• About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact
Tuesday, January 13, 2026
  • Login
Bajeti
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo
No Result
View All Result
Bajeti
No Result
View All Result
Home Habari

COSTECH yawafunda wanahabari kuhusu Sayansi,Teknolojia na Ubufuni

by bajeti
March 29, 2023
in Habari
0
COSTECH yawafunda wanahabari kuhusu Sayansi,Teknolojia na Ubufuni

Afisa Mratibu Utafiti Mwandamizi kutoka Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) Method Retachura akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu kuandika habari za utafiri Machi 8,2023 jijini Dar es Salaam.(Picha na Goodluck Hongo)

Share on FacebookShare on Twitter

NA MWANDISHI WETU

WAANDISHI wa habari nchini wametakiwa kujikita katika kuandika habari za Sayansi,Teknolojia na Ubunifu ili kuwasaidia wananchi kupata taarifa za kitafiti kwa lugha walioizoea.

Wananchi wengi wamekuwa wakikosa fursa mbalimbali za maendelo na kutatua changamoto zao kutoka na tafiti nyingi za Sayansi na Teknolojia kushindwa kuwafikia kutokana na kile kinachoelezwa kuwa lugha ngumu inayotumika hivyo wananchi wengi kukosa fursa ya kujua umuhimu na matokea ya tafiti hizo katika maisha yao ya kila siku.

Hata hivyo Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) chini ya Mkurugenzi wake Dkt.Amos Nungu imekuwa ikifanya juhudi mbalimbali ili kuhakikisha kuwa taarifa za kisayansi na teknolojia  zinawafikia wananchi wa hali ya chini kupitia vyombo vya habari.

Akizungumza jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki wakati wa Mafunzo ya Uandishi wa Habari za Sayansi,Teknolojia na Ubunifu kati ya waandishi wa habari na watafiti yaliyoandaliwa na COSTECH,Afisa Mratibu Utafiti Mwandamizi kutoka Tume hiyo Method Retachura amesema baadhi ya majukumu ya Tume hiyo ni pamoja na  kukusanya,kuchakata,kuhifadhi na kusambaza taarifa za Sayansi,Teknolojia na Ubunifu

Amebainisha kuwa jukumu lingeni ni pamoja na Kuishauri Serikali kuhusu masuala ya sayansi, teknolojia na ubunifu yakiwemo vipaumbele vya utafiti, mgawo wa matumizi ya fedha za utafiti kufuatana na vipaumbele vilivyokubaliwa, ushirikiano wa kikanda na kimataifa katika utafiti, mafunzo na ajira za watafiti, pamoja na Sera ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia.

Akizungumzia mbinu za uandishi wa habari za kitafiti,Retachura amesema ni muhimu kujua utafiti umegundua kitu gani kipya (findings) ambacho kinatakiwa kuwasilishwa kwa umma unaoweza  kuboresha kipato, kuondoa maradhi, kuboresha teknolojia au kuongeza mavuno ya kilimo na mengine.

Aidha amefafanua kuwa mbali na hilo lakini pia mwandishi ni muhimu kufahamu athari za utafiti (research impact) ili kusaidia jamii kujua mambo muhimu yanaendelea kwa manufaa ya Taifa zima.

Akizungumzia kuhusu wajibu Mwandishi wa Habari,Retachura ameeleza kuwa baada ya kupata taarifa za utafiti kupitia njia sahihi ni wajibu wa mwanahabari kuripoti kwa mujibu wa sera ya habari ya  taasisi yake (Editorial Policy).

Aisha Retachura amesema taarifa za msingi zifikishwe bila ya kupotoshwa au kutiwa chumvi(kuongezea maneno mengine) kwa madhumuni ya kutia hofu umma.

“Taarifa za Sayansi, Teknolojia na Ubunifu zinaungwa mkono, au kutofautishwa na taarifa nyingine, kwa kutumia lugha ya takwimu na ukweli.

“Ninaamini mfumo huu utasaidia mno kufikisha taarifa za utafiti wa kisayansi kwa umma.

 “Aidha, malalamiko ya kwamba waandishi hawafahamu taarifa zilizomo katika tafiti yatapungua kwa kiwango kikubwa”amesema Retachura

Kwa upande wake Mratibu wa Mafunzo ya Uandishi wa Habari za Sayansi,Teknolojia na Ubunifu kutoka COSTECH Deusideth Leoanaed amesema hayo ni mafunzo ya tisa kufanyika tangu mwaka 2015 ya kuwakutanisha Waandishi wa Habari,Watafiti na Wabunifu.

“Lengo ni kuwaleta pamoja na kubadilishana uzoefu ili tafiti nyingi ziweze kuandikwa kwa lugha rahisi,kupata ongezeko la uhawilishaji wa teknolojia kati ya Watafiti na Jamii  na kuwajengea uwezo waandishi wa habari ili waweze kuandika taarifa za Sayansi,Teknolojia na Ubunifu kama ilivyo katika maeneo mengine ikiwemo siasa na michezo”amesema Leonaed.

Waandishi mbalimbali wa habari kutoka katika magazeti,luninga,redio na blog wamefanikiwa kupata mafunzo juu ya kuandika Habari za Sayansi,Teknolojia na Ubunifu ili kusaidia katika kufikisha taarifa sahihi kwa wananchi kwa lengo la  kutatua changamoto zinazowakabili.

Next Post
Mungano wa Tanganyika na Zanzibar ni kipekee duniani

Mungano wa Tanganyika na Zanzibar ni kipekee duniani

Rais Dkt Samia:Sioni sababu kuminya uhuru wa habari

Rais Dkt Samia:Sioni sababu kuminya uhuru wa habari

BRELA yashukuru vyombo vya habari ongezeko usajili wa makampuni

BRELA yashukuru vyombo vya habari ongezeko usajili wa makampuni

Discussion about this post

Contact us:

BAJETI COMMUNICATION

info@bajeti.co.tz
bajetinews@gmail.com
+255718699828
P.o.BOX 18133,
DAR ES SALAAM,
TANZANIA

Category

  • Habari
  • Magazeti
  • Makala
  • Mazingira
  • Michezo
  • Picha
  • Sayansi na Teknolojia
  • Siasa

Our Visitors

  • Today's visitors:6
  • Today's page views 6
  • Total visitors 13,062
  • Total page views 14,807

Kuhusu Tovuti Hii

Hii ni tovuti ya habari iliyojikita katika kuandika  habari za kina   zikiwemo za mazingira kwa lengo la kuelimisha na kuuhabarisha umma.

Subscribe

  • About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact

© 2025 Bajeti

No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo

© 2025 Bajeti

Welcome Back!

Login to your account below

Forgotten Password?

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In