NA MWANDISHI WETU
MKURUGENZI wa Kampuni ya Nyirenda Company Limited Wilbroad Nyirenda ameiomba Serikali na wadau wengine wa Sayansi na Teknolojia kuendelea kusaidia bunifu ndogondogo kwa kuwa zinaweza kuifanya Tanzania kuwa bora kiteknolojia.
Nyirenda amesema bidhaa kama ya Mita ya Maji aliyoibuni ambayo hulipia kulingana na matumizi yako na yenye mfumo wa mtu kutofika kusoma mita hizo kujua uniti zilizotumika utaongeza mapato kwa Serikali na ajira kwa watanzania.
Nyirenda ametoa wito huo Aprili 9,2023 wakati akizungumza na tovuti hii ya Bajeti jijini Dar es Salaam juu ya umuhimu wa kuendeleza bunifu zinazobuniwa na watanzania ili kuifanya nchi kujitegemea na teknolojia yake wakiwemo wanasayansi .
Amesema bunifu zipo nyingi na vinaja wanajitahidi kuziendeleza hivyo kuwashika mkono ili kuendeleza bunifu zao ni jambo muhimu kwa maendeleo ya nchi.
“Tunawaomba wadau na serikali waendelee kusaidia wabunifu hasa vijana ili kutimiza malengo yao na kuwa mkombozi kwa jamii”amesema Nyirenda
Nyirenda ameongeza kuwa Tanzania inaweza kuzalisha ajira nyingi kupitia bunifu hizo za vijana na nchi kukua kiteknolojia na kujitegemea .
Awali Nyirenda aliishukuru Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) kwa kumpa kumsaidia kubadilisha kutoka ubunifu kwenda kwenye vitendo halisi wa kutengeneza mita za kisasa kwa kumpatia kiasi cha Sh.Milioni 250 kuanzisha kiwanda kidogo cha kuzalishia mita hizo .




Discussion about this post