NA MWANDISHI WETU
‘MAUAJI ya kimbari’ yanayoendelea katika Mamkala ya Ndani ya Palestina katika eneo la Ukanda wa Gaza yameendelea kulaaniwa na taasisi mbalimbali za kimataifa huku Afrika Kusini ikiwa ndio nchi pekee barani Afrika kuishitaki Israel katika Mahakama ya Kimataifa ya Haki (ICJ) kupinga mauaji hayo ya kiholela yanayofanya na Taifa la Israel.
Israel ambayo imekuwa ikibomoa nyumba za kuishi,hospitali,miundombinu ya barabara,shule,maji,umeme na kuuwa kila anayeonekana mbele ya macho yao kwa kile inachodai kupigana na kundi la Hamas ambalo lilifanya shambulizi mnano Oktoba 7,2023 na kuuwa watu zaidi ya 1000 na kuwateka nyara raia zaidi ya 250 wa Israel.
Hadi sasa zaidi ya watu 43000 wameuawa kwa upande wa Gaza pekee ambapo baadhi ya picha zikionesha mitaa mingi ikiwa imejaa vifusi vya nyumba zilizobomolewa ambapo wengi wa waliofariki ni watoto na wanawake huku wapiganaji wa Hamas wakiendelea na mapigano bila kuchoka.
Kutokana na mauaji hayo,Taasisi ya Hizb ut Tahrir / Tanzania imeungana na mataifa mengine duniani kutoa wito wa usitishwaji wa vita hivyo vilivyogharimu maisha ya maelfu ya watu na mchakato wa amani uanze mara moja.
Akizungumza na waandishi wa habari mwishoni mwa wiki mkoani Dar es Salaam ,Mwakilishi wa vyombo vya habari wa taasisi hiyo Masoud Mselem amesema wanapinga mauaji yanayofanywa na Israel katika eneo la Ukanda wa Gaza,Lebanon,Syria na kuongeza kuwa nchi zilizo jirani zipeleka majeshi yao katika maeneo hayo ili kusimamisha vita hivyo.
Amesema kwa wao walioko mbali na maeneo hayo basi waendelea kutoa kauli na kuomba dua ili vita hivyo viishe na maisha ya raia yaendelee kama ilivyokuwa awali
‘’Kwa upande wetu sisi tuliye mbali tutaomba dua kwa ajili ya ndugu zetu na hii ndio dhamira kuu ili kuwanusuru ndugu zetu hasa wanawake na watoto ambao wanagandamizwa na kuuwa kama kuku’’amesema Mselem
Mselem ameongeza kuwa ni zaidi ya mwaka mmoja sasa Israel ikisaidiwa na nchi za Magharibi ikiwemo Marekani,Uingereza,Ufaransa na Ujerumani wamendelea kwa mfufulizo kuuwa watu kwa kubomoa kila kitu na sasa Israel inaendelea kushambulia nchi sita katika eneo hilo.
‘’Gaza imeshateketezwa,Gaza imeshamalizwa na sasa Israel wanaendelea Lebanon na sehemu zingine,ni zaidi ya mwaka mmoja sasa Israel wakisaidiwa na nchi za magharibi wameendelea kwa mfululizo kuuwa watu kwa halaiki,kubomoa majengo,kubomoa miundominu,kubomoa nyumba za ibada (Misikiti),vituo vya afya na kufanya kila kitu ambacho hakipaswi kufanyiwa mwanadamu.
‘’Mpaka sasa karibu watu 43.000 wameshauawa,lakini hawakuishia hapo tu kubomoa nyumba,vituo vya afya bali pia hata mahema ambayo watu walikuwa wamekaa na kujificha na kujisitiri lakini bado Israel wanaendelea kupiga na kuuwa usiku na mchana’’amesema Mselem
Mselem amebainisha kuwa inashangaza kuona Nchi za Magharibi zikiisaidia Israel katika vita hivyo lakini haitaki kuona nchi zingine zikiwasaidia Wapalestina kupata misaada mingine na kujiona wao ndio wenye haki pekee ya kufanya chochote watakacho ulimwenguni.
‘’Kama nchi za Magharibi zinaisaidia Israel ambayo badala ya kupamba na Hamas wao wanaua raia na kuharibu miundombinu yote kwa makusudia na kuuwa maelfu ya raia kwa umati na wakati mwingine kuwanyima hata chakula ili wafe,ni wakati sasa kwa nchi zingine ikiwemo Saudi Arabia,Misri,Jordan,Iran,Uturuki na zingine kupeleka majeshi yao kupambana na Israel kama wanavyofanya nchi za Magharibi kwa Israel.
‘’Wao wakiisaidia Israel ni sawa lakini Palestina ikisaidiwa ni kosa sasa hapo haki iko wapi,ni lazima sasa nchi hizo na zingine kupeleka majeshi yao ili kusimamisha mauaji hayo ya makusudi yanayofanywa na Israel na washirika wao wa magharibi.
‘’Misri na nchi zingine zikitaka kuingilia ili kuzuia mauaji hayo,inaambiwa jambo hilo haliwahusu,ni jambo la ndani lakini mbona nchi za magharibi ikiwemo Marekani.Ufaransa,na zingine ziko mbali kabisa na Israel lakini ndio zinaongoza kwa kupeleka misaada ya kijeshi wakiwemo askari na zana za kijeshi kwa Israel?sasa nazo nchi hizi zipeleke majeshi yao kwa wingi kuzuia umwagikaji mkubwa wa damu unaofanywa na Israel.
Mmoja wa wakazi wa Jiji la Dar es salaam John Shaibu amesema kwa sasa inatosha kwa Israel kwa mauaji na uharibifu walioufanya Gaza,Lebanon,Syria,Yemen na maeneo mengine kwani idadi ya watu waliouawa hadi sasa wanaweza kufikia 100000 ukijumlisha maeneo yote hayo.
‘’Umelipiza kisasa,lakini pambana na hao waliofanya shambulizi sasa wewe kila siku unaharibu barabara,nyumba,vyanzo vya maji,umeme,shule hata mahema na mbaya zaidi hata Shule na Ofisi za Umoja wa Mataifa wanabomoa sasa hawa watu kweli wana dini au dini ipo kwa ajili ya kutawala nchi zingine zisipinge ukandamizwaji’’amesema Shaibu
Hata hivyo licha ya Israel kushambulia kwa hasira eneo la Gaza na kuwauwa viongozi wa kundi la Hamas lakini hadi sasa si Israel wala washirika wao wenye silaha za kisasa,ndege vita,magari na matumizi ya teknolojia ya hali ya juu wameshindwa kabisa kujua mateka waliotekwa na Hamas wamefichwa wapi.
Kitendo hicho kinaonekana kuwapa hasira nchi za Magharibi na Israel kwa kuwa ikiwa watakubali kusitisha vita bila kupatikana kwa mateka zaidi ya 90 wanaoshikiliwa na Hamas itakuwa ni sawa na kushindwa vita hivyo na kundi dogo lisilokuwa na ndege vita za kisasa,silaha,magari ya deraya wala kuungwa mkono kijeshi na mataifa mengi duniani.




Discussion about this post