• About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact
Thursday, January 22, 2026
  • Login
Bajeti
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo
No Result
View All Result
Bajeti
No Result
View All Result
Home Makala

Upatikanaji wa Kaboni utakavyosaidia kulinda mazingira ,afya za wachimbaji wadogo wa dhahabu

by bajeti
March 26, 2023
in Makala
0
Upatikanaji wa Kaboni utakavyosaidia kulinda  mazingira ,afya za wachimbaji wadogo wa dhahabu

Waandishi wa Habari na Watafiti wakimsikiliza Mtafiti na Mbunifu wa Kaboni inayotokana na vifuu vya nazi Tiberius Mario Machi 8,2023 katika eneo la kiwanda chake kilichopo Goba jijini Dar es salaam jinsi kaboni anayozalisha inavyoweza kutumika katika migodi ya uchimbaji madini na kulinda mazingira.(Picha na Goodluck Hongo)

Share on FacebookShare on Twitter

NA GOODLUCK HONGO

SEKTA ya wachimbaji wadogo wa dhahabu nchini inatoa ajira za moja kwa moja kwa zaidi ya watu Milioni 1.2

Kati ya hizo ajira zisizo za moja kwa moja zinawahusu watu Milioni 7.2 ikiwa ni sawa na asilimia 13 ya idadi ya watu nchini.

Tathmini hiyo inaonesha kuwa wachimbaji wadogo wa dhahabu  hutumia kiasi cha tani 13.2 na 24.4 ya  Zebaki  kwa mwaka ambapo matumizi yasiyo salama ya kemikali hiyo husababisha athari kwa afya ya binadamu na mazingira.

Hata hivyo Mtafiti na Mbunifu wa Kaboni inayotokana na vifuu vya nazi  Tiberius Mario ameomba kiasi  cha Sh.Milioni 36 ili aweze kuongeza uzalishaji utakaowasaidia wachimbaji wadogo wa dhahabu kuacha kutumia kemikali hatari ya Zebaki kuchenjulia madini ya dhahabu.

Kugundulika kwa Kaboni hiyo kutasadia Mpango Kazi wa Serikali wa 2020-2025 wa kukabiliana na matumizi ya kemikali hatari ya Zebaki ambayo ina madhara makubwa kwa afya za binadamu na mazingira yake.

Kemikali hiyo ambayo inatajwa na Shirika la Afya Duniani (WHO) kama mojawapo ya magonjwa 10 hatari duniani  inadaiwa kuharibu ubongo na mfumo wa mishipa ya fahamu, figo,kuzaliwa watoto wenye ulemavu,kupoteza kumbukumbu ikiwemo kushindwa kupumua ambayo  imekuwa ikiingizwa nchini kwa kificho huku watumiaji wakubwa ni wachimbaji wadogo wanayoitumia bila kufuata utaratibu wake.

Katika Mpango-Kazi wa Taifa wa Kupunguza Matumizi ya Zebaki kwa Wachimbaji Wadogo wa Dhahabu kwa mwaka 2020-2025 ambao umeandaliwa na Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira unaonesha kuwa tani 24 za kemikali hatari ya Zebaki hutumika kwa mwaka katika shughuli za uchenjuaji wa dhahabu nchini ambapo wachimbaji wadogo   ndio watumiaji wakubwa.

Mpango-Kazi  huo umekuja baada ya Jumuia ya Kimataifa mnamo mwaka 2013 kupitisha Mkataba wa unaojulikana kama MINAMATA  wenye madhumuni ya kulinda afya ya binadamu dhidi ya madhara ya uchafuzi wa mazingira unaotokana na Zebaki.

Hata hivyo kutokana na Serikali kuona umuhimu wa kulinda afya za watanzania na mazingira kwa ujumla iliuridhia mkataba huo na kuusaini rasmi mwaka 2020.

Mpango-Kazi huo unabainisha kuwa wachimbaji wadogo huchenjua dhababu kwa kutumia mbinu ambazo huhatarisha afya za binadamu na mazingira.

