• About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact
Friday, May 15, 2026
  • Login
Bajeti
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo
No Result
View All Result
Bajeti
No Result
View All Result
Home Habari

TAWA yanadi fursa za uwekezaji maonesho ya Sabasaba 2024

by bajeti
July 15, 2024
in Habari
0
TAWA yanadi fursa za uwekezaji  maonesho ya Sabasaba 2024

Afisa utalii kutoka Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA) Daud Tesha akizungumza jUAI 6,2024 na raia wa kigeni ambaye jina lake halikutaliwa mara moja katika banda la taasisi hiyo wakati wa Maonesho ya 48 ya Kimataifa ya Kibiashara Sabasaba yanayoendelea mkoani Dar es Salaam(Picha na TAWA)

Share on FacebookShare on Twitter

 

NA BEATUS MAGANJA,DAR ES SALAAM

MAMLAKA ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA) inatumia maonesho ya 48 ya kimataifa ya kibiashara yanayoendelea mkoani  Dar es Salaam kuhamasisha Umma wa watanzania na wageni kutoka mataifa mbalimbali kuwekeza katika maeneo inayoyasimamia huku ikijinasibu kuwa na fursa lukuki za uwekezaji.

Akizungumza Julai 6,2024  na wageni waliotembelea banda la TAWA lililopo ndani ya Banda la Wizara ya Maliasili na Utalii Afisa Utalii Daud Tesha amesema TAWA ina uwanda mpana wa fursa za uwekezaji unaotoa mwanya kwa wawekezaji wa aina mbalimbali kuwekeza katika taasisi hiyo

Tesha amesema yapo maeneo mengi yanayohitaji wawekezaji na uwekezaji katika taasisi hiyo kama vile maeneo ya utalii wa picha kwenye maeneo ya hifadhi za Wanyamapori, maeneo ya kihistoria yenye Utalii wa kiutamaduni, eneo la uwekezaji mahiri (Special Wildlife Investment Concession Areas – SWICA), Uwindaji wa Kitalii na Ufugaji wa Wanyamapori

“TAWA imetenga maeneo kadhaa kwa ajili ya kufanyika shughuli za Utalii wa Picha kutokana na ikolojia na aina ya vivutio vilivyopo katika maeneo hayo ikiwemo Pori la Akiba Mpanga/Kipengere eneo ambalo lina maporomoko ya maji zaidi ya 10 yanayotoa burudani safi kwa watalii.

“Maeneo mengine ni Pori la Akiba Wamimbiki, Tabora ZOO, Ruhila ZOO , Makuyuni Wildlife Park ambapo wananchi wanakaribishwa kuwekeza kwenye miundombinu ya Utalii ikiwemo kujenga Kambi za Kulala wageni (Campsites), Hosteli, Loji na maeneo ya mapumziko mafupi kwa watalii (Picnic Sites) amesema Tesha

Watu wakiwa wamejipanga kuingia katika Banda la Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori (TAWA) Julai 6,2024 kushuhudia vivutio mbalimbali wakiwemo wanyamapori katika Maonesho ya 48 ya Biashara ya Kimataifa Sabasaba yanayoendelea mkoani Dar es Salaam

Kwa upande wake Afisa Habari wa TAWA Beatus Maganja ametumia fursa hiyo kuwakaribisha wananchi wote kutembelea Banda la TAWA Ili kupata maelezo ya fursa mbalimbali za uwekezaji zilizopo katika taasisi hiyo.

“Kama kauli mbiu ya Maonesho haya inavyosema kuwa Tanzania ni Mahali Sahihi pa Biashara na Uwekezaji, nitumie fursa hii kuwaambia watanzania wote kuwa TAWA ni Taasisi sahihi kwa biashara na uwekezaji kwani inatoa fursa za uwekezaji wa aina mbalimbali kama vile ujenzi wa loji, kumbi za mikutano katika maeneo yetu, kambi za watalii, michezo ya watoto lakini kama haitoshi mwekezaji anaweza akatumia fursa ya kuwekeza katika mashamba ya wanyamapori, bustani za wanyamapori n k” amesema Maganja

“Kwahiyo hii ni fursa adhimu Kwa wawekezaji wote kutembelea banda letu ili waweze kupata ufafanuzi wa fursa mbalimbali za uwekezaji zilizopo katika taasisi yetu” ameongeza Maganja

Maonesho haya yenye Kauli Mbiu “Tanzania ni Mahali Salama Pa Biashara na Uwekezaji” yameanza Juni 28, 2024 na yanatarajiwa kufikia tamati 14 Julai, 2024

 

Afisa Habari wa Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA) Beatus Maganja akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) Julai 6,2024 wakati wa Maonesho ya 48 ya Biashara ya Kimataifa Sabasaba yanayoendelea mkoani Dar es Salaam
Next Post
CPA Kasore:VETA tunatoa watu wenye ujuzi unaohitaji katika soko la ajira

CPA Kasore:VETA tunatoa watu wenye ujuzi unaohitaji katika soko la ajira

Bodi ya Mkonge:Mahitaji ya Mkonge ni makubwa kuliko uzalishaji

Bodi ya Mkonge:Mahitaji ya Mkonge ni makubwa kuliko uzalishaji

LATRA ‘yapata dawa’ kwa daladala zinazokatisha njia

LATRA ‘yapata dawa’ kwa daladala zinazokatisha njia

Discussion about this post

Contact us:

BAJETI COMMUNICATION

info@bajeti.co.tz
bajetinews@gmail.com
+255718699828
P.o.BOX 18133,
DAR ES SALAAM,
TANZANIA

Category

  • Habari
  • Magazeti
  • Makala
  • Mazingira
  • Michezo
  • Picha
  • Sayansi na Teknolojia
  • Siasa

Our Visitors

  • Today's visitors:12
  • Today's page views 13
  • Total visitors 16,227
  • Total page views 18,400

Kuhusu Tovuti Hii

Hii ni tovuti ya habari iliyojikita katika kuandika  habari za kina   zikiwemo za mazingira kwa lengo la kuelimisha na kuuhabarisha umma.

Subscribe

  • About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact

© 2025 Bajeti

No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo

© 2025 Bajeti

Welcome Back!

Login to your account below

Forgotten Password?

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In