• About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact
Tuesday, January 13, 2026
  • Login
Bajeti
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo
No Result
View All Result
Bajeti
No Result
View All Result
Home Mazingira

Dawa za kulevya zadaiwa kuwafanya Papa kuwa na “Wazimu” baharini

by bajeti
July 22, 2023
in Mazingira
0
Dawa za kulevya zadaiwa kuwafanya Papa kuwa na “Wazimu” baharini

Mmoja wa wanyama wa baharini Papa

Share on FacebookShare on Twitter

WASHINGTON DC,MAREKANI

WATAFITI nchini Marekani wamesema kuna uwezekano kuwa wanyama wa baharini wakiwemo Papa wanatumia dawa za kulevya zinazodondoshwa na walanguzi wa mihadarati na kuwafanya kuwa na “Wazimu”

Hayo yanakuja kutokana na Walinzi wa Pwani wa Marekani kueleza kuwa wamekamata kiasi cha kilo 6,400 za dawa za kulevya aina Cocaine katika Bahari ya Bahari ya Atlantiki katika kipindi cha mwezi mmoja uliopita.

Kwa mujibu wa tovuti ya Serikali ya Urusi ya RT imewanukuu Watafiti wanaofanya kazi kwenye kipindi cha luninga cha’Cocaine Sharks’ wakizungumza siku ya Alhamisi Julai 20,2023 kwamba wamegundua baadhi ya Papa wamekuwa na tabia ya ajabu katika eneo hilo na wakaendesha majaribio kadhaa kutoka kwenye Pwani ya Florida, ambapo wavuvi wameripotiwa kukutana na samaki walioathiriwa na dawa za kulevya.

Mwanabiolojia wa baharini Tom Hird, na mwanasayansi wa Mazingira wa Chuo Kikuu cha Florida Tracy Fanara wameeleza kuwa wakati wa kupiga mbizi waliona  spishi ambayo huwaepuka wanadamu mara kwa mara – ikipita moja kwa moja kwenye timu inapoogelea

Wanasayansi hao pia walifanya jaribio ambapo waliweka ndani ya maji kitu mfano wa kifurushi cha ukubwa sawa na mwonekano wa kama vile vinavyodoshwa baharini na walanguzi wa dawa za kulevya.

Wamesema kwa mshangao Papa hawakuvamia vifurushi vingine na badala yake walielekea moja kwa moja kwenye ‘vifurushi venye mfano wa cocaine’ na kisha  kujaribu kuchukua kwa kuuma ambapo  mmoja kati ya viumbe hao alichukua na kuogelea nayo.

Wanasayansi hao pia walifanya jaribio ambapo walitengeneza mpira wa chambo kutoka kwa unga wa samaki wanaodaiwa kuwa walikuwa cocaine na Papa hao walipokula unga huo waliwaona wakienda porini kabisa.

“Tuliwapa kile nadhani ni kitu bora zaidi na iliwasha akili zao moto na  ilikuwa ni wazimu.”amesema Hird

Timu hiyo pia ilidondosha marobota ya kokeini kutoka kwa ndege ili kuiga hali halisi ya kushuka kwa dawa na ikagundua kuwa aina nyingi za papa zilihamia kwenye vifurushi mara moja.

Wanabiolojia hao wamekiri, hata hivyo, kwamba uchunguzi wao bado haujathibitisha kuwa kweli Papa wanatumia Cocaine, wakisema kwamba hawajui ni  nini cocaine inaweza kufanya kwa Papa.

Hata hivyo Hird ameonyesha matumaini kwamba kuandikwa kwa mfululizo wa makala kunaweza kusababisha utafiti zaidi juu ya suala hilo na  jinsi dawa zingine zinavyoathiri viumbe vya baharini

 

Next Post
Magonjwa yanayowaathiri  wanyamapori yatajwa

Magonjwa yanayowaathiri wanyamapori yatajwa

Kinana:Waliojaribu kuigawa nchi kwa misingi ya ukabila na udini wameshindwa

Kinana:Waliojaribu kuigawa nchi kwa misingi ya ukabila na udini wameshindwa

Matukio 1718 ya milipuko na moto hayajachunguzwa

Matukio 1718 ya milipuko na moto hayajachunguzwa

Discussion about this post

Contact us:

BAJETI COMMUNICATION

info@bajeti.co.tz
bajetinews@gmail.com
+255718699828
P.o.BOX 18133,
DAR ES SALAAM,
TANZANIA

Category

  • Habari
  • Magazeti
  • Makala
  • Mazingira
  • Michezo
  • Picha
  • Sayansi na Teknolojia
  • Siasa

Our Visitors

  • Today's visitors:9
  • Today's page views 9
  • Total visitors 13,065
  • Total page views 14,810

Kuhusu Tovuti Hii

Hii ni tovuti ya habari iliyojikita katika kuandika  habari za kina   zikiwemo za mazingira kwa lengo la kuelimisha na kuuhabarisha umma.

Subscribe

  • About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact

© 2025 Bajeti

No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo

© 2025 Bajeti

Welcome Back!

Login to your account below

Forgotten Password?

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In