Aidha unaeleza kuwa shughuli za wachimbaji wadogo wa dhahabu zimekuwepo nchini kwa zaidi ya miaka 100 huku tathmini ikionesha kuwa takribani tani 13.2 hadi 24.4 za Zebaki hutumika kwa mwaka katika shughuli za uchenjuaji wa dhahabu huku Mkoa wa Geita ukiongoza kwa kutumia tani 4,480 kwa mwaka.

“Uchomaji holela wa dhahabu,uchenjuaji wa dhahabu karibu na maeneo ya makazi na vyanzo vya maji na uchenjuaji wa marudio yenye Zebaki kwa kutumia sayanadi kunachangia zaidi uchafuzi wa mazingira.

“Tafiti kadhaa zimefanyika katika maeneo mbnalimbali ya wachimbaji wadogo wa dhahabu ,zimebainisha athari za Zebaki kwa afya ya binadamu na mazingira,inakadiriwa kuwa asilimia 25 hadi 33 ya wachimbaji wa dhahabu hapa nchini wameathiriwa na Zebaki.

“Tafiti hizo zinabainisha kuwa baadhi ya wachimbaji wadogo wa dhahabu wana kiwango kikubwa cha Zebaki katika miili yao hadi mara 13 zaidi ya kiwango kinachokubalika na Shirika la Afya Duniani (WHO) hivyo kuashiria uwepo wa changamoto za kiafya zinazotokana na Zebaki katika maeneo ya wachimbaji wadogo wa dhahabu”unafafanua Mpango Kazi huo.

Hata hivyo lengo la Mpango-Kazi huo ni kupunguza na pale inapowezekana kuondosha matumizi ya Zebaki katika shughuli za Wachimbaji Wadogo wa Dhahabu ili kulinda afya za wananchi na mazingira.

Katika Mpango-Kazi wa Taifa wa Kupunguza Matumizi ya Zebaki kwa Wachimbaji Wadogo wa Dhahabu 2020-2025 uliozinduliwa Mwezi Juni 2020  unazitaja Taasisi 30 za Serikali zinazotakiwa kushiriki kikamilifu na kila moja  ikiwekewa jukumu lake.

Mpango-Kazi huo unabainisha jukumu la Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) kuwa ni kuratibuna kusimamia tafiti za teknolojia mbadala wa Zebaki na kusambaza teknolojia husika katika maeneo ya wachimbaji wadogo huku vyombo vya habari vikiwa na jukumu la kutoa elimu kwa umma kuhusu masuala ya Zebaki na madhara ya kiafya yatokanayo na matumizi ya kemikali hiyo.

Pamoja na jitihada hizo za Serikali za kulinda afya za watanzania ikiwemo kuwajengea makaro kuzuia maji yenye kemikali hiyo kutosambaa kwa kuingia mtoni au kusambazwa na maji ya mvua lakini bado kuna changamoto ya matumizi mbadala wa kemikali hiyo katika matumizi ya uchimbaji wa  madini  hasa kwa wachimbaji wadogo.

Hata hivyo COSTECH  inayoongozwa na Mkurugenzi wake Dkt.Amos Nungu imeonesha jukumu lake katika kutekeleza kikamilifu Mpango-Kazi huo wa Taifa baada ya kufuatilia na kuitambua rasmi Bunifu ya Mtafiti Mtanzania Tiberius Mario ya kutumia vifuu vya nazi kuzalisha Kaboni ambayo inakwenda kuwa mbadala wa matumizi ya kemikali hatari ya Zebaki.

Kaboni hiyo ya Mario imemfanya kuwa mshindi wa kwanza katika Mashindano ya Kitaifa ya Ubunifu,Sayansi na Teknolojia (MAKISATU) kwa mwaka 2022 jijini Dodoma na kupata fursa ya kupewa zawadi na Makamu wa Rais Dkt.Philip Mpango na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa.

Akizungumza Machi 8,2023 mbele ya waandishi wa habari na watafiti jijini Dar es Salaam wakati wa Mafunzo ya Uandishi wa Habari za Sayansi,Teknolojia na Ubunifu kati ya waandishi wa habari na watafiti yaliyoandaliwa na Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia  (COSTECH),Mario anasema Tanzania inauwezo wa kuokoa dola za kimarekani Milioni sita za kuagiza Kaboni kutoka nje ya nchi.

