• About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact
Tuesday, January 13, 2026
  • Login
Bajeti
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo
No Result
View All Result
Bajeti
No Result
View All Result
Home Mazingira

Wadau wa mazingira watakiwa kuweka mkazo suala la nishati safi ya kupikia

by bajeti
July 19, 2024
in Mazingira
0
Wadau wa mazingira watakiwa kuweka mkazo suala la nishati safi ya kupikia

Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira) Christina Mndeme akifungua Kikao Kazi cha Wadau cha Kukusanya Maoni Kuhusu Rasimu ya Mpango Kazi wa Taifa wa Masuala ya Jinsia na Mabadiliko ya Tabianchi, jijini Dodoma Julai 19, 2024.

Share on FacebookShare on Twitter

NA MWANDISHI WETU DODOMA

NAIBU Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais  (Mazingira) Christina Mndeme amewataka  wadau wa mazingira nchini kuwekea mkazo suala la nishati safi ya kupikia katika Rasimu ya Mpango Kazi wa Taifa wa Masuala ya Jinsia na Mabadiliko ya Tabianchi.

Amesema hapa nchini wanawake hutumia muda mwingi kutafuta kuni kwa ajili ya kupikia badala ya kufanya shughuli za kujiingizia kipato hivyo ni muhimu kupanga mipango ya kushirikisha nishati safi katika masuala ya kijinsia.

Mndeme ameyasema  hayo wakati akifungua Kikao Kazi cha Wadau cha Kukusanya Maoni Kuhusu Rasimu ya Mpango Kazi wa Taifa wa Masuala ya Jinsia na Mabadiliko ya Tabianchi, jijini Dodoma  Julai 19, 2024.

Amesema athari za mabadiliko ya tabianchi zinaathiri sekta za kiuchumi ambazo wanawake, wanaume, watoto, wazee, vijana na makundi maalum hutegemea kwa maisha yao ya kila siku.

Ameongeza kuwa sababu mbalimbali zikiwemo majukumu yao kijinsia, utamaduni, umri, uchumi, mila na desturi huchangia makundi hayo ya jamii kuathirika na athari za mabadiliko ya tabianchi.

“Hii ni hatua kubwa katika uwezeshaji wa masuala ya jinsia hapa nchini, kama mnavyofahamu, Tanzania ni Mwanachama wa  Mkataba wa Umoja wa Mataifa wa Mabadiliko ya Tabianchi, Itifaki ya Kyoto na Makubaliano ya Paris.

‘’Makubaliano ya Paris yanazitaka Nchi Wanachama kuandaa Mpango Kazi wa utekelezaji wa Programu ya Lima kuhusu masuala ya Jinsia na Mabadiliko ya tabianchi,” amesema Mndeme.

Mkataba huo ulianzishwa mwaka 2014 katika Mkutano wa 20 wa Nchi Wanachama wa Mabadiliko ya Tabianchi (COP20) uliofanyika Lima Mji Mkuu wa Peru.

Madhumuni ya LWPG ni kuzihimiza nchi Wanachama wa Mkataba kuhuisha masuala ya jinsia katika mipango kazi ya kitaifa ili kutekeleza Mkataba na Makubaliano ya Paris,hivyo, Ofisi ya Makamu wa Rais kama Ofisi Kiungo wa Mkataba wa Mabadiliko ya Tabianchi nchini, inaratibu maandalizi ya Mpango Kazi husika.

Hata hivyo,Mndeme amebainisha kuwa  tafiti zimeonesha kuwa nchi zinazoendelea bado hazijahuisha Programu ya Lima katika mipango, sera na mikakati ili kuwezesha kuwa na takwimu za makundi hayo, usawa wa kijinsia, uwezeshaji wanawake katika majadiliano ya kimataifa, uhuishaji wa masuala ya jinsia katika sera, mipango na mikakati ya Taifa na kujenga uwezo wa kifedha, utaalam, fedha na taasisi katika kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi.

Serikali  ya Tanzania tayari  imehuisha masuala ya Jinsia na Mabadiliko ya Tabianchi katika Sera ya Taifa ya Mazingira (2021), Mpango Kabambe wa Mazingira (2022-2032), Mkakati wa Taifa wa Mabadiliko ya Tabianchi (2021-2026) na Mchango wa Taifa wa Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi (2021-2026).

Maandalizi ya Mpango Kazi wa Taifa wa Masuala ya Jinsia na Mabadiliko ya Tabianchi ni mwendelezo ya Jitihada za Serikali katika kukabiliana na mabadiliko ya tabainchi kwa kwa makundi yote ya kijamii ili kuweza kuleta maendeleo endelevu hapa nchini.

Next Post
Serikali yahimiza ulinzi maeneo tengefu na hifadhi za bioanuai

Serikali yahimiza ulinzi maeneo tengefu na hifadhi za bioanuai

Rais Dkt. Samia aagiza kutengenezwa muongozo wa kuwatambua machifu na kazi zao

Rais Dkt. Samia aagiza kutengenezwa muongozo wa kuwatambua machifu na kazi zao

Wanawake zaidi ya 800 wakamatwa wakijihushisha na biashara ya dawa za kulevya

Mikoa 12 wanawake waongoza matumizi dawa za kulevya,Njombe ‘ngoma droo’

Discussion about this post

Contact us:

BAJETI COMMUNICATION

info@bajeti.co.tz
bajetinews@gmail.com
+255718699828
P.o.BOX 18133,
DAR ES SALAAM,
TANZANIA

Category

  • Habari
  • Magazeti
  • Makala
  • Mazingira
  • Michezo
  • Picha
  • Sayansi na Teknolojia
  • Siasa

Our Visitors

  • Today's visitors:1
  • Today's page views 1
  • Total visitors 13,057
  • Total page views 14,802

Kuhusu Tovuti Hii

Hii ni tovuti ya habari iliyojikita katika kuandika  habari za kina   zikiwemo za mazingira kwa lengo la kuelimisha na kuuhabarisha umma.

Subscribe

  • About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact

© 2025 Bajeti

No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo

© 2025 Bajeti

Welcome Back!

Login to your account below

Forgotten Password?

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In