• About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact
Thursday, January 22, 2026
  • Login
Bajeti
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo
No Result
View All Result
Bajeti
No Result
View All Result
Home Habari

Rais Dkt Samia:Sioni sababu kuminya uhuru wa habari

by bajeti
March 29, 2023
in Habari
0
Rais Dkt Samia:Sioni sababu kuminya uhuru wa habari
Share on FacebookShare on Twitter

Exuperius Kachenje

RAIS Dkt.Samia Suluhu Hassan amewataka Wahariri wa Vyombo vya Habari nchini kufanya kazi kwa kuzingatia maadili ya taaluma ya habari na haoni sababu ya kuminya uhuru wa habari.

Hata hivyo amewataka pia kufanya kazi zao bila upendeleo wala kumuonea mtu ikiwemo kutoogopa wanapotekeleza majukumu yao ya kikazi.

Rais Dk. Samia ametoa rai hiyo Machi 29,2023 mjini Morogoro katika salam zake kwa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF’), linalofanya mkutano wake wa 12 wa mwaka wa kitaaluma.

Akitoa salam hizo za Rais mbele ya wahariri wa vyombo vya habari, Waziri wa Habari,Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye amesema Rais amemtuma awaambie kuwa wafanye kazi bila woga,kitaaluma na pasipo upendeleo wala kumuonea mtu.

Nape aliyekuwa mgeni rasmi katika ufunguzi wa mkutano huo alifafanua kuwa Rais Dkt. Samia aliwahi kumwambia wakati wa mchakato wa kupitia Sheria ya Habari kwamba wahakikishe hawaingilii haki ya watu kujieleza.

“Rais kanituma, waambie wafanye kazi bila woga, kitaaluma, bila upendeleo wala kumuonea mtu,haya ni maneno ya Rais mwenyewe.”amesema Nape

Amesema Rais Dkt.Samia ni muumini wa haki ya kujieleza na kutoa maoni hivyo haoni sababu ya kuminya uhuru wa habari.

Nape alivitaka vyombo ya habari kuandika habari za kiuchunguzi zenye lengo la kulisaidia taifa pamoja na wahariri kusaidia kurithisha weledi waandishi vijana hasa kwenye mitandao ya kijamii akieleza kuwa eneo hilo lina shida kidogo ya weledi.

Aidha ameongeza kuwa ingawa vyombo vya habari vinayumba kiuchumi kwa sababu mbalimbali ikiwamo kutolipwa madeni yanayofikia Sh.Bilioni 18, kuna madai ya wahariri na waandishi kwa vyombo hivyo kuwa hawalipwi mishahara.

“Tutavibana vyombo vishughulikiea maslahi ya wahariri na waandishi,” amesema Nape

Akizungumzia kuhusu alivyoshughulikia uvamizi wa kituo cha luninga na redio cha Clouds Media uliofanywa na aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda,Nape amebainisha kuwa wakati anajiandaa kuwasilisha ripoti hiyo, alizuiwa kufanya hivyo na mwajiri wake na kuagizwa ikiwa  ataitoa atapoteza ajira.

“Niliambiwa nisiendelee na uchunguzi au nitapoteza ajira, nikachagua heshima, lakini leo nipo hapa,” amesema Nape.

Mwezi Machi 2017 Makonda akiwa na askari polisi waliokuwa na bunduki aliingia katika ofisi za studio za redio na Televisheni ya Clouds majira ya saa 4:46 usiku  huku baadhi ya vipindi vikiwa vinaendelea kwa kuendeshwa na watangazaji wa zamu wa kipindi maarufu cha  Shilawadu kilichokuwa chini ya Mtangazaji ‘Soudy Brown’.

Naye Mwenyekiti wa TEF, Deodatus Balile alimshukuru Rais Dk.Samia Suluhu Hassan, Wizara ya Habari na watendaji wake kwa ushirikiano na vyombo vya habari unaowezesha ukuaji wa vyombo hivyo.

“Idadi ya kesi kwa vyombo vya habari imepungua, mwaka sasa hakuna shitaka jipya,hii ni ishara njema ya ukuaji vyombo vya habari, hata kimataifa tulikuwa wa 124 mwaka 2021 lakini  mwaka 2022 tumekuwa wa 12,”amesema Balile.
Hata hivyo, Balile aongeza kuwa pamoja na matumaini hayo mapya, hali ya uchumi wa vyombo vya habari si nzurii na kuikumbusha  Serikali deni  la takribani Sh.Bilioni 20 ambazo vyombo vya habari vinadai kwa wadau mbalimbali ikiwemo.

 

 

 

Next Post
BRELA yashukuru vyombo vya habari ongezeko usajili wa makampuni

BRELA yashukuru vyombo vya habari ongezeko usajili wa makampuni

Kiwango cha kuzaliana chashuka Japan,yashuhudia watoto chini ya 800,000 wazaliwa kwa mwaka

Kiwango cha kuzaliana chashuka Japan,yashuhudia watoto chini ya 800,000 wazaliwa kwa mwaka

Ekari Milioni 5.2 za Misitu kurejeshwa  ifikapo 2030

Ekari Milioni 5.2 za Misitu kurejeshwa ifikapo 2030

Discussion about this post

Contact us:

BAJETI COMMUNICATION

info@bajeti.co.tz
bajetinews@gmail.com
+255718699828
P.o.BOX 18133,
DAR ES SALAAM,
TANZANIA

Category

  • Habari
  • Magazeti
  • Makala
  • Mazingira
  • Michezo
  • Picha
  • Sayansi na Teknolojia
  • Siasa

Our Visitors

  • Today's visitors:18
  • Today's page views 18
  • Total visitors 13,277
  • Total page views 15,025

Kuhusu Tovuti Hii

Hii ni tovuti ya habari iliyojikita katika kuandika  habari za kina   zikiwemo za mazingira kwa lengo la kuelimisha na kuuhabarisha umma.

Subscribe

  • About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact

© 2025 Bajeti

No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo

© 2025 Bajeti

Welcome Back!

Login to your account below

Forgotten Password?

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In