Amesema Tanzania ni nchi ya 16 duniani kwa kuzalisha nazi baada ya nchi kama Indonesia,India,Brazil na Ufilipino hivyo kuna kiwango kikubwa cha nazi na ni fursa pia kwa watanzania kujua kuwa vifuu vya nazi ni mali inayoweza kuzalisha Kaboni.

“Baada ya kumaliza Chuo nilianza kufanya utafiti wa kuzalisha Kaboni na ndipo nilipobuni uzalishaji kwa kutumia vifuu vya nazi na baada ya kupimwa na kuthibitishwa imeonekana kuwa na uwezo wa asilimia 98 kukamata madini yaliyopo katika udongo”anasema Mario

Anasema kila mgodi wa dhababu lazima uwe na Kaboni kwa ajili ya kusaidia kukamatisha dhababu na Tanzania inahitaji tani 1500 pekee za Kaboni ambazo asilimia kubwa huingizwa kutoka nje ya nchi.

Mario anaongeza kuwa pamoja na yeye kufanikiwa kuzalisha Kaboni kwa kutumia vifuu vya nazi ambapo baadhi ya maeneo katika jijini la Dar es Salaam tayari wameshazoea kumuuzia lakini gharama za uzalishaji ni kubwa.

Mario anabainisha kuwa amekuwa akitumia makaa yam awe katika kupata moto wenye uwezo wa kuunguza vifuu vya nazi hadi vinapokuwa havina moshi lakini uwezo alionao bado ni mdogo hivyo anahitaji msaada ili aweze kuzalisha kwa wingi na itumike katika migodi yote yenye wachimbaji wadogo.

“Nahitaji Milioni 36 ili niweze kuzalisha Kaboni ikiwemo kuwa na tanuri la kuchomea vifuu lakini mahitaji ya Kaboni yangu ni makubwa  katika migodi baada ya kupimwa katika maabara na kuthibitishwa inaweza kukamata dhahabu kwa asilimia 98 na tayari baadhi ya migodi nimeshaipelekea.

“Vifuu vya nazi ni dili na hakuna kutupa vifuu kwani tuna malighafi nyingi za kuzalisha Kaboni lakini bado nyingi inazalishwa nje ya nchi na kisha kuingizwa nchini ilihali malighafi zingine wanatoa hapa kwetu”anaongeza Mario

Aidha anafafanua kuwa mfuko mmoja wa kilo 25 wa Kaboni kutoka nje unauzwa hadi Sh.400,000 au 250,000 lakini kwa Kaboni yake anaiuza Sh.20,000 kwa kila kilo 25 japokuwa Sheria hairuhusu usafirishaji wa Kaboni kutoka sehemu moja kwenda nyingine lakini Tanzania ina malighafi nyingi kuliko mahitaji.

Hata hivyo  Mario anaongeza  kuwa pamoja na changamoto alizonazo katika kufanikisha ubunifu wake huo bado anaishukuru Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) kwa kumfikisha hapo alipo baada ya kutambua bunifu yake.

Hata hivyo Mario anategemea pia kutumia mabaki ya mbegu za chikichiki kuzalisha Kaboni kwa kuwa zao hilo nalo linalimwa Tanzania hivyo itasaidia pia kuondoa uchafu wa mabaki ya mbegu za Chikichi.

Waandishi wa habari na watafiti wakimsikiliza mbunifu wa Kaboni kwa kutumia vifuu vya nazi Tiberius Mario Machi 8,2023 jinsi Kaboni hiyo inavyoweza kutumika katika kuchuja maji yenye sumu na kutumika kuchenjulia dhahabu.(Picha na Goodluck Hongo)

“Sasa hivi nazalisha kilo 100 tu za Kaboni lakini mahitaji ni mengi lakini Kaboni ni dawa na sio sumu kwani hii ninayoitengeneza mimi inaweza kutunza mazingira kwa kuondoa uchafu wote kwenye maji,na inaweza kutumika katika kuondoa kemikali zilizopo katika udongo,maji na kazi zingine nyingi ikiwemo kufyonza dhahabu yote iliyopo katika udongo.

