• About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact
Tuesday, January 13, 2026
  • Login
Bajeti
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo
No Result
View All Result
Bajeti
No Result
View All Result
Home Makala

NHC kuitambulisha Masasi na Masasi Commercial Complex

Ni Mkandarasi wa majengo 'Plus A'

by bajeti
November 15, 2024
in Makala
0
Share on FacebookShare on Twitter

NA GOODLUCK HONGO,MTWARA

SHIRIKA  la Nyumba la Taifa (NHC) limeendelea kuwa chachu ya maendeleo katika Mkoa wa Mtwara  kwa kutoa huduma bora za makazi na biashara kupitia mradi wa kisasa wa Masasi Commercial  Complex pamoja na maboresho ya majengo yake katika mkoa huo.

Mradi wa Masasi Commercial Complex, ulioanza ujenzi kwa kujenga maduka ya kuuza bidhaa mbalimbali ,huduma za hoteli zikiwemo ,kumbi mbalimbali za kufanyia mikutano ,ofisi na huduma pia za kibenki, umekuwa chanzo cha fursa za kiuchumi na ajira kwa wakazi wa Masasi.

Aidha,ujenzi wa nyumba 50 katika wilaya hiyo na  maboresho ya majengo ya NHC mkoani humo yamelenga kuboresha mazingira ya biashara na makazi kwa wapangaji wake katika mkoa huo.

Meneja wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) Mkoa wa Mtwara Joseph John Mwabusila akizungumza na waandishi wa habari kutoka Bajeti Communiction mkoani humo hivi karibuni

NHC yajenga fursa za kibiashara kwa wakazi wa Mtwara

Kwa mujibu wa Joseph Mwabusila, Meneja wa NHC Mkoa wa Mtwara, Mradi wa Masasi Commercial Complex umefungua milango kwa wazabuni na wasambazaji wa vifaa vya ujenzi, huku ukitoa ajira kwa vibarua wengi . Mradi huu kwa sasa unaendelea katika hatua nyingine baada ya kumaliza eneo la chini(underground),

‘’Mradi huu unatoa fursa kwa wakazi wa Mtwara na nchi jirani ya Msumbiji kwani Masasi ni centre,ukiwa Masasi unaweza kwenda Wilaya ya Nachingwea,Liwale,Ruangwa,Newala,Nanyumbu,Mkoa wa Ruvuma,Dar es Salaam na nchi jirani ya Msumbiji

“Mradi huu uko katika hatua za mwanzo za ujenzi, ambapo kazi zinaendelea kwa kasi ili kuhakikisha unakamilika kwa wakati.

 ‘’NHC tumefanya upembuzi yakinifu na tumegundua mwenendo wa uchumi wa wananchi wa Mtwara,na Wilaya ya Masasi ni eneo ambalo maendeleo yake yanakuwa kwa kasi sana na mradi huu unatoa fursa za ajira kwa wafanyakazi mbalimbali lakini pia utaongeza fursa za ajira kwa wakazi wa Masasi na Mkoa wa Mtwara’” ameeleza Mwabusila  wakati akizungumza hivi karibuni na Bajeti Communication

NHC ni  mkandarasi mzoefu katika ujenzi wa majengo

NHC pia ni wakandarasi wazoefu wa majengo ya aina mbalimbali licha ya kujenga nyumba za kuuza na kupangisha lakinia pia ujenzi wa maghalambalimbali ya kuhifadhi bidhaa yakiwemo mazao.NHC mkoani Mtwara wamejenga majengo ya kisasa na bora ambayo mengine yameanza kutumika .

Kwa mujibu wa Mwabusila moja ya majengo yaliyojengwa na NHC mkoani Mtwara ni pamoja na Hospitali ya Rufaa Kanda ya Kusini-Mtwara na kuyakamilisha kwa wakati na kwa viwango vinavyokubalia ambapo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan alikwenda kuifungua hospitali hiyo Septemba 15,2023.

Kukamilika kwa wakati wa Jengo la Hospitali hiyo kunawanufaisha wakazi wa mikoa ya Lindi,Mtwara,Ruvuma na nchini jirani za Msumbiji na Visiwa vya Comoro ambapo kwa sasa imeondoa gharama kwa wananchi wa eneo hilo kusafiri mikoa mingine kutafuta huduma za kibingwa za madaktari bingwa.

Jengo la Hospitali ya Rufaa Kanda ya Kusini-Mtwara lililojengwa na Shirika la Nyumba la Taifa (NHC)

Mradi mwingine ambao NHC imejenga kama mkandarasi ni wa Jengo la OPD la Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mtwara Regula ambao nao umeshakamilika kwa viwango bora na kwa wakati na yatari wameshakabidhi

‘’Sisi ni wakandarasi wazoefu na ni Plus A,tumejenga Hospitali ya Kanda Musoma,Hospitali ya Rufaa Kanda ya Kusini,Jengo la OPD la Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Mtwara na yote hayo yamekamilika kwa wakati na kwa viwango bora hivyo sisi pia tunaomba tenda za ujenzi kama wanavyoomba wakandarasi wengine,sisi pia tunaaminika kwa kuwa ni Shirika la Nyumba la Taifa’’anasema Mwabusila

Jengo la OPD katika Hopsitali ya Rufaa Mkoa wa Mtwara (Regula) lililojengwa na Mkandarasi Shirika la Nyumba la Taifa (NHC)

Msimamizi wa Ujenzi pamoja na Matengenezo  wa NHC mkoani Mtwara, Mhandisi Aman Baraka anasema jengo la OPD la Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mtwara (Regula) limegharimu kiasi cha Sh,Bilioni 2.5 na kubainisha kuwa wamelijenga kwa viwango vya hali ya juu na kasha kulikabidhi.

