• About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact
Sunday, January 18, 2026
  • Login
Bajeti
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo
No Result
View All Result
Bajeti
No Result
View All Result
Home Habari

Jeshi Niger lakataa amri ya ECOWAS,lapanga safu yake ya uongozi

Mali,Bukina Faso zatuma ujumbe kuwaunga mkono

by bajeti
August 8, 2023
in Habari
0
Jeshi  Niger lakataa amri ya ECOWAS,lapanga safu yake ya uongozi

Watawala wa kijeshi wa Niger wakiwapungia wananchi wa nchi hiyo waliojitokeza kuwashangilia

Share on FacebookShare on Twitter

NIAMEY,NIGER

WAKATI Mataifa ya Afrika Magharibi yanayounda Jumuiya ya Kiuchumi inayojulikana kama (ECOWAS)  kutangaza mkutano mwingine wa dharura kushughulikia mzozo wa kisiasa nchini Niger, Viongozi wa kijeshi wa nchi hiyo wamepuuza amri ya kuachia madaraka.

Katika kuonesha msimamo wake,Kiongozi wa Serikali ya Niger Jenerali Abdourahmane Tchiani amemteua waziri wa zamani wa fedha kuwa waziri mkuu mpya wan chi hiyo.

Waziri Mkuu huyo mpya Ali Mahaman Lamine Zeine anachukua nafasi ya Mahamadou Ouhoumoudou, ambaye alikuwa nchini Italia  wakati wa mapinduzi ambapo Zeine aliwahi kuwa Mkurugenzi wa Baraza la Mawaziri na Waziri wa Fedha kuanzia 2001 hadi kupinduliwa kwa aliyekuwa Rais wa zamani Mamadou Tandja na jeshi mnamo 2010.

Mbali na kuteuliwa Waziri Mkuu mpya lakini pia Jeshi hilo  Agosti 7,2023 ilimteua Brig Jenerali Amadou Didilli kama Mkuu wa Mamlaka ya Juu ya Ujumuishaji wa Amani ya Nchi (HACP) na Brig Jenerali Abou Tague Mahamadou kama Mkaguzi Mkuu wa Jeshi na Jeshi la kitaifa na kumtangaza Kanali Ibro Amadou Bachirou kuwa Mkuu wa Watumishi wa Kijeshi huku  Lt Kanali Habibou Assoumane akiteuliwa kama Kamanda wa Walinzi wa Rais.

Zaidi ya wiki moja iliyopita,ECOWAS inayoongozwa na Mwenyekiti wake Rais wa Naigeria Bola Tinubu waliiamrisha Serikali ya kijeshi iliyompindua Rais Mohamed Bazoum wa Niger kumrejesha madarakani rais huyo ndani ya siku saba , kipindi ambacho kilimalizika Jumapili  na ikiwa watashindwa kufanya hivyo  basi watakabiliwa na uingiliaji kati wa kijeshi ili kurejesha ‘utawala wa kikatiba’.

Hata hivyo Agosti 6,2023 watawala wa kijeshi walijibu kitisho hicho  kwa kufunga anga ya nchi hiyo baada ya muda waliopewa kuondoka madarakani kumalizika hali iliyojumbisha usafiri wa ndege ambazo sasa zinatumia umbali mrefu kufika baadhi ya nchi hasa za Kusini mwa Afrika kutoka Ulaya.

ECOWAS, imetangaza kuitisha mkutano siku ya Alhamisi katika mji mkuu wa Nigeria Abuja utakaoongozwa na Rais Tinubu na watazingatia na kujadili hali ya kisiasa yakiwemo matukio ya hivi karibuni nchini Niger wakati wa mkutano huo.

Wajumbe kutoka serikali za kijeshi za Mali na Burkina Faso wamewahakikishia viongozi wa mapinduzi ya kijeshi ya Niger msaada wao kamili katika ziara yao waliyoifanya siku ya Jumatatu walipokutana na Jenerali Abdourahamane Tchiani katika Mji Mkuu wa Niger,Niamey.

Msemaji wa serikali ya kijeshi ya Mali, Abdoulaye Maiga amesema vikwazo vya ECOWAS dhidi ya Niger ni”kinyume cha sheria, haramu na visivyo vya kibinadamu” na kuongeza kuwa  Burkina Faso, Mali na Niger zimekuwa zikishughulikia “matokeo mabaya ya kijamii na kiuchumi, usalama, kisiasa na kibinadamu ya matukio hatari ya NATO nchini Libya kwa zaidi ya muongo mmoja sasa .”.

Mjumbe huyo wa Mali pia aliwahimiza raia wa Niger kuwa “wastahimilivu na wakali” kupitia “nyakati ngumu” na kuwahakikishia ushindi na msaada wao usioyumba.

Viongozi wa kijeshi wa Mali na Burkina Faso wameonya dhidi ya uingiliaji wa kijeshi wa ECOWAS nchini Niger, wakisema unamaanisha “kutangaza vita na wao wako tayari kupeleka vikosi kuwasaidia wenzao wa Mali dhidi ya kikosi cha ECOWAS”.

Hata hivyo ECOWAS inakabiliwa na wakati mgumu kutokana na maelfu ya wananchi wa Niger kuunga mkono mapinduzi hayo hivyo kuwa tayari kulinda nchi yao dhidi ya wavamizi huku Algeria matumizi ya kijeshi dhidi ya Niger

 

 

 

Next Post
UVCCM yaonya siasa za kukwamisha juhudi za maendeleo

UVCCM yaonya siasa za kukwamisha juhudi za maendeleo

Serikali yaandaa mwongozo Uingizaji, Matumizi na Utupaji Salama wa Zebaki.

Serikali yaandaa mwongozo Uingizaji, Matumizi na Utupaji Salama wa Zebaki.

Maafisa Ununuzi na Ugavi wahimizwa kuzingatia sheria

Maafisa Ununuzi na Ugavi wahimizwa kuzingatia sheria

Discussion about this post

Contact us:

BAJETI COMMUNICATION

info@bajeti.co.tz
bajetinews@gmail.com
+255718699828
P.o.BOX 18133,
DAR ES SALAAM,
TANZANIA

Category

  • Habari
  • Magazeti
  • Makala
  • Mazingira
  • Michezo
  • Picha
  • Sayansi na Teknolojia
  • Siasa

Our Visitors

  • Today's visitors:25
  • Today's page views 25
  • Total visitors 13,182
  • Total page views 14,928

Kuhusu Tovuti Hii

Hii ni tovuti ya habari iliyojikita katika kuandika  habari za kina   zikiwemo za mazingira kwa lengo la kuelimisha na kuuhabarisha umma.

Subscribe

  • About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact

© 2025 Bajeti

No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo

© 2025 Bajeti

Welcome Back!

Login to your account below

Forgotten Password?

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In