“Tanzania hatuna kiwanda cha kutengeneza Kaboni  na mimi nimekuja na teknolojia hii ya kutumia vifuu vya nazi kutengeneza Kaboni ambayo itasaidia pia kutunza mazingira kwa kuondoa uchafu mtaani unaotokana na kuzagaa kwa vifuu vya nazi,pia itasaidia afya kwa wananchi kwa kuondoa uchafu ambao unazalisha mbu mtaani wanaoleta ugonjwa wa Malaria,lakini pia inaondoa harufu kwenye maji.

“Nikifanikiwa kuzalisha kwa kiwango kikubwa basi Kaboni yangu itakwenda kutumika zaidi na wachimbaji wadogo wa dhahabu nchini na kuwasaidia kuondokana na matumizi ya Mecury(Zebaki) katika uchenjuaji wa dhahabu”anaeleza Mario.

Mtafiti na Mbunifu wa Kaboni kwa kutumia vifuu vya nazi Tiberius Mario (mwenye kofia) akiwa na Makamu wa Rais Dkt.Philip Mpango (wa tatu kulia),Waziri Mkuu Kassim Majaliwa (kushoto) na Waziri wa Elimu,Sayansi na Teknolojia Prof.Adolf Mkenda mara baada ya kuwa mshindi wa kwanza katika mashindano ya Ubunifu wa Sayansi na Teknolojia maarufu kama MAKISATU jijini Dodoma mwaka 2022.(Picha na COSTECH)

Kwa upande wake Mratibu wa Mafunzo ya Uandishi wa Habari za Sayansi,Teknolojia na Ubunifu kutoka COSTECH Deusideth Leoanaed amesema hayo ni mafunzo ya tisa kufanyika tangu mwaka 2015 ya kuwakutanisha Waandishi wa Habari,Watafiti na Wabunifu.

“Lengo ni kuwaleta pamoja na kubadilishana uzoefu ili tafiti nyingi ziweze kuandikwa kwa lugha rahisi,kupata ongezeko la uhawilishaji wa teknolojia kati ya Watafiti na Jamii  na kuwajengea uwezo waandishi wa habari ili waweze kuandika taarifa za Sayansi,Teknolojia na Ubunifu kama ilivyo katika maeneo mengine ikiwemo siasa na michezo”amesema Leonaed.

Mtafiti na Mbunifu wa Kaboni kwa kutumia vifuu vya nazi Tiberius Mario akiwaonesha waandishi wa habari aina ya mtambo anaoutumia kuzalishia kaboni hiyo(Picha na Goodluck Hongo)

 

Next Post
TARI:Mahitaji ya nazi ni makubwa nchini

TARI:Mahitaji ya nazi ni makubwa nchini

COSTECH yawafunda wanahabari kuhusu Sayansi,Teknolojia na Ubufuni

COSTECH yawafunda wanahabari kuhusu Sayansi,Teknolojia na Ubufuni

Mungano wa Tanganyika na Zanzibar ni kipekee duniani

Mungano wa Tanganyika na Zanzibar ni kipekee duniani

Discussion about this post

Contact us:

BAJETI COMMUNICATION

info@bajeti.co.tz
bajetinews@gmail.com
+255718699828
P.o.BOX 18133,
DAR ES SALAAM,
TANZANIA

Category

  • Habari
  • Magazeti
  • Makala
  • Mazingira
  • Michezo
  • Picha
  • Sayansi na Teknolojia
  • Siasa

Our Visitors

  • Today's visitors:18
  • Today's page views 18
  • Total visitors 13,277
  • Total page views 15,025

Kuhusu Tovuti Hii

Hii ni tovuti ya habari iliyojikita katika kuandika  habari za kina   zikiwemo za mazingira kwa lengo la kuelimisha na kuuhabarisha umma.

Subscribe

  • About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact

© 2025 Bajeti

No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo

© 2025 Bajeti

Welcome Back!

Login to your account below

Forgotten Password?

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In