• About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact
Tuesday, January 13, 2026
  • Login
Bajeti
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo
No Result
View All Result
Bajeti
No Result
View All Result
Home Siasa

UVCCM yaonya siasa za kukwamisha juhudi za maendeleo

Yasema Uwekezaji wa DP World na Bandari una maslahi ya kuimarisha uchumi wa nchi

by bajeti
August 12, 2023
in Siasa
0
UVCCM yaonya siasa za kukwamisha juhudi za maendeleo

Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Taifa, Mohamed Kawaida, akiwahutubia wanachama wa chama hicho na wananchi (hawapo pichani) katika uwanja wa Chaani Mkoa wa Kaskazini Unguja viziwani Zanzibar Agosti 11,2023(Picha na CCM )

Share on FacebookShare on Twitter

NA  MWANDISHI WETU,ZANZIBAR.

MWENYEKITI wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Taifa, Mohamed Kawaida, amevionya baadhi ya Vyama vya upinzani kuacha siasa za chokochoko zinazolenga kukwamisha juhudi za maendeleo nchini.

Hayo ameyasema Agosti 11,2023 katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika uwanja wa Chaani, Mkoa wa Kaskazini Unguja visiwani Zanzibar na kuongeza kuwa  UVCCM itaendelea kulinda,kutetea na kusimamia maslahi ya Serikali zinazotoka na Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Aidha Kawaida, amevikumbusha vyama hivyo vya upinzani kuwa kizazi kilichofanya Mapinduzi 1964 bado kipo hai, na sasa kimejielekeza katika   utetezi wa Chama,Serikali na viongozi wake.

“Nasaha zangu kwa upinzania wasitumie vibaya fursa ya mikutano ya hadhara kama kichaka cha kutekeleza mipango yao miovu dhidi ya Serikali, badala yake watoe ushauri na maoni ya kuibua hoja na changamoto zinazowakabili wananchi ili zitafutiwe ufumbuzi.”, amesema Kawaida.

Amesema Serikali inaendelea kufanya mambo mengi ya maendeleo kwa nia ya kumaliza changamoto mbalimbali zinazowakabili wananchi wa mijini na vijijini.

Kawaida ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa, amebainisha  kuwa Makubalino ya Uwekezaji baina ya kampuni ya DP World na Bandari ya Dar es saalam una maslahi makubwa ya kuimarisha uchumi wa nchi.

Mohamed, ameongeza kuwa utatuzi wa kero na changamoto za Wananchi Mijini na Vijijini ndio kielelezo cha ushindi wa CCM katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025.

Naye Kaimu Katibu Mkuu wa UVCCM Taifa Mussa Haji Mussa, amewataka  wananchi kupuuza upotoshaji unaofanywa na Chama kimoja cha upinzani wa kudai kuwa Mkoa huo umetelekezwa na hauna maendeleo.

Nao Wajumbe wa Kamati tekelezaji ya UVCCM Taifa wakiwemo Wabunge,Wawakilishi na Wajumbe wa NEC kutoka katika Umoja huo wamesema Serikali zote mbili ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar zimetekeleza kwa ufanisi Ilani ya CCM ya mwaka 2020/2025.

 

Next Post
Serikali yaandaa mwongozo Uingizaji, Matumizi na Utupaji Salama wa Zebaki.

Serikali yaandaa mwongozo Uingizaji, Matumizi na Utupaji Salama wa Zebaki.

Maafisa Ununuzi na Ugavi wahimizwa kuzingatia sheria

Maafisa Ununuzi na Ugavi wahimizwa kuzingatia sheria

Magonjwa yatajwa chanzo cha Mbwamwitu  kutoweka

Magonjwa yatajwa chanzo cha Mbwamwitu kutoweka

Discussion about this post

Contact us:

BAJETI COMMUNICATION

info@bajeti.co.tz
bajetinews@gmail.com
+255718699828
P.o.BOX 18133,
DAR ES SALAAM,
TANZANIA

Category

  • Habari
  • Magazeti
  • Makala
  • Mazingira
  • Michezo
  • Picha
  • Sayansi na Teknolojia
  • Siasa

Our Visitors

  • Today's visitors:5
  • Today's page views 5
  • Total visitors 13,061
  • Total page views 14,806

Kuhusu Tovuti Hii

Hii ni tovuti ya habari iliyojikita katika kuandika  habari za kina   zikiwemo za mazingira kwa lengo la kuelimisha na kuuhabarisha umma.

Subscribe

  • About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact

© 2025 Bajeti

No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo

© 2025 Bajeti

Welcome Back!

Login to your account below

Forgotten Password?

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In