NA GOODLUCK HONGO
BALOZI Mstaafu wa Tanzania nchini Sweden Dkt.Willibrod Slaa amesema kuwa hataacha kupiga kelele kutetea maslahi ya Taifa na kwamba katika suala la Bandari hakuna siasa.
Amesema tafsiri halisi ya siasa ni maisha,hivyo kama ni maisha basi kila mtu anafanya siasa kwa kuwa hata anayepanga bajeti ya familia yake kuhusu chakula naye anafanya siasa.
Balozi Mstaafu Slaa ametoa kauli hiyo hivi karibuni nyumbani kwake jijini Dar es Salaam wakati wa mahojiano maalum na mwandishi wa habari wa Bajeti Communication.
Amesema “Sisi hatupingi uwekezaji wowote ule na Tanzania tumewekeza miaka yote tangu uhuru kwani hata Arusha kuna mashamba makubwa ya maua na hela za Umoja wa Ulaya (EU) ndio zinafadhili mashamba hayo na huo ni uwekezaji na hakuna mtu anayepiga kelee”
“Tarehe Mosi Septemba nilitoa ahadi kuwa nimejitoa kwenye vyama vya siasa yaani siasa za vyama nimeacha (Active Party Politics).
“Nikaahidi kwa maslahi ya Taifa langu sitaacha kupiga kelele ndio watu mnashangaa sasa mbona Dokta sasa unafanya siasa,hapana ni maslahi ya Taifa,katika suala la Bandari si suala la siasa, hapa hakuna siasa,hapa ni urithi wa watoto wetu na wajukuu watatulaani tuliachia,ni urithi wao.”amesema Dkt Slaa
Dkt Slaa ambaye pia licha ya kuwa Balozi wa Tanzania nchini Sweden lakini pia aliwakilisha Nchi za Nordic na Baltic zikiwemo Finland na Denmark ameongeza kuwa kuna hela za Umoja wa Ulaya(EU) zinapanda maua kule Arusha na wako watanzania wamepewa hela na EU kwa ajili hiyo kwani yeye alikuwa kwenye Bunge la pamoja na EU na analifahamu hilo .
Amesema amekuwa mwakilishi wa Tanzania katika Bunge linaloitwa (Afrika,Carribean and Pacific Union (ACPU)(Bunge linalotokana na Mkataba wa Lome wa mwaka 1975) ambapo mwaka 1995 alipoingia bungeni alipata bahati ya kuingia kwenye Bunge hilo ambalo limeundwa kwa mujibu wa hicho kifungu cha Sheria ya Mkataba huo wa Lome ambao ni mji Mkuu wa Togo nchi iliyopo Afrika Magharibi.
Dkt.Slaa ameongeza kuwa kupitia mkatana huo EU ilikubaliana na nchi za kiafrika kwamba watakuwa na mahusiano kwa kuwa na Bunge la pamoja na nchi za Afrika,Carribean,Pacific na Bunge la Ulaya ambapo Bunge hilo la pamoja ndio linaloleta hela hapa Tanzania.
“Hela ya bajeti support ilikuwepo tangu mwaka 1975,sasa hatuhitaji popularity ya namna hiyo na tusitafute umaarufu mahali ambako hapako kwa kuonesha kuwa wewe ndiye umefanikisha kuletwa kwa fedha hizo.
“Mimi nimekuwa kwa miaka mitano kwenye Bunge linaloidhinisha hela zinazokuja Tanzania kutokea EU na mimi ni mpinzani ningetaka ningeweza kuzizuia lakini hata siku moja sikufungua mdomo wangu kuzuia kwa sababu hela zile zinakuja nchini kwangu na hii ipo angalieni recods kuanzia 1997”amesema Dkt.Slaa
Akizungumzia kuanzishwa kwa Bunge la pamoja la nchi za Kusini mwa Afrika SADC,Dkt.Slaa amebainisha kuwa baada ya kuingia bungeni mwaka 1995 na 1997 alichaguliwa na Bunge la Tanzania kuwa miongoni mwa wabunge wa kwanza wa Tanzania akiwemo Philip Marmo walioenda kuanzisha Bunge la SADC(SADC Parlimentary Forum ) na wakati huo kulikuwa na nchi 12 pekee.
Amesema yeye na Marmo ndio waanzilishi wa kwanza wa Bunge hilo na ndio walioshiriki kuandaa Katiba ya kwanza ya SADC kwa kushirikiana na Spika wa Bunge la Afrika ya Kusini ambaye wakati wa ukombozi aliishi Tanzania na alikuwa mhariri wa gazeti la kwanza la Kiingereza Tanzania baada ya Uhuru na kubainisha kuwa kitaaluma alikuwa mwanasheria.
“Kutokana na nafasi hiyo amekaa katika Bunge hilo hadi 2010 na kwa bahati mbaya nilikuwa Mwenyekiti wa kinachoitwa Kamati ya Enterparliamentry Cooperation Committee na hilo lilinipeleka kuzunguka nchi zote 12 za SADC hivyo ninachofanya sio siasa bali ni kwa ajili ya maslahi ya Taifa na hataacha kupiga kelele”amesema Dkt.Slaa




Discussion about this post