• About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact
Monday, May 25, 2026
  • Login
Bajeti
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo
No Result
View All Result
Bajeti
No Result
View All Result
Home Mazingira

Migogoro ya binadamu,wanyamapori yajeruhi watu zaidi ya 600 kati ya mwaka 2012-19

by bajeti
January 17, 2023
in Mazingira
0
Migogoro ya binadamu,wanyamapori yajeruhi watu zaidi ya 600 kati ya mwaka 2012-19

Mkurugenzi wa Chama cha Waandishi wa Habari za Mazingira Tanzania (JET) John Chikomo

Share on FacebookShare on Twitter

NA MWANDISHI WETU, PWANI

ZAIDI ya watu 600 wamejeruhiwa huku wengine 1,069 wakipoteza maisha  kufuatia migogoro kati ya wanadamu na wanyamapori katika maeneo mbalimbali nchini kuanzia mwaka 2012 hadi 2019.

Hayo yameelezwa Januari 12,2023 wilayani Bagamoyo Mkoa wa Pwani na Meneja Ufuatiliaji na tathmini wa Shirika la Marekani la USAID ,John Noronha  wakati akitoa mada katika mafunzo ya wanahabari kuhusu uhifadhi maliasili yaliyoendeshwa na Chama cha Waandishi wa Habari za Mazingira nchini (JET),

Noronha ametoa takwimu hizo wakati akitoa mada kuhusu migogoro kati ya wanadamu na wanyama, sababu matokeo na utatuzi wake.

“Migogoro ya binadamu na wanyapori inatokana na mwingiliano baina yao, inaweza kuwa na matokeo chanya au hasi.

“Tatizo bado lipo na takwimu zinaonyesha kuwa kati ya mwaka 2012 hadi 2019 nchini Tanzania watu 642 wamejeruhiwa  au kupata ulemavu kwa kujeruhiwa na wanyamapori na watu 1,069wamepoteza maisha” amesema Noronha.

Aidha ameongeza kuwa  katika kipindi hicho mifugo 792 iliuaawa na ekari 41,401 za mazao ziliharibiwa, huku takriban Sh.Bilioni 4.6 zikitumika kulipia fidia.

Akizungumzia Mradi wa USAID Tuhifadhi Maliasili, Noronha amebainisha kuwa  unaangalia mapitio ya wanyama (Shoroba)kwa ajili ya kuondoa changamoto zilizopo ili kuboresha makazi ya binadamu na wanyama.

“Pia tunalenga kuzijengea uwezo taasisi za kiserikali na zisizo za kiserikali kwa kuzipa fedha na vifaa, pamoja na kuboresha sera na sheria kutumia wataalam na vyanzo vya ndani.

“Mradi huu ulianza Juni 2021, hii ni awamu ya pili na itagharimu Sh. Bilioni 7.16) katika utekelezaji wake”amefafanua Noronho

Kwa upande wake Mkurugenzi wa JET, John Chikomo amesema elimu ya uhifadhi maliasili na mazingira wanayopewa waandishi wa habari wanaoifikisha kwa jamii inachagiza kuwepo kwa ongezeko la watalii nchini.

“Ongezeko la Tembo tunaloliona sasa limechangiwa na uhifadhi wa wanyamapori, tumeona mwaka 2022 watalii milioni 1.2 waliingia nchini na waandishi wamehusika kuelimisha jamii, zipo pia faida mbalimbali zinazotokana na uhifadhi ikiwemo pia ongezeko la watalii,”  amesema Chikomo

Amesema mafunzo hayo kwa wanahabari 25 wa Tanzania Bara na visiwani ni sehemu ya Mradi wa Tuhifadhi Maliasili, ambao unatekelezwa na Shirika la RTI likishirikiana na JET chini ya ufadhili wa Shirika la USAID.

Next Post
Mtama wapandwa anga za juu kukabili mabadiliko tabianchi.

Mtama wapandwa anga za juu kukabili mabadiliko tabianchi.

JET  yawataka waandishi wa habari kujikita katika uhifadhi wa maliasili,mapito ya wanyamapori(Shoroba)

JET yawataka waandishi wa habari kujikita katika uhifadhi wa maliasili,mapito ya wanyamapori(Shoroba)

Dkt Mpango ataka wezi na wanaochepusha maji kutoka kwenye mito bila vibali kuchukuliwa hatua

Dkt Mpango ataka wezi na wanaochepusha maji kutoka kwenye mito bila vibali kuchukuliwa hatua

Discussion about this post

Contact us:

BAJETI COMMUNICATION

info@bajeti.co.tz
bajetinews@gmail.com
+255718699828
P.o.BOX 18133,
DAR ES SALAAM,
TANZANIA

Category

  • Habari
  • Magazeti
  • Makala
  • Mazingira
  • Michezo
  • Picha
  • Sayansi na Teknolojia
  • Siasa

Our Visitors

  • Today's visitors:26
  • Today's page views 30
  • Total visitors 16,480
  • Total page views 18,695

Kuhusu Tovuti Hii

Hii ni tovuti ya habari iliyojikita katika kuandika  habari za kina   zikiwemo za mazingira kwa lengo la kuelimisha na kuuhabarisha umma.

Subscribe

  • About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact

© 2025 Bajeti

No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo

© 2025 Bajeti

Welcome Back!

Login to your account below

Forgotten Password?

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In