• About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact
Tuesday, January 13, 2026
  • Login
Bajeti
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo
No Result
View All Result
Bajeti
No Result
View All Result
Home Habari

SHIVYAWATA washukuru mfumo wa walemavu wa miguu kuendesha gari

by bajeti
April 12, 2023
in Habari
0
SHIVYAWATA washukuru mfumo wa walemavu wa miguu kuendesha gari

Gari likiwa limefungwa vifaa kwa ajili ya watu wenye ulemavu wa miguu kuliendesha

Share on FacebookShare on Twitter

NA MWANDISHI WETU,TANGA

SHIRIKISHO la Vyama vya Watu Wenye Walemavu Tanzania (SHIVYAWATA) limeshukuru kuwepo kwa mfumo wa kusaidia watu wenye ulemavu wa miguu  kuendesha gari  kwa kuwa hali hiyo inaonesha jinsi Serikali na watanzania wengine wanavyowakumbuka wenye hali hiyo.

Hayo yameelezwa Aprili 11,2023 na Mwenyekiti wa SHIVYAWATA Ernest Kimaya wakati akizungumza na tovuti hii ya Bajeti juu ya mfumo huo ambao umebuniwa na mtanzania Joseph Taifa unaowafanya watu wenye ulemavu wa miguu kuendesha gari kama walivyo wengine.

Amesema wamefurahi kusikia watanzania wengine wanawakumbuka na kuwajali watu wenye ulemavu hadi kufikia hatua ya kubuni kitu hicho cha kuwafanya nao kuendesha vyombo vya moto vyenye vifaa vinavyoendana na mazingira yao.

“Tunaishukuru sana Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) kwa kuendeleza ubunifu huo ili watu wenye ulemavu wa miguu nao waweze kutumia magari,tunashukuru sana na sisi tutasambaza nchi nzima ili ufahamike”amesema Kimaya

Haya hivyo Kimaya  amebainisha kuwa wanajipanga ili  kutembelea karakana ya mbunifu huyo kujionea anavyotengeneza na kuona jinsi gani ya kuuendeleza ili kuwanufaisha watu wenye ulemavu nchi nzima.

Mbunifu wa mfumo wa watu wenye ulemavu wa miguu kuendesha gari Joseph Taifa akitoa ufafanuzi jinsi unavyofanya kazi kwa wananchi waliomtembelea jijini Dar es Salaam.(Picha na mpigapicha wetu)

Kwa upande wake Mtafiti na Mbunifu huyo Joseph Taifa amesema amefurahi kusikia kitu alichokibuni kinaweza kuwasaidia watu wengi wenye ulemavu wa miguu ambao walikata tamaa ya kuendesha gari kutokana na hali waliyokuwa nayo na alitumia muda mwingi kuwafikiria baada ya kuhitimu masomo yake chuoni.

“Tunawasubiri sana SHIVYAWATA ili tuwaonesha mfumo huu ambao ili mtu mwenye ulemavu aweze kuendesha gari lazima pia asome kwanza chuo ambacho tunaendelea na maandalizi ya mwisho ili kukamilisha taratibu  za kiserikali ambapo hadi sasa tumeshafunga magari matatu.

“Lazima kila dereva anayetumia mfumo huu asome chuo kwa kuwa anaweza kusababisha ajali kwa kushindwa kumudu kulisimamisha ama kuondoka kutokana na vifaa vyake vingi kutumia mikono pekee na sio miguu”amesema Taifa

Hata hivypo Taifa ameongeza kuwa mfumo huo hauruhusu gari kuharibika na kwamba unaweza kufungwa ama kuondolewa katika gari bila tatizo..

 

Next Post
Mwanafunzi kidato cha kwanza atengeneza redio

Mwanafunzi kidato cha kwanza atengeneza redio

MUUNGANO

DODOMA

Jeshi la Polisi latakiwa kujitathmini kukabiliana na mabadiliko ya kiteknolojia.

Jeshi la Polisi latakiwa kujitathmini kukabiliana na mabadiliko ya kiteknolojia.

Discussion about this post

Contact us:

BAJETI COMMUNICATION

info@bajeti.co.tz
bajetinews@gmail.com
+255718699828
P.o.BOX 18133,
DAR ES SALAAM,
TANZANIA

Category

  • Habari
  • Magazeti
  • Makala
  • Mazingira
  • Michezo
  • Picha
  • Sayansi na Teknolojia
  • Siasa

Our Visitors

  • Today's visitors:1
  • Today's page views 1
  • Total visitors 13,057
  • Total page views 14,802

Kuhusu Tovuti Hii

Hii ni tovuti ya habari iliyojikita katika kuandika  habari za kina   zikiwemo za mazingira kwa lengo la kuelimisha na kuuhabarisha umma.

Subscribe

  • About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact

© 2025 Bajeti

No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo

© 2025 Bajeti

Welcome Back!

Login to your account below

Forgotten Password?

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In