NA MWANDISHI WETU
SHILINGI ya Tanzania imeimarika dhidi ya dola ya Marekani katika wiki za hivi karibuni hatua ambayo ni habari njema kwa wazalishaji wa viwandani, waagizaji wa magari na watumiaji wa mafuta, miongoni mwa wengine.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na kituo cha habari cha China cha CRI kinachomilikiwa na Serikali ya nchi hiyo ya Novemba 29,2024, imenukuu takwimu rasmi kutoka Benki Kuu ya Tanzania (BoT) zinazoonesha kuwa, sarafu ya ndani imepanda thamani kwa karibu asilimia tatu katika kipindi cha mwezi mmoja uliopita.
‘’Oktoba 25, 2024, BoT ilinukuu dola moja ikibadilishwa kwa Sh2,703.6/ Sh2,730.64; lakini hadi jana, thamani ya shilingi ilikuwa imeongezeka hadi Sh2,652.84/Sh2,652.1.
‘’Kiwango cha wastani cha kubadilisha fedha kiliimarika kutoka Sh2,717.122 Oktoba 25 hadi Sh2,638.97 kufikia jana.
Kuimarika kwa shilingi kunatarajiwa kuleta utulivu au kupunguza gharama za bidhaa kubwa zinazoagizwa, ikiwa ni pamoja na bidhaa za mafuta, magari na vipuri vyake, sukari kwa matumizi ya viwandani, bidhaa za dawa, chuma na vyuma, pamoja na vitu vyote hivi, kwa kawaida huchangia sehemu kubwa ya gharama za uagizaji Tanzania.



Discussion about this post