WARSAW,POLAND
RAIS wa zamani wa Urusi Dmitry Medvedev amesema vita vya nyuklia vinaweza kuanza ikiwa Marekani itaikubalia Poland ya kuweka silaha za nyuklia katika ardhi ya nchi hiyo.
Medvedev ambaye ni Naibu Mwenyekiti wa Baraza la Usalama wa Taifa la Urusi ametoa kauli hiyo siku chache baada ya Waziri Mkuu wa Poland Mateusz Morawiecki kuuomba Umoja wa Kijihami wa Nchi za Magharibi(NATO) kuijumuisha nchi yake katika mpango wa kugawana Nyuklia wa Umoja huo.
Medvedev alitoa majibu hayo katika akaunti yake ya mtandao Telegraph mnamo Julai Mosi,2023 baada ya kuulizwa maoni yake kutoka kwa waaandishi wa habari juu ya Poland kuomba mgawao huo.
Rais huyo wa zamani wa Urusi aliuelezea uongozi wa Poland na kuonya kuwa kuwepo kwa silaha za nyuklia nchini humo kungemaanisha kwamba zitatumika.
Akizungumza na waandishi wa habari mjini Brussels Juni 30,2023 Waziri Mkuu wa Poland Mateusz Morawiecki alisema kutokana na ukweli kwamba Urusi inakusudia kupeleka silaha za kinyuklia nchini Belarus,wanatoa wanaiomba NATO kuwaruhusu katika ugawanaji wa Nyuklia.
Mpango wa Kugawana Nyuklia wa NATO umeshuhudia mabomu ya nyuklia ya Marekani B-61 yakipelekwa katika maeneo mbalimbali kote barani Ulaya.
Kutokana na usambazaji huo,Urusi nayo iliamua kupelekwa silaha za nyuklia huko Belarus mnamo mwezi Machi na makubaliano yalikamilishwa Mei mwaka 2023.
Hata hivyo katikati ya mwezi Juni, Rais Vladmir Putin wa Urusi alimweleza mwenzake Rais wa Belarus Alexander Lukashenko kwamba maandalizi yatakamilika mapema Julai, huku kukiwa na vichwa kadhaa vya nyuklia vikiwa vimeanza kupelekwa.
Awali Rais Lukasjenko alieleza sababu za kuomba silaha hizo kuwa kulikuwa na tishio lililoelekezwa kwa nchi yake, ambayo ilibidi kukabiliana nalo na kusisitiza kuwa hatasita kutumia silaha hizi za Urusi katika uchokozi wowote dhidi ya Belarus




Discussion about this post