• About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact
Tuesday, January 13, 2026
  • Login
Bajeti
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo
No Result
View All Result
Bajeti
No Result
View All Result
Home Mazingira

Serikali yahimiza ulinzi maeneo tengefu na hifadhi za bioanuai

Yazindua Hifadhi hai ya Rufiji- Mafia- Kibiti-Kilwa (RUMAKI),WWF yaitaja Tanzania kinara wa uhifadhi

by bajeti
July 20, 2024
in Mazingira
0
Serikali yahimiza ulinzi maeneo tengefu na hifadhi za bioanuai

Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Khamis Hamza Khamis akizungumza jambo wakati wa hafla ya uzinduzi wa Hifadhi hai ya Rufiji-Mafia-Kilwa (RUMAKI) iliyofanyika Julai 19, 2024 wilayani Rufiji Mkoa Pwani. Kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Rufiji, Meja Edward Gowele na kushoto ni Mkurugenzi wa Tafiti za Mazingira wa Baraza la Taifa na Hifadhi ya Mazingira (NEMC), Dkt. Menan Jangu.

Share on FacebookShare on Twitter

NA MWANDISHI WETU,RUFIJI

SERIKALI imewataka wananchi na wadau katika Mikoa ya Lindi na Pwani kuendelea kulinda maeneo tengefu na hifadhi ya bioanuai ili kubakisha katika ubora na viwango vilivyoainishwa kitaifa na kimataifa.

Hayo yamesemwa Julai 19, 2024 wilayani Rufiji Mkoa wa Pwani na Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Khamis Hamza Khamis wakati akizindua Hifadhi hai ya Rufiji- Mafia- Kibiti-Kilwa (RUMAKI).

Khamis amesema mifumo ikolojia iliyopo katika hifadhi hai ni miongoni mwa bioanuai muhimu za Ukanda wa Pwani ya Afrika Mashariki inayohifadhi bioanuai nyingi na za kipekee zinazotambulika kitaifa na kimataifa.

”Tunapaswa kufanya kila linalowezekana kuhakikisha kuwa Hifadhi Hai hii ya RUMAKI inabaki kuwa kwenye ubora na viwango vinavyokubalika kwa mujibu wa vigezo vyetu vya ndani na vya UNESCO” amesema Khamis.

Ameongeza kuwa Hifadhi Hai ya RUMAKI ni kielelezo kizuri cha juhudi nyingi zilizofanywa na Serikali kwa kushirikiana na wadau mbalimbali ikiwemo mashirika ya kimataifa kwa miaka mingi ambayo inaenda sambamba na dhamira na malengo ya uhifadhi maeneo tengefu, hifadhi ya malikale na bioanuai.

Aidha Khamis amelitaka Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) kushirikiana na taasisi mbalimbali za Serikali kutayarisha mipango endelevu na shirikishi ya kulinda, kuhifadhi na kuendeleza hifadhi hiyo ili iendelee kubaki katika ubora wake.

Naibu Waziri Khamis amehimiza wananchi kujiepusha na uharibifu wa mazingira ikiwemo uchomaji moto, ukataji misitu ikiwemo mikoko na uvuvi haramu na kuitaka NEMC kutumia mfumo maalum wa tahadhari za majanga ndani ya hifadhi hizo.

Amefafanua kuwa iwapo Hifadhi Hai ya RUMAKI itaendelea kulindwa na kuhifadhiwa kwa kuzingatia viwango na vigezo vya kitaifa na kimatifa itasaidia shughuli endelevu za kijamii, kiuchumi, kitalii na kimazingira na hivyo kubaki katika mtandao wa Hifadhi Hai Duniani.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Tafiti za Mazingira wa Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC), Dkt. Menan Jangu amewapongeza wananchi wa Wilaya za Rufiji, Mafia na Kilwa kwa kuendelea kutunza mazingira juhudi ambazo zimeweza maeneo hayo kutambulika kimataifa.

Amesema NEMC itaendelea kuratibu masuala ya uhifadhi na usimamizi wa mazingira kupitia kwa wananchi na taasisi mbalimbali na kuanisha maeneo yote yenye sifa na vigezo vya kutambulika kimataifa.

”Tunapokuwa na eneo la hifadhi hai lina sifa na malengo makuu matatu ambayo ni maendeleo endelevu, uhifadhi na utunzaji wa viumbe hai vinavyotunzwa kwa faida ya vizazi vya sasa na baadae” amesema Dkt. Menan.

Naye Mwakilishi kutoka Shirika la Kimataifa la Uhifadhi wa Mazingira ulimwenguni (WWF),Joan Itanisa amesema ameishukuru Serikali kwa kuendelea kuunga mkono juhudi za Shirika hilo katika uendelezaji wa miradi ya uhifadhi na usimamizi wa mazingira nchini.

Ameongeza kuwa uzinduzi wa hifadhi hiyo ni moja ya ahadi zilizowekwa na Wakuu wa Nchi mbalimbali  duniani kuwa ifikapo mwaka 2030 asilimia 30 ya eneo la dunia iwe imehifadhiwa na kupongeza juhudi utayari wa Tanzania katika kutekeleza azimio hilo.

“Uzinduzi wa RUMAKI ni ishara kuwa Tanzania ipo mstari wa mbele katika kuwa kinara wa masuala ya uhifadhi…Tutaendelea kushirikiana na Serikali katika kuhakikisha wananchi wanaozunguza hifadhi hizi wanapata manufaa kutokana na uhifadhi huu” amesema Itanisa.

Next Post
Rais Dkt. Samia aagiza kutengenezwa muongozo wa kuwatambua machifu na kazi zao

Rais Dkt. Samia aagiza kutengenezwa muongozo wa kuwatambua machifu na kazi zao

Wanawake zaidi ya 800 wakamatwa wakijihushisha na biashara ya dawa za kulevya

Mikoa 12 wanawake waongoza matumizi dawa za kulevya,Njombe ‘ngoma droo’

Watanzania watakiwa kulinda amani,matunda yake yanawafaidisha wote

Watanzania watakiwa kulinda amani,matunda yake yanawafaidisha wote

Discussion about this post

Contact us:

BAJETI COMMUNICATION

info@bajeti.co.tz
bajetinews@gmail.com
+255718699828
P.o.BOX 18133,
DAR ES SALAAM,
TANZANIA

Category

  • Habari
  • Magazeti
  • Makala
  • Mazingira
  • Michezo
  • Picha
  • Sayansi na Teknolojia
  • Siasa

Our Visitors

  • Today's visitors:9
  • Today's page views 9
  • Total visitors 13,065
  • Total page views 14,810

Kuhusu Tovuti Hii

Hii ni tovuti ya habari iliyojikita katika kuandika  habari za kina   zikiwemo za mazingira kwa lengo la kuelimisha na kuuhabarisha umma.

Subscribe

  • About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact

© 2025 Bajeti

No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo

© 2025 Bajeti

Welcome Back!

Login to your account below

Forgotten Password?

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In