• About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact
Tuesday, January 13, 2026
  • Login
Bajeti
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo
No Result
View All Result
Bajeti
No Result
View All Result
Home Habari

Putin aionya Poland

by bajeti
July 22, 2023
in Habari
0
Putin aionya Poland

Rais wa Urusi Vladmir Putin

Share on FacebookShare on Twitter

MOSCOW,URUSI

RAIS wa Urusi Vladmir Putin ameionya Poland juu ya uamuzi wake kupeleka wanajeshi karibu na mpaka wa Belalus na kubainisha kuwa Moscow itajibu kwa njia zote vitisho juu ya mshirika wake mkuu Belarus

Kwa mujibu wa tovuti ya  Serikali ya nchi hiyo ya RT ilimnukuu Kiongozi huyo wa Urusi Julai 21,2023 akisema kuwa  viongozi wa Poland wanapanga kuunda muungano unaoungwa mkono na Jumuia ya Kujihami ya Nchi za Magharibi (NATO) ili kuingilia kati mzozo wa Ukraine na kutwaa baadhi ya maeneo ya magharibi mwa Ukraine pamoja na, pengine, Belarus,

Akizungumza katika Mkutano na Wajumbe wa Kudumu wa Baraza la Usalama la Urusi Julai 21,2023 jijini Moscow, Putin amesema serikali ya Kiev iko tayari kufanya lolote lile ili kusalia madarakani, ikiwa ni pamoja na kuuza watu wake na kukabidhi maeneo ya Ukraine kwa “wamiliki wa kigeni.”

Amesema wa kwanza katika mstari huo ni Wapolandi, ambao wanatarajia kuunda aina fulani ya muungano chini ya ‘mwavuli wa NATO’ na kuingilia moja kwa moja mgogoro wa Ukraine, ili ‘kung’oa’ kipande kikubwa zaidi cha ardhi na kurejesha kwao kama wanavyoaminikuwa  maeneo yao ya kihistoria magharibi mwa Ukraine ya leo.

Akizungumzia ripoti ya Huduma ya Kijasusi ya Kigeni ya Urusi (SVR), Putin alipendekeza kwamba dhumuni la kweli la muungano kama huo lingekuwa tu kuchukua maeneo ya Ukrain.

“Matarajio ni dhahiri – ikiwa vitengo vya Poland vitaingia, kwa mfano, Lvov au maeneo mengine ya Ukraine, basi watabaki huko na watakaa humo milele.” na kuongeza kuwa inajulikana kwamba Warsaw inaota pia kudai sehemu za eneo la Belarusi.

Kiongozi huyo wa Urusi ameonya hata hivyo kwamba, wakati Ukraine ina haki ya kuuza sehemu kubwa ya eneo lake kama inavyotaka, linapokuja suala la Belarusi, uchokozi wowote dhidi ya sehemu ya Jimbo la Muungano utamaanisha uchokozi dhidi ya Urusi.

“Tutajibu hili kwa njia zote tulizo nazo,” amesema Rais Putin

Kwa upande wake Mkuu wa Huduma ya Kijasusi ya Kigeni ya Urusi (SVR), Sergei Naryshkin,amesema kuwa Warsaw ilikuwa ikifikiria kuteka maeneo ya magharibi ya Ukraine kwa kupeleka wanajeshi wake katika eneo hilo kama sehemu ya mpango wa usalama wa Poland-Lithuania-Ukreni.

Naryshkin amesema maafisa wa Poland wanafikia hatua kwa hatua kutambua kwamba “suala la kushindwa kwa Ukraine ni suala la muda tu,” bila kujali kiasi cha msaada wa kijeshi wa Magharibi uliotumwa kwa Kiev.

Next Post
Dawa za kulevya zadaiwa kuwafanya Papa kuwa na “Wazimu” baharini

Dawa za kulevya zadaiwa kuwafanya Papa kuwa na “Wazimu” baharini

Magonjwa yanayowaathiri  wanyamapori yatajwa

Magonjwa yanayowaathiri wanyamapori yatajwa

Kinana:Waliojaribu kuigawa nchi kwa misingi ya ukabila na udini wameshindwa

Kinana:Waliojaribu kuigawa nchi kwa misingi ya ukabila na udini wameshindwa

Discussion about this post

Contact us:

BAJETI COMMUNICATION

info@bajeti.co.tz
bajetinews@gmail.com
+255718699828
P.o.BOX 18133,
DAR ES SALAAM,
TANZANIA

Category

  • Habari
  • Magazeti
  • Makala
  • Mazingira
  • Michezo
  • Picha
  • Sayansi na Teknolojia
  • Siasa

Our Visitors

  • Today's visitors:1
  • Today's page views 1
  • Total visitors 13,057
  • Total page views 14,802

Kuhusu Tovuti Hii

Hii ni tovuti ya habari iliyojikita katika kuandika  habari za kina   zikiwemo za mazingira kwa lengo la kuelimisha na kuuhabarisha umma.

Subscribe

  • About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact

© 2025 Bajeti

No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo

© 2025 Bajeti

Welcome Back!

Login to your account below

Forgotten Password?

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In