• About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact
Tuesday, January 13, 2026
  • Login
Bajeti
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo
No Result
View All Result
Bajeti
No Result
View All Result
Home Habari

CPA Kasore:VETA tunatoa watu wenye ujuzi unaohitaji katika soko la ajira

by bajeti
July 6, 2024
in Habari
0
CPA Kasore:VETA tunatoa watu wenye ujuzi unaohitaji katika soko la ajira

Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Ufundi Stadi (VETA) CPA Antony Kasore (kushoto) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) Julai 6,2024 katika Maonesho ya 48 ya Biashara ya Kimataifa Sabasaba yanayoendelea mkoani Dar es Salaam.Kulia ni Mkufunzi wa Useremala na Ujasiriamali VETA Mkoa wa Tanga Yussuph Mkahallah(Picha na Bajeti )

Share on FacebookShare on Twitter

NA GOODLUCK HONGO

MKURUGENZI Mkuu wa Mamlaka ya Ufundi Stadi (VETA) CPA Antony Kasore amesema mamlaka hiyo inatoa watu bora na wenye ujuzi unaohitajika katika soko la ajira.

Mbali na soko la ajira lakini pia inatoa watu wenye ujuzi wa aina mbalimbali wanaohitajika  na wawekezaji ikiwemo pia kujiajiri wenyewe.

Kauli ya CPA Kasore ameitoa Julai 6,2024 katika Banda la VETA  wakati wa Maonesho ya 48 ya Biashara ya Kimataifa  Sabasaba yanayoendelea mkoani Dar es Salaam.

Amesema VETA hufanya utafiti wa soko la ajira kabla ya kuandaa mitaala ya kufundishia hivyo kurahisisha mahitaji ya wawekezaji wanaokuja kuwekeza nchini kupata watu wa kuwaajiri na kutoa fursa za ajira kwa watanzania.

‘’ Sisi VETA tunatoa watu wanaohitajika na wawekezaji,na huu ujuzi tunampatia mtanzania ataweza kuajiriwa sehemu mbalimbali ikiwemo Sekta ya Madini,Ujenzi, Utalii,Uchumi wa Buluu,Viwanda na maeneo mengine lakini pia anaweza kujiari mwenyewe na kujiingizia kipato.

‘’Sisi VETA tunaiangalia kauli mbiu ya Sabasaba inayosema “Tanzania ni Mahali Salama Pa Biashara na Uwekezaji”  tunaiangalia katika kuhakikisha kuwa wawekezaji wanaokuja kuwekeza nchini wanapata watu wenye ujuzi wanaowahitaji  katika fani zote’’amesema CPA Kasore

Hata hivyo CPA Kasore ameongeza kuwa VETA inatoa mafunzo hata kwa wahitimu wa Vyuo Vikuu na kwamba wakati mwingine hufika katika Vijiji na kuangalia fursa zilizopo katika eneo hilo na wao kuandaa mitaala yao ya kufundishia vijana kulingana na fursa zilizopo katika eneo hilo.

Kwa upande wake Mkufunzi wa Useremala wa VETA mkoani Tanga Yusuph Mkahallah amebainisha kuwa yeye anawafundisha vijana jinsi ya kutengeneza thamani za mbao ikiwemo sinia za mbao pamoja na ujasiriamali.

‘’Kwa upande wa ujasiriamali sisi tuna mashine ya kutotoleshea vifaranga vya kuku ambayo inauwezo wa kuweka trei 36 kwa wakati mmoja na ina uwezo wa kukaa masaa 36 bila kuwa na umeme.

‘’Sasa tukishamfundisha ujasiriamali kama huu pindi atakaporudi nyumbani basi ataweza kujiingizia kipato kwa utengenezaji wa thamani za mbao au kwa ujasiriamali huu wa kutumia mashine kutotolesha vifaranga vya kuku zaidi ya 10,000 kwa wakati mmoja’’amesema Mkahallah

Maonesho ya Sabasaba yenye Kauli Mbiu “Tanzania ni Mahali Salama Pa Biashara na Uwekezaji” yameanza Juni 28, 2024 na yanatarajiwa kufikia tamati Julai 14, 2024

Next Post
Bodi ya Mkonge:Mahitaji ya Mkonge ni makubwa kuliko uzalishaji

Bodi ya Mkonge:Mahitaji ya Mkonge ni makubwa kuliko uzalishaji

LATRA ‘yapata dawa’ kwa daladala zinazokatisha njia

LATRA ‘yapata dawa’ kwa daladala zinazokatisha njia

Tani dawa za kulevya ‘zautikisa’ mwaka 2023.

Tani dawa za kulevya ‘zautikisa’ mwaka 2023.

Discussion about this post

Contact us:

BAJETI COMMUNICATION

info@bajeti.co.tz
bajetinews@gmail.com
+255718699828
P.o.BOX 18133,
DAR ES SALAAM,
TANZANIA

Category

  • Habari
  • Magazeti
  • Makala
  • Mazingira
  • Michezo
  • Picha
  • Sayansi na Teknolojia
  • Siasa

Our Visitors

  • Today's visitors:0
  • Today's page views 0
  • Total visitors 13,056
  • Total page views 14,801

Kuhusu Tovuti Hii

Hii ni tovuti ya habari iliyojikita katika kuandika  habari za kina   zikiwemo za mazingira kwa lengo la kuelimisha na kuuhabarisha umma.

Subscribe

  • About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact

© 2025 Bajeti

No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo

© 2025 Bajeti

Welcome Back!

Login to your account below

Forgotten Password?

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In