• About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact
Tuesday, January 13, 2026
  • Login
Bajeti
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo
No Result
View All Result
Bajeti
No Result
View All Result
Home Habari

Mungano wa Tanganyika na Zanzibar ni kipekee duniani

by bajeti
March 26, 2023
in Habari
0
Mungano wa Tanganyika na Zanzibar ni kipekee duniani

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Dkt. Selemani Jafo akiwasilisha Taarifa ya Utekelezaji wa Bajeti ya Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano) kwa Mwaka wa Fedha 2022/2023 pamoja na Makadirio ya Matumizi ya Ofisi hiyo kwa Mwaka wa Fedha 2023/2024 kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala,Katiba na Sheria katika Ofisi za Bunge jijini Dodoma Machi 24, 2023.(Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)

Share on FacebookShare on Twitter

NA MWANDISHI WETU

WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Dkt. Selemani Jafo amesema Mungano wa Tanganyika na Zanzibar umeendelea kuimarika kutokana na upendo na mshikamano miongoni mwa wananchi na hivyo kuufanya uwe wa kipekee duniani.

Hata hivyo Dkt.Jafo amebainisha kuwa Ofisi ya Makamu wa Rais inatarajia kuanzisha kituo cha Kumbukumbu na Nyaraka za Muungano ili kutoa elimu kwa wananchi kuhusu faida za Muungano.

Dkt.Jafo ameyasema hayo Machi 24, 2023 jijini Dodoma wakati wa Kikao cha Kupokea na kujadili Taarifa ya Utekelezaji wa Bajeti ya Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano) kwa Mwaka wa Fedha 2022/2023 pamoja na Makadirio ya Matumizi ya Ofisi hiyo kwa Mwaka wa Fedha 2023/2024 kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria.

Amesema Serikali itafanya ufuatiliaji wa utekelezaji wa maagizo yaliyotolewa na Kamati ya Pamoja na yale masuala 22 ya Muungano kwa mujibu wa Katiba wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ili kuhakikisha utekelezaji unafanyika ipasavyo.

“Ofisi ya Makamu wa Rais kupitia wataalamu wetu itaendelea kutoa elimu kwa umma kuhusu Muungano na faida zake kwa jamii kupitia vyombo vya habari na maadhimisho mbalimbali.

“Aidha, ili kuboresha utoaji elimu kwa umma, Ofisi imeandaa Kitabu cha Historia ya Muungano kitakachotumika kuelimisha umma kuhusu faida za Muungano kiuchumi, kijamii na kiutamadun“ amesema Dkt.Jafo.

Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria  Joseph Mhagama pamoja na baadhi ya wajumbe wa kamati hiyo wamepongeza Ofisi ya Makamu wa Rais kwa taarifa nzuri.

Wamesema kuna umuhimu wa kutoa ufafanuzi kuhusu hoja za Muungano zilizotatuliwa ili wananchi wapate uelewa kuhusu mambo gani yaliyopata ufumbuzi kwa pande zote mbili za Muungano.

 

Next Post
Rais Dkt Samia:Sioni sababu kuminya uhuru wa habari

Rais Dkt Samia:Sioni sababu kuminya uhuru wa habari

BRELA yashukuru vyombo vya habari ongezeko usajili wa makampuni

BRELA yashukuru vyombo vya habari ongezeko usajili wa makampuni

Kiwango cha kuzaliana chashuka Japan,yashuhudia watoto chini ya 800,000 wazaliwa kwa mwaka

Kiwango cha kuzaliana chashuka Japan,yashuhudia watoto chini ya 800,000 wazaliwa kwa mwaka

Discussion about this post

Contact us:

BAJETI COMMUNICATION

info@bajeti.co.tz
bajetinews@gmail.com
+255718699828
P.o.BOX 18133,
DAR ES SALAAM,
TANZANIA

Category

  • Habari
  • Magazeti
  • Makala
  • Mazingira
  • Michezo
  • Picha
  • Sayansi na Teknolojia
  • Siasa

Our Visitors

  • Today's visitors:0
  • Today's page views 0
  • Total visitors 13,056
  • Total page views 14,801

Kuhusu Tovuti Hii

Hii ni tovuti ya habari iliyojikita katika kuandika  habari za kina   zikiwemo za mazingira kwa lengo la kuelimisha na kuuhabarisha umma.

Subscribe

  • About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact

© 2025 Bajeti

No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo

© 2025 Bajeti

Welcome Back!

Login to your account below

Forgotten Password?

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In