• About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact
Thursday, January 22, 2026
  • Login
Bajeti
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo
No Result
View All Result
Bajeti
No Result
View All Result
Home Habari

Ushirikiano wa Tanzania na Urusi kuzidi kuimarishwa.

Changamoto zinazoikabili dunia kwa sasa ni ugaidi na uhalifu wa mtandao

by bajeti
May 1, 2024
in Habari
0
Ushirikiano wa Tanzania na Urusi kuzidi kuimarishwa.

Waziri wa Katiba na Sheria wa Tanzania Balozi, Dkt. Pindi Chana,akizungumza na Balozi wa Shirikisho la Urusi nchini Tanzania Andrey Avetisyan Aprili 30, 2024 kabla ya kufungua mafunzo yaliyotolewa na wataalamu kutoka Ofisi ya Mwendesha Mashtaka Mkuu wa Serikali ya Urusi, yaliyofanyika katika Taasisi ya Mafunzo ya Uanasheria kwa Vitendo (LST) iliyopo jijini Dar es salaam.

Share on FacebookShare on Twitter

NA MWANDISHI WETU

WAZIRI wa Katiba na Sheria,Balozi, Dkt. Pindi Chana amesema uhusiano na ushirikiano baina ya nchi ya Tanzania na Urusi katika nyanja mbalimbali utazidi kuimarishwa kwa lengo la kuongeza tija na kuchochea maendeleo.

Hata hivyo Uhusiani kati ya Tanzania na Urusi ulianza tangu kipindi cha uongozi wa Hayati Mwl. Julius K. Nyerere.

Dkt. Chana ameyasema hayo Aprili 30,2024 mkoani Dar es Salaam alipokuwa akifungua rasmi mhadhara wa kitaaluma uliofanyika katika Taasisi ya Mafunzo ya Uanasheria kwa Vitendo (LST).

Akizungumzia umuhimu wa mhadhara huo, Balozi Dkt. Pindi Chana amesema kuwa wanafunzi wa sheria kwa vitendo walioshiriki katika mhadhara huo watapata faida kubwa kwa kulinganisha mambo mbalimbali ya kisheria kwa wenzao wa Urusi na kujifunza jinsi ya kutatua changamoto katika harakati za kujiweka salama, kisheria na kiuchumi.

Amesema kuwa tukio hilo ni fursa ya kudumisha na kutekeleza falsafa ya Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan inayojulikana kama 4R hivyo nchi  lazima ishirikiane na nyingine ili kupata ujuzi na uzoefu kutoka kwa wageni.

Ameongeza kuwa mihadhara kama hiyo huleta tija kwa wanafunzi wa fani mbalimbali na kuwaongezea ufahamu na weledi katika masomo yao kwa manufaa yao na taifa.

“Urusi ni wazuri wa mambo ya Teknolojia katika ulinzi na usalama pamoja na masuala ya kisheria hivyo vijana wetu wakijifunza kutoka kwa wataalamu wataongeza ujuzi kwa manufaa yao na nchi yao” ameeleza Dkt. Pindi Chana.

Aidha, Dkt. Chana amesema wataalamu hao kutoka Ofisi ya Mwendesha Mashitaka Mkuu wa Urusi wamekuja kutembelea Tanzania kwa shughuli za kujifunza na kudumisha uhusiano na ushirikiano uliokuwepo hata kabla ya Uhuru.

Balozi wa Shirikisho la Urusi nchini Tanzania Andrey Avetisyan akizungumza Aprili 30, 2024 mkoani Dar es Salaam wakati wa mafunzo yaliyotolewa na wataalamu kutoka Ofisi ya Mwendesha Mashtaka Mkuu wa Serikali ya Urusi, yaliyofanyika katika Taasisi ya Mafunzo ya Uanasheria kwa Vitendo (LST) iliyopo jijini Dar es salaam

Kwa upande wake Balozi wa Shirikisho la Urusi nchini, Andrey Avetisyan ameeleza kufurahishwa na hatua kubwa za kimageuzi katika mifumo ya kisheria nchini Tanzania.

Aidha umefafanuwa kuwa anafurahishwa na mazingira rafiki na mazuri yanayowekwa na Serikali na Tanzania katika uwekezaji na biashara, huku akiwahimiza wawekezaji kutoka Urusi kuja kuwekeza  Tanzania.

Kaimu Mkuu wa Taasisi ya Mafunzo ya Uanasheria kwa Vitendo (LST), Prof. Sist Mramba akizungumza Aprili 30, 2024 mkoani Dar es Salaam wakati wa mafunzo yaliyotolewa na wataalamu kutoka Ofisi ya Mwendesha Mashtaka Mkuu wa Serikali ya Urusi.

Naye Kaimu Mkuu wa Taasisi ya Mafunzo ya Uanasheria kwa Vitendo (LST), Prof. Sist Mramba amesema kuwa kunahitajika ushirikiano wa kimataifa ili kukabili vitendo vya ugaidi na uhalifu wa kimtandao.

“Changamoto zinazoikabili dunia kwa sasa ni ugaidi na uhalifu wa mtandao hivyo kunahitajika ushirikiano wa mataifa mbalimbali katika kupeana ujuzi ili kukabiliana na changamoto zilizopo,” amesema Prof.Mramba.

Mhadhara huo umehudhuriwa na wanafunzi wa taasisi hiyo, wataalamu kutoka Urusi, wadau mbalimbali wa sheria pamoja na wahadhiri wa tasnia ya sheria kutoka vyuo vikuu hapa nchini.

Next Post
James Mbatia:Asante Mahakama

James Mbatia:Asante Mahakama

Wakili Mchau:Mahakama za Tanzania ni za sheria

Wakili Mchau:Mahakama za Tanzania ni za sheria

TMDA:Waandishi andikeni habari za Dawa, Vifaa Tiba na Bidhaa za Tumbaku zenye kuleta tija kwa jamii

TMDA:Waandishi andikeni habari za Dawa, Vifaa Tiba na Bidhaa za Tumbaku zenye kuleta tija kwa jamii

Discussion about this post

Contact us:

BAJETI COMMUNICATION

info@bajeti.co.tz
bajetinews@gmail.com
+255718699828
P.o.BOX 18133,
DAR ES SALAAM,
TANZANIA

Category

  • Habari
  • Magazeti
  • Makala
  • Mazingira
  • Michezo
  • Picha
  • Sayansi na Teknolojia
  • Siasa

Our Visitors

  • Today's visitors:18
  • Today's page views 18
  • Total visitors 13,277
  • Total page views 15,025

Kuhusu Tovuti Hii

Hii ni tovuti ya habari iliyojikita katika kuandika  habari za kina   zikiwemo za mazingira kwa lengo la kuelimisha na kuuhabarisha umma.

Subscribe

  • About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact

© 2025 Bajeti

No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo

© 2025 Bajeti

Welcome Back!

Login to your account below

Forgotten Password?

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In