Msimamizi wa Ujenzi pamoja na Matengenezo wa NHC Mkoa wa Mtwara Mhandisi Aman Baraka

Maboresho ya majengo ya NHC Mtwara

Pamoja na Mradi wa Masasi Commercial Complex, NHC imefanya maboresho makubwa kwenye majengo yake katika Mkoa wa Mtwara , ili kuboresha mazingira ya biashara na makazi kwa wapangaji wake.

Mwabusila anafafanuwa kuwa kufanya maboresho katika nyumba zao ni jukumu lao la msingi ili kuhakikisha nyumba zinakuwa katika mazingira bora kwani kuna maboresho ya dharula na yale ya muda mrefu ambayo yanahitaji ukarabati mkubwa.

‘’Baada ya maboresho na mazingira bora ya nyumba zetu basi jukumu letu lingine ni kukusanya kodi kwa asilimia 100 kwa wapangaji wote wenye mikataba hai na NHC’’anaongeza Mwabusila

Mwabusila anasisitiza kuwa maboresho haya yanaendana na dhamira ya NHC ya kuhakikisha kuwa huduma bora za makazi na biashara zinapatikana kwa wapangaji wake. “NHC inalenga kutoa huduma za hali ya juu kwa wapangaji wake na kuhakikisha kwamba mazingira ya biashara na makazi yanakidhi viwango vya kisasa.

‘’Ni kosa mpangaji kuhama na kumuweka mtu mwingine ndani ya nyumba bila taarifa na hilo tukiligundua basi tunachukua hatua,lakini pia ni muhimu kwa watanzania na wakazi wa Mtwara kufika katoka Ofisi za NHC kupata taarifa sahihi za kupata nyumba za kununua au kupanga maana unaweza kupata nyumba za NHC kwa kupanga,kununua au mpangaji mnunuzi ambaye utalipa kodi halali na kuongeza kiasi kingine hadi utakapomaliza na kukabidhiwa nyumba yako’’anabainisha Mwabusila

NHC inachangia maendeleo ya kiuchumi mkoani Mtwara

Kupitia mradi wa Masasi Commecial Complex na maboresho ya majengo yake, NHC inachangia kikamilifu katika maendeleo ya kiuchumi ya Mkoa wa Mtwara. Mradi huu ni sehemu ya mpango mpana wa NHC wa kupanua uwekezaji katika mikoa mbalimbali ya Tanzania na kuongeza nafasi za ajira na biashara. Aidha, NHC inachangia kukuza sekta ya huduma za kifedha na biashara katika mkoa huo, na hivyo kusaidia wakazi wa Mtwara kufikia huduma bora karibu nao.

Kwa juhudi hizi, Shirika la Nyumba la Taifa limeendelea kuwa mshirika muhimu katika maendeleo ya Mtwara, likileta mageuzi ya kiuchumi na kijamii kwa wakazi wa mkoa huo kupitia miradi yake ya kisasa na yenye manufaa kwa jamii.

Next Post
Taasisi ya Hizb ut Tahrir / Tanzania yalaani mauaji yanayoendelea Gaza

Taasisi ya Hizb ut Tahrir / Tanzania yalaani mauaji yanayoendelea Gaza

Rais Dkt.Pezeskhian wa Iran amshukuru Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan

Rais Dkt.Pezeskhian wa Iran amshukuru Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan

ACT-Wazalendo kufanya kampeni nchi nzima Uchaguzi Serikali za Mitaa

ACT-Wazalendo kufanya kampeni nchi nzima Uchaguzi Serikali za Mitaa

Discussion about this post

Contact us:

BAJETI COMMUNICATION

info@bajeti.co.tz
bajetinews@gmail.com
+255718699828
P.o.BOX 18133,
DAR ES SALAAM,
TANZANIA

Category

  • Habari
  • Magazeti
  • Makala
  • Mazingira
  • Michezo
  • Picha
  • Sayansi na Teknolojia
  • Siasa

Our Visitors

  • Today's visitors:1
  • Today's page views 1
  • Total visitors 13,057
  • Total page views 14,802

Kuhusu Tovuti Hii

Hii ni tovuti ya habari iliyojikita katika kuandika  habari za kina   zikiwemo za mazingira kwa lengo la kuelimisha na kuuhabarisha umma.

Subscribe

  • About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact

© 2025 Bajeti

No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo

© 2025 Bajeti

Welcome Back!

Login to your account below

Forgotten Password?

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In