• About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact
Thursday, January 22, 2026
  • Login
Bajeti
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo
No Result
View All Result
Bajeti
No Result
View All Result
Home Mazingira

Waziri Mavunde asimamisha shughuli za uchimbaji madini katika Mto Zila

Akemea wananchi kujichukulia sheria mkononi kwa kuharibu mali  za mwekezaji

by bajeti
December 31, 2024
in Mazingira
0
Waziri Mavunde asimamisha shughuli za uchimbaji madini katika Mto Zila

Waziri wa Madini Antony ,Mavunde (mwenye kofia) akitoa maelezo ya kufungwa kwa shughuli za uchimbaji madini katika Mto Zila uliopo katika Kijiji cha Ifumbo, wilayani Chunya Mkoa wa Mbeya Desemba 30,2025

Share on FacebookShare on Twitter

NA MWANDISHI WETU,MBEYA

WAZIRI wa Madini,Anthony Mavunde amesimamisha shughuli za uchimbaji madini zilizokuwa zikifanywa na Kampuni ya G & I Tech Mining Company Ltd kwa kipindi cha masika hadi itakapofanyika tathmini ya kitaalam ya mazingira  juu ya shughuli za uchimbaji kwenye Mto Zila.

Mavunde ametoa agizo hilo Desemba 30, 2024 katika Kijiji cha Ifumbo, wilayani Chunya Mkoa wa Mbeya wakati alipotembelea eneo la leseni ya mwekezaji ambalo lilivamiwa na wananchi na kusababisha mgogoro mkubwa na uharibifu wa mali .

“Tumetembelea maeneo yote mawili, na sote tumejionea hali halisi ya mazingira,ni dhamira na maelekezo ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kuona shughuli zote za kiuchumi hususani  za madini zinafanyika kwa utulivu bila kuleta migogoro na pasipo kuathiri mazingira ya eneo shughuli zinapofanyika.

‘’Nimesikiliza hoja za wananchi juu ya uharibifu  wa mazingira ya Mto Zila,Serikali itaunda Timu ya wataalamu kufanya tathmini ya kina ya mazingira juu ya athari zinazoweza kutokea wakati wa uchimbaji wa madini na kwasasa shughuli zote za uchimbaji madini zisimame kipindi hiki cha masika kama Baraza la Usimamizi wa Mazingira (NEMC ) ilivyoelekeza”amesema Mavunde

Wakazi wa Kijiji cha Ifumbo, wilayani Chunya Mkoa wa Mbeya wakimsikiliza Waziri wa Madini Antony ,Mavunde Desemba 30,2025 wakati alipotembelea eneo hilo kutatua mgogoro wa wananchi hao na mwekezaji mwenye leseni ya uchimbaji madini kutoka Kampuni ya G & I Tech Mining Company Ltd

Amebainisha kuwa Wizara ya Madini kwa kushirikiana na watalaam wa mazingira, mkoa na wananchi katika muda mfupi ujao inakwenda kuunda Timu ya pamoja ya kufanya tathmini ili kueleza kitaalam iwapo shughuli hizo zinaweza kuendelea kufanyika pasipo athari kwenye mazingira ya Mto Zila.

‘’Nitumie fursa hii kuwataka wananchi wote kuacha vitendo vya uvunjifu wa amani na kujichukulia sheria mkononi,tunalaani kitendo cha kuvamia na kuharibu mali za mwekezaji“amesema Mavunde

Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Juma Homera akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Ifumbo, wilayani Chunya Mkoa wa Mbeya wakati wa ziara ya Waziri wa Madini Antony Mavunde Desemba 30,2025.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Mbeya,Juma  Homera, amemshukuru Waziri  Mavunde kwa kutembelea chