NA MWANDISHI WETU,MARA
MAKAMU Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara Kanali Mstaafu Abdulrahman Kinana ametembelea Kaburi la Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere na kmwelezea kuwa ni mwanamapinduzi wa kweli na shujaa wa Afrika.
Amesema wakati Tanzania ikiadhimisha siku ya mashujaa, Mwalimu Nyerere anabaki kuwa shujaa namba moja wa Tanzania huku pia akimtembelea Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama Mstaafu Jenerali David Musuguri (103) na kumwelelezea kuwa ni alama ya uzalendo wa Taifa, ukombozi na anastahili kuombewa afya njema.
Kanali Mstaafu Kinana ameyasema hayo Julai 25, 2023 baada ya kuzulu Kaburi la Mwalimu Nyerere na kumtembelea Mzee Musuguli nyumbani kwake Butiama mkoani Mara akiwa katika ziara kukagua uhai wa Chama, utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM na kuzungumza na wanachama.
Akiwa katika Kaburi la Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere na baada ya kuweka shada la maua, Kinana amemwelezea kuwa ni shujaa wa Tanzania na Afrika na kutoa mwito kwa nchi zinazotamani kuzikalia nchi nyingine kiuchumi kuiga mema ya Baba wa Taifa ambaye aliongoza mapambano ya kumaliza udhalimu wa nduli Idd Amin nchini Uganda.

Aidha, akiwa nyumbani kwa Jenerali Musuguri, Kinana alimwelezea kuwa mzalendo wa kweli aliyeongoza mapambano dhidi ya Idd Amin.
“Jenerali Musuguli ameliongoza Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania kwa zaidi ya miaka 50, ameliongoza Jeshi katika nafasi mbalimbali, wakati leo tunaadhimisha miaka 44 ya vita ya Uganda Jenerali Musuguri ndiye aliyeyaongoza majeshi ya Tanzania kumng’oa Nduli Idd Amin.
“Jenerali Musuguri ana nishani zote za juu za Jeshi, nishani zote kubwa za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ni alama ya shujaa, ni alama ya ukombozi, ni alama ya uzalendo wa taifa letu,” amesema Kinana
Kanali Mstaafu Kinana aliyekuwa ameambatana na viongozi wa Chama na Serikali Mkoa wa Mara kumjulia hali Jenerali Musugul na kuongeza kuwa amefurahi sana kuwa naye ambapo ametimiza miaka 103 ikiwemo kumtakia afya njema




Discussion about this post