• About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact
Thursday, January 22, 2026
  • Login
Bajeti
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo
No Result
View All Result
Bajeti
No Result
View All Result
Home Mazingira

Gundi ya Nyuki hutumika kutengeneza dawa na vipodozi

by bajeti
June 30, 2023
in Mazingira
0
Gundi ya  Nyuki hutumika kutengeneza dawa na vipodozi

Nyuki akitafuta malighali katika maua ili kuzalisha asali.

Share on FacebookShare on Twitter

NA GOODLUCK HONGO

AFISA Ufugaji Nyuki kutoka Idara ya Misitu na Nyuki Wizara ya Maliasili na Utalii Aneth Moshi  amesema Nyuki ni wadudu rafiki kwa mazingira hivyo wanatakiwa kutunzwa na kulindwa kutokana na umuhimu wake ikiwemo kuzalisha gundi.

Amesema baadhi ya tafiti zimeonesha kuwa Nyuki wanasaidia sana katika suala zima la uzalishaji wa chakula hivyo kukosekana kwao kutaongeza uhaba wa chakula.

Moshi ametoa kauli hiyo jijini Dar es Salaama wakati akizungumza na Bajeti Communication katika Maonesho ya 47 ya Biashara ya Kimataifa yanayoendelea katika viwanja vya Sabasaba.

Amesema mbali na mdudu huyo kuzalisha Asali,Nta  na maziwa lakini pia huzalisha gundi ambayo hutumiwa katika kutengeneza dawa na vipodozi.

Amesema huwa hawapendi usumbufu kutoka kwa wadudu wengine ama madui zake hivyo hutumia gundi wanazozitoa katika miti mbalimbali na kuichukua na kisha kwenda kuziba eneo lao wanaloishi  ili lisiingiliwe na wadudu wengine kama Mchwa,Sisimizi na Siafu.

Amesema Nyuki huchukua jukumu la kuweka gundi kwa ajili ya kuzuia maadaui muda wote ambapo hiyo ni moja ya njia ya kulinda kundi lao lisishambuliwe na maadui na ndipo huziba kila eneo na kuacha sehemu yao ya kuingilia pekee.

“Nyuki  wanaweka gundi kwa ajili ya kuzuia maadui muda wote na hii ni moja wapo ya njia za kulinda kundi lao lisishambuliwe na maadui .

“Hawataki maadui kama siafu hivyo hutumia gundi kama ulinzi wake na hapo ndipo inapovunwa na baadaye kutengeneza dawa,vipodozi na hata chakula kutokana na mchanganyiko wa miti wanayotumia kutengeneza gundi hiyo”amesema Moshi

Hata hivyo Moshi amebainisha kuwa licha ya kuwepo kwa zao hilo la nyuki lakini bado wavunaji wake ni wachache.

Nyuki wakiwa katika mizinga ya kisasa

Akizungumzia kuhusu mazao ya nyuki yanayotumika sana,Moshi ameeleza  kuwa kwa sasa mazao ya Asali na Nta ndio yanayovunwa sana na mikoa inayoongoza kwa uvunaji huo ni Kanda ya Magharibi inayojumuisha Kigoma,Katavi na Tabora.

Kwa upande wa Kanda ya Ziwa ni Shinyanga ambayo huzalisha kidogo na Kanda ya Kati ni Dodoma na Singida ambapo Kanda ya Kaskazini ni pamoja na mikoa ya Arusha na Manyara huku Kanda ya Kusini ikiwakilishwa na Mtwara.

“Asali na Nta ndiyo yanayovunwa  kwa wingi licha ya kuwa nyuki anazalisha maziwa na sumu yake ambavyo vyote ni muhimu lakini kutokana na changamoto mbalimbali Asali na Nta ndiyo yanaongoza kwa kuvunwa”amesema Moshi

Next Post
Poland yakumbwa na ugonjwa unaoua Paka

Poland yakumbwa na ugonjwa unaoua Paka

Serikali kuimarisha teknolojia ya anga za juu

Serikali kuimarisha teknolojia ya anga za juu

Mwanamfalme Harry wa Uingereza apokonywa  nyumba baada ya  kuikosoa familia yake

Mwanamfalme Harry wa Uingereza apokonywa nyumba baada ya kuikosoa familia yake

Discussion about this post

Contact us:

BAJETI COMMUNICATION

info@bajeti.co.tz
bajetinews@gmail.com
+255718699828
P.o.BOX 18133,
DAR ES SALAAM,
TANZANIA

Category

  • Habari
  • Magazeti
  • Makala
  • Mazingira
  • Michezo
  • Picha
  • Sayansi na Teknolojia
  • Siasa

Our Visitors

  • Today's visitors:18
  • Today's page views 18
  • Total visitors 13,277
  • Total page views 15,025

Kuhusu Tovuti Hii

Hii ni tovuti ya habari iliyojikita katika kuandika  habari za kina   zikiwemo za mazingira kwa lengo la kuelimisha na kuuhabarisha umma.

Subscribe

  • About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact

© 2025 Bajeti

No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo

© 2025 Bajeti

Welcome Back!

Login to your account below

Forgotten Password?

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In