• About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact
Thursday, January 22, 2026
  • Login
Bajeti
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo
No Result
View All Result
Bajeti
No Result
View All Result
Home Siasa

CCM yampongeza Rais Samia kuunda Wizara ya Mipango

by bajeti
July 16, 2023
in Siasa
0
CCM yampongeza Rais Samia kuunda Wizara ya Mipango

Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzu Taifa (CCM) Abdulrahman Kinana, akizungumza na wanachama wa chama hicho pamoja na wananachi katika mkutano wa hadhara uliondaliwa na Mbunge wa Jimbo la Kibiti Ally Mpembenwe kueleza kazi kubwa ya Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM uliyofanyika Julai 15,2023 wilayani Kibiti Mkoa wa Pwani.(Picha na CCM)

Share on FacebookShare on Twitter

NA MWANDISHI WETU,PWANI

MAKAMU Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara Abdulrahman Kinana amepongeza uamuzi wa Rais Dk.  Samia Suluhu Hassan Hassan wa kuunda wizara inayohusika na mipango.

Pia, amepongeza hatua ya kuifanya Tume ya Mipango kuwa chini ya ofisi ya Rais ambapo amesema itaongeza kasi na uhakika wa mipango ya maendeleo nchini.

Kinana ameyasema hayo Juni 15,2023 wilayani Kibiti  Mkoa wa Pwani kupitia mkutano wa hadhara uliondaliwa na Mbunge wa Jimbo la Kibiti Ally Mpembenwe kueleza kazi kubwa ya utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM iliyofanyika katika jimbo hilo.

Amesema hivi karibuni Rais ameunda wizara mpya inayoshughulika na mipango, ambapo kwa lugha nyingine ni Tume ya Mipango ambayo ipo ofisini kwake ikiwa na lengo lake moja ni moja tu.

“Rais akaona wizara ile inapoitwa Wizara ya Fedha na Mipango inafanya kazi zaidi ya kukusanya na kutumia kuliko kupanga akaona hapana, nadhani ni vizuri sasa tutengengeze wizara ya mipango,” amefafanua Kinana

Aidha ameongeza kuwa Tanzania tangu Baba wa Taifa Hayati Mwalimu Julius Nyerere akiwa hai, wizara hiyo ilikuwepo, ndiyo iliyokuwa ikipanga maendeleo ya nchi hata hivyo iliondolewa.

“Rais katika uzoefu wake akaona hapana, hakuna maendeleo bila ya mpango, hakuna mapato bila mpango, hakuna matumizi bila mpango, kwa hiyo wizara hii na tume hii itakapoanza kazi ninawahakikishia watanzania maendeleo yatakuwa ya uharaka zaidi kuliko ya sasa na kuliko mlivyowahi kuyaona. 

“Kwa hiyo tunampongeza sana Rais (Dk. Samia), tunakipongeza Chama Cha Mapinduzi kwa sera nzuri kwa sababu na Rais wetu ni Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi na Serikali yake inasimamia utekelezaji wa Sera na Ilani ya Uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi,” amesema Kinana

 

Next Post
JET  yawataka waandishi wa habari kujikita katika uhifadhi wa maliasili,mapito ya wanyamapori(Shoroba)

Ghala la Pembe za Ndovu latekelezwa

Kaburi la ajabu lililoshindikana kuhamishwa

Kaburi la ajabu lililoshindikana kuhamishwa

Wafungwa 3252 ‘waigeuza jela nyumbani’

Wafungwa 3252 ‘waigeuza jela nyumbani’

Discussion about this post

Contact us:

BAJETI COMMUNICATION

info@bajeti.co.tz
bajetinews@gmail.com
+255718699828
P.o.BOX 18133,
DAR ES SALAAM,
TANZANIA

Category

  • Habari
  • Magazeti
  • Makala
  • Mazingira
  • Michezo
  • Picha
  • Sayansi na Teknolojia
  • Siasa

Our Visitors

  • Today's visitors:18
  • Today's page views 18
  • Total visitors 13,277
  • Total page views 15,025

Kuhusu Tovuti Hii

Hii ni tovuti ya habari iliyojikita katika kuandika  habari za kina   zikiwemo za mazingira kwa lengo la kuelimisha na kuuhabarisha umma.

Subscribe

  • About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact

© 2025 Bajeti

No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo

© 2025 Bajeti

Welcome Back!

Login to your account below

Forgotten Password?

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In