• About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact
Thursday, January 22, 2026
  • Login
Bajeti
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo
No Result
View All Result
Bajeti
No Result
View All Result
Home Siasa

Demokrasia yaanza kuwashinda wamarekani

by bajeti
July 16, 2023
in Siasa
0
Demokrasia yaanza kuwashinda wamarekani

Wafuasi wanaodaiwa kuwa ni wa Rais Mstaafu wa Marekani Donald Trump wakiwa katika Bunge la Marekani Januari 7,2021.Picha kwa hisani ya DW

Share on FacebookShare on Twitter

WOSHINGTON DC,MAREKANI

UVUMILIVU wa kufurahia demokrasia umeanza kuwashinda wamarekani baada ya utafiti kuonesha kuwa wanawasiwasi kuhusu namna mfumo huo unavyoendeshwa nchini kwao

Hata hivyo utafiti huo unakuja wakati ambapo Marekani ikiwa ndio taifa kubwa zaidi duniani linalokemea na kuweka vikwazo dhidi ya nchi zingine ambazo hazifuati kile inachodai kuwa demokrasia na uvunjaji wa haki za binadamu.

Marekani ambayo bado inateswa na tukio kubwa lililoushangaza ulimwengu la Januari 7,2021 baada ya wafuasi wanaodaiwa kuwa ni wa Rais wa zamani wa nchi hiyo Donald Trump kuandamana na kisha kuvamia bunge la nchi hiyo ili kubadili matokeo ya uchaguzi wa rais wa Novemba 3,2020 yaliompa ushindi Rais Joe Biden.

Viongozi wa dunia walieleza kushtushwa na tukio hilo ambapo aliyekuwa Waziri Mkuu wa Uingereza wakati wa tukio hilo Borris Johnson aliandika katika ujumbe wake wa twitter na kuelezea kuwa  matukio katika bunge la Congress ni fedheha kwani Marekani ilisimamia demokrasia duniani kote na kwamba ilikuwa muhimu kuwa na mabadiliko ya amani ya utawala.

Marekani ilishindwa kuwavumilia wafuasi hao waliovamia Bunge na kutumia nguvu kuwaondoa huku wabunge wakiwa wamejificha kuhofia usalama wao hali iliyoonesha kuwa hata taifa hilo haliwezi kuvumilia demokrasia iliyovuka mipaka katika kulinda amani na umoja wa kitaifa.

Kwa mujibu taarifa ya iliyotangazwa na Sauti ya Amerika (VOA) ya Julai 15,2023  imeeleza kuwa ukusanyaji maoni uliofaywa na Shirika la habari la Asociated Press na Kituo cha Utafiti wa Masuala ya Umma NORC,umeeleza kuwa  takribani asilimia 49 ya wamarekani wanasema demokrasia haifanyi kazi vizuri nchini Marekani.

Taarifa hiyo imeeleza kuwa ni asilimia 10 pekee ndio wanaosema demokrasia inafanya kazi vizuri sana, wakati asilimia 40 wakisema kwamba inafanya kazi kiasi ambapo vyama vikuu viwili vya siasa nchini Marekani vya Republican na Democratic vyote vilipata alama za chini kwa namna vinavyoendesha misingi ya demokrasia.

Asilimia 47 ya watu waliohojiwa wamesema kwamba wademokrat wanafanya kazi isiyoridhisha katika kudumisha demokrasia, wakati asilimia 56 wakisema kwamba warepablikan wanahitaji kufanya vizuri zaidi.

Kwa mujibu wa utafiti huo,ukusanyaji  wa maoni unaonesha kuna migawanyiko mikubwa ya kisiasa, wakati taifa hilo likijikwamua kutokana na janga la virusi vya UVIKO-19, mfumuko wa bei na hofu ya kudorora kwa uchumi ambapo takwimu hizo zilikusanywa kati ya Juni 22 na 26 mwaka huu

Aprili 7, 2023 dunia ilishangazwa pia na taifa hilo kumfikisha mahakamani Rais wa zamani wa nchi hiyo Donald Trump akikabiliwa na mashtaka 34 ya jinai  huko New York  ikiwemo kughushi rekodi za biashara kwa mara ya kwanza katika historia ya nchi hiyo.

Juni 21, 2023 Mtoto wa rais wa Marekani Joe Biden, Hunter Biden, siku ya jumanne  alifikia makubaliano na Idara ya Sheria ya kukiri mashtaka matatu ya kukwepa kulipa kodi na kumiliki silaha kinyume cha sheria, ambayo yanaelezwa kama yanayopunguza uwezekano wake kufungwa gerezani.

Kulingana na kesi iliyowasilishwa mahakamani siku ya Jumanne, Hunter Biden, mwenye umri wa miaka 53, ambaye kwa muda mrefu ametatizwa na uraibu wa mihadarati na uchunguzi wa shughuli zake za biashara nje ya nchi, atakubali mashtaka mawili ya makosa ya kukosa kulipa kwa wakati, kati ya mwaka 2017 na 2018, na kukubali kuwekwa katika hali ya uangalizi, maarufu probation.

Kwa kuongezea, nyaraka za mahakama zilionyesha kwamba Idara ya Sheria ilikubali kutomfungulia mashataka kuhusiana na ununuzi wake wa bunduki mnamo mwaka wa 2018 alipokuwa akitumia dawa za kulevya, ingawa alidai kwenye hati ya ununuzi kuwa hakuwa anatumia dawa hizo.

Makubaliano hayo yanamtaka Biden kusalia bila kutumia dawa kwa miaka miwili na akubali kutomiliki tena bunduki, lakini ni lazima yaidhinishwe na jaji.

Kutofungwa kwa mtoto wa Rais huyo wa Marekani kumetia doa demokrasia ya nchi hiyo kwa kuonesha upendeleo wa kisheria kuwa watoto wa viongozi hulindwa kama zilivyo baadhi ya nchi zingine duniani ambapo matukio hayo hayako kwa Viongozi wa Afrika au Asia bali kila nchi huchukua hatua kulingana na vipaumbele vya usalama wa taifa lao.

Taarifa hii imeandaliwa kwa msaada wa mashirika mbalimbali ya habari ya kimataifa ikiwemo DW,AP na VOA

Next Post
Bilioni 5.68 zatumika kuwalisha wahamiaji haramu

Bilioni 5.68 zatumika kuwalisha wahamiaji haramu

CCM yampongeza Rais Samia kuunda Wizara ya Mipango

CCM yampongeza Rais Samia kuunda Wizara ya Mipango

JET  yawataka waandishi wa habari kujikita katika uhifadhi wa maliasili,mapito ya wanyamapori(Shoroba)

Ghala la Pembe za Ndovu latekelezwa

Discussion about this post

Contact us:

BAJETI COMMUNICATION

info@bajeti.co.tz
bajetinews@gmail.com
+255718699828
P.o.BOX 18133,
DAR ES SALAAM,
TANZANIA

Category

  • Habari
  • Magazeti
  • Makala
  • Mazingira
  • Michezo
  • Picha
  • Sayansi na Teknolojia
  • Siasa

Our Visitors

  • Today's visitors:18
  • Today's page views 18
  • Total visitors 13,277
  • Total page views 15,025

Kuhusu Tovuti Hii

Hii ni tovuti ya habari iliyojikita katika kuandika  habari za kina   zikiwemo za mazingira kwa lengo la kuelimisha na kuuhabarisha umma.

Subscribe

  • About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact

© 2025 Bajeti

No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo

© 2025 Bajeti

Welcome Back!

Login to your account below

Forgotten Password?

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In