

Jafo aipa wiki mbili Kampuni ya SUMA JKT

Jafo aipa wiki mbili Kampuni ya SUMA JKT

Discussion about this post

Contact us:

BAJETI COMMUNICATION

info@bajeti.co.tz
bajetinews@gmail.com
+255718699828
P.o.BOX 18133,
DAR ES SALAAM,
TANZANIA

Category

  • Habari
  • Magazeti
  • Makala
  • Mazingira
  • Michezo
  • Picha
  • Sayansi na Teknolojia
  • Siasa

Our Visitors

  • Today's visitors:18
  • Today's page views 18
  • Total visitors 13,277
  • Total page views 15,025

Kuhusu Tovuti Hii

Hii ni tovuti ya habari iliyojikita katika kuandika  habari za kina   zikiwemo za mazingira kwa lengo la kuelimisha na kuuhabarisha umma.

Subscribe

  • About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact

© 2025 Bajeti

No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo

© 2025 Bajeti

Welcome Back!

Login to your account below

Forgotten Password?

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In