• About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact
Tuesday, January 13, 2026
  • Login
Bajeti
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo
No Result
View All Result
Bajeti
No Result
View All Result
Home Makala

NHC kuleta mageuzi makubwa ya kiuchumi Mkoa wa Lindi kupitia Mradi wake wa Mtanda Complex

Yafanya maboresho mkubwa ya majengo yake

by bajeti
November 15, 2024
in Makala
0
NHC kuleta mageuzi makubwa ya kiuchumi Mkoa wa Lindi kupitia Mradi wake wa  Mtanda Complex

Muonekano wa jengo la Mtanda Complex linalojengwa na Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) mkoani Lindi

Share on FacebookShare on Twitter

 

NA MWANDISHI WETU,LINDI

SHIRIKA la Nyumba la Taifa (NHC) limeendelea kuwa chachu ya maendeleo katika Mkoa wa Lindi kwa kutoa huduma bora za makazi na biashara kupitia mradi wa kisasa wa Mtanda Complex pamoja na maboresho ya majengo yake katika mkoa huo.

Mradi wa Mtanda Complex, ulioanza ujenzi kwa kujenga maduka na ofisi kwa taasisi za kifedha, umekuwa chanzo cha fursa za kiuchumi na ajira kwa wakazi wa Lindi. Aidha, maboresho ya majengo ya NHC yamelenga kuboresha mazingira ya biashara na makazi kwa wapangaji wake katika mkoa huo.

Meneja wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) Mkoa wa Lindi Omari Makalamangi

NHC yajenga fursa za kibiashara kwa wakazi wa Lindi

Kwa mujibu wa Bw.Omari Makalamangi, Meneja wa NHC Mkoa wa Lindi, mradi wa Mtanda Complex umefungua milango kwa wazabuni na wasambazaji wa vifaa vya ujenzi, huku ukitoa ajira kwa zaidi ya vibarua 100. Mradi huu ulioanza rasmi Julai 7, 2024, unaendelea katika hatua ya awali ya uchimbaji wa msingi, uwekaji wa nondo za zege, na kumwaga zege. “Mradi huu uko katika hatua za mwanzo za ujenzi, ambapo kazi zinaendelea kwa kasi ili kuhakikisha unakamilika kwa wakati,” alieleza Bw. Makalamangi wakati akizungumza hivi karibuni na Maisha ni Nyumba.

Mafundi wakiendelea na ujenzi wa jengo la kisasa la biashara la Mtanda Complex linalojengwa mkoani Lindi na Shirika la Nyumba la Taifa (NHC)

Mradi huu unakadiriwa kugharimu Sh. Bilioni 4.2 na unatarajiwa kukamilika ifikapo Desemba 31, 2025. Kulingana na Bw. Makalamangi, mradi wa Mtanda Complex unatoa nafasi za biashara kwa wakazi wa Lindi na kuongeza kipato kwa wajasiriamali wadogo kama mama lishe na baba lishe wanaowahudumia wafanyakazi wa mradi.

Mafundi wakiendelea na kazi za ujenzi wa jengo la kisasa la kibiashara la Mtanda Complex linalojengwa na Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) Mkoa wa Lindi

Manufaa kwa Wazabuni wa Vifaa vya Ujenzi

Askari kutoka kampuni ya ulinzi mkoani Lindi (ambaye jina lake halipatikana) akilinda vifaa vya ujenzi katika eneo la mradi wa Mtanda Complex ambao umetoa ajira kwa wakazi wengi wa mkoa huo yakiwemo makampuni ya ulinzi

NHC imetoa fursa kwa makampuni mbalimbali katika Mkoa wa Lindi kushiriki kwenye mradi huu kupitia usambazaji wa vifaa vya ujenzi. Miongoni mwa makampuni yaliyonufaika na mradi huu ni Lindi World Distributor na AG Autos, ambayo yamesambaza vifaa kama saruji, nondo, na mchanga kwa ajili ya ujenzi wa msingi. Ushirikiano huu ni sehemu ya mikakati ya NHC ya kuwawezesha wazabuni wa ndani na kuchochea maendeleo ya kiuchumi katika mkoa huu.

Mashine ikihamisha udongo katika eneo la ujenzi wa Mradi wa Mtanda Complex mkoani Lindi

“Mafanikio ya mradi huu yanadhihirisha juhudi za NHC za kuwahusisha wazabuni wa ndani katika miradi yake. Ushirikiano huu unasaidia kuimarisha uchumi wa ndani na kuwapatia fursa za kujiongezea kipato,” anasema Bw. Makalamangi.

Maboresho ya Majengo ya NHC Lindi

Majengo ya NHC Mkoa wa Lindi

Pamoja na mradi wa Mtanda Complex, NHC imefanya maboresho makubwa kwenye majengo yake katika Mkoa wa Lindi, ili kuboresha mazingira ya biashara na makazi kwa wapangaji wake. Kwa sasa, majengo 12 kati ya 16 ya NHC yamekamilika kuboreshwa, huku majengo manne yaliyosalia yakiwa yanaendelea kufanyiwa ukarabati. Maboresho haya yanalenga kuboresha mandhari ya mji na kuvutia wawekezaji zaidi katika mkoa wa Lindi.

Bw. Makalamangi anasisitiza kuwa maboresho haya yanaendana na dhamira ya NHC ya kuhakikisha kuwa huduma bora za makazi na biashara zinapatikana kwa wapangaji wake. “NHC inalenga kutoa huduma za hali ya juu kwa wapangaji wake na kuhakikisha kwamba mazingira ya biashara na makazi yanakidhi viwango vya kisasa,” alisema.

Maendeleo ya NHC katika Mkoa wa Lindi

Kupitia mradi wa Mtanda Complex na maboresho ya majengo yake, NHC inachangia kikamilifu katika maendeleo ya kiuchumi ya Mkoa wa Lindi. Mradi huu ni sehemu ya mpango mpana wa NHC wa kupanua uwekezaji katika mikoa mbalimbali ya Tanzania na kuongeza nafasi za ajira na biashara. Aidha, NHC inachangia kukuza sekta ya huduma za kifedha na biashara katika mkoa huo, na hivyo kusaidia wakazi wa Lindi kufikia huduma bora karibu nao.

Nyumba za Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) mkoani Lindi baada ya kufanyiwa ukarabati

Kwa juhudi hizi, Shirika la Nyumba la Taifa limeendelea kuwa mshirika muhimu katika maendeleo ya Lindi, likileta mageuzi ya kiuchumi na kijamii kwa wakazi wa mkoa huo kupitia miradi yake ya kisasa na yenye manufaa kwa jamii.

 

Next Post
NHC kuitambulisha Masasi na Masasi Commercial Complex

NHC kuitambulisha Masasi na Masasi Commercial Complex

Taasisi ya Hizb ut Tahrir / Tanzania yalaani mauaji yanayoendelea Gaza

Taasisi ya Hizb ut Tahrir / Tanzania yalaani mauaji yanayoendelea Gaza

Rais Dkt.Pezeskhian wa Iran amshukuru Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan

Rais Dkt.Pezeskhian wa Iran amshukuru Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan

Discussion about this post

Contact us:

BAJETI COMMUNICATION

info@bajeti.co.tz
bajetinews@gmail.com
+255718699828
P.o.BOX 18133,
DAR ES SALAAM,
TANZANIA

Category

  • Habari
  • Magazeti
  • Makala
  • Mazingira
  • Michezo
  • Picha
  • Sayansi na Teknolojia
  • Siasa

Our Visitors

  • Today's visitors:5
  • Today's page views 5
  • Total visitors 13,061
  • Total page views 14,806

Kuhusu Tovuti Hii

Hii ni tovuti ya habari iliyojikita katika kuandika  habari za kina   zikiwemo za mazingira kwa lengo la kuelimisha na kuuhabarisha umma.

Subscribe

  • About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact

© 2025 Bajeti

No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo

© 2025 Bajeti

Welcome Back!

Login to your account below

Forgotten Password?

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In