NA MIRIAM SARAKIKYA,ARUSHA
VIKUNDI mbalimbali vinavyonzishwa na makabila yanayoshia nje ya maeneo walikozaliwa wametakiwa kusaidiana katika kudhamini elimu na sio kushiriki katika misiba na sherehe pekee.
Ikiwa vikundi vinavyounda umoja wataamua kusaidiana kwa kuwakopesha au kuwasaidia wale wasio na uwezo wa kusomesha watoto wao na wanaohitaji kuongeza elimu watawainua zaidi katika maendeleo yao kupitia elimu watakayoipata.
Hayo yameelezwa Agosti 2,2023 jijini Arusha na Mtaalamu wa Sheria Dkt.Gilbert Bankobeza wakati akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya hafla ya Umoja wa Kabila la Wanyambo unaojulikana kama Kanono Group wanaotoka Wilaya ya Karagwe na Kyera mkoani Kagera waishio mkoani Arusha.
Amesema ni muhimu kwa vikundi kama hivyo vinavyowakutanisha watu wengi wa eneo moja kusaidiana katika masuala ya elimu na sio kusaidiana katika sherehe na misiba pekee.
“Mkisaidiana kwa kuwakopesha au kuwasaidia wale wasio na uwezo wa kusomesha watoto wao au wale wanaohitaji kuongeza elimu mtawainua zaidi katika maendeleo yao kupitia elimu.
“Watu walio wengi wamekutana katika shule ,vyuo na kuwa marafiki hivyo wakisaidiana katika masuala ya elimu watajenga msingi imara wa elimu kwao na kwa vizazi vijavyo”amesema Dkt.Bankobeza

Kwa upande wake mmoja wa mwananchama wa Kanono Group Erick fidelis amesema kipaumbele kikubwa kitaelekezwa kuwaelimisha vijana umuhimu wa kuenzi na kuendeleza mbinu zilizotumiwa na waasisi wa taifa hili kukabiliana na maovu ikiwemo ya kuimarisha baadhi ya mila na tamaduni zisizo na madhara
Naye Helen Kazoba amesema mchango wa tamaduni za asili ,mila na desturi katika kukabiliana na maovu katika jamii ni mkubwa hivyo ni muhimu kuziendelea ili kukabiliana na matendo maovu nayowazunguka vijana na watoto.




Discussion about this post