• About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact
Thursday, January 22, 2026
  • Login
Bajeti
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo
No Result
View All Result
Bajeti
No Result
View All Result
Home Habari

Dawa ya kuwatambua ‘wachawi ’yaua watu 50

by bajeti
March 16, 2024
in Habari
0
Dawa ya kuwatambua ‘wachawi ’yaua watu 50

Ramani ya Angola

Share on FacebookShare on Twitter

LUANDA,ANGOLA

WATU  50 wamefariki dunia baada ya kunywa dawa ya mitishamba maarufu kama‘Mbulungo’ waliyopewa na waganga wa kienyeji ili kuthibitisha kama wao ni wachawi au sio.

Jeshi la Polisi nchini humo limethibitisha vifo vya watu hao baada ya kulazimishwa kunywa dawa hiyo ili kuthibitisha kwamba hawakuwa wachawi.

Kwa mujibu wa kituo cha RT kilichonukuu vyanzo vya taarifa hiyo,ilieleza kuwa vifo hivyo vilitokea katika kipindi cha miezi miwili iliyopita karibu na mji wa Camacupa, ambapo  diwani wa eneo hilo Luzia Filemone alinukuliwa na redio ya taifa ya nchi hiyo kuwa waganga hao wa kienyeji walitumia mchanganyiko hatari katika taratibu hizo.

“Zaidi ya waathiriwa 50 walilazimishwa kunywa maji haya ya ajabu, ambayo yanathibitisha  kama mtu anafanya uchawi au la,”amesema  Filemone

Baadhi ya jamii za mashambani katika nchi hiyo ya Kusini mwa Afrika bado wana imani kubwa ya uchawi.

“Ni tabia iliyoenea sana kuwafanya watu wanywe sumu  kwa sababu ya imani ya uchawi,” Msemaji wa Jeshi la Polisi Antonio Hossi amesema.

Hakuna sheria kuhusu vitendo vya uchawi nchini humo na iwapo watu wanashukiwa kuwa wachawi, wanalazimishwa kunywa mchanganyiko wa mitishamba wenye sumu unaojulikana kama ‘Mbulungo’.

Ikiwa watakufa kwa sababu hiyo, inachukuliwa kuwa ushahidi wa wao kuwa wachawi.

 

Next Post
Serikali kuwashirikisha wananchi matokeo ya Sensa ya Watu na Makazi ya mwaka 2022

Serikali kuwashirikisha wananchi matokeo ya Sensa ya Watu na Makazi ya mwaka 2022

CCM-Zanzibar:ACT-Wazaleno haina hati miliki ya Zanzibar

CCM-Zanzibar:ACT-Wazaleno haina hati miliki ya Zanzibar

ZAMBIA

ZAMBIA

Discussion about this post

Contact us:

BAJETI COMMUNICATION

info@bajeti.co.tz
bajetinews@gmail.com
+255718699828
P.o.BOX 18133,
DAR ES SALAAM,
TANZANIA

Category

  • Habari
  • Magazeti
  • Makala
  • Mazingira
  • Michezo
  • Picha
  • Sayansi na Teknolojia
  • Siasa

Our Visitors

  • Today's visitors:18
  • Today's page views 18
  • Total visitors 13,277
  • Total page views 15,025

Kuhusu Tovuti Hii

Hii ni tovuti ya habari iliyojikita katika kuandika  habari za kina   zikiwemo za mazingira kwa lengo la kuelimisha na kuuhabarisha umma.

Subscribe

  • About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact

© 2025 Bajeti

No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo

© 2025 Bajeti

Welcome Back!

Login to your account below

Forgotten Password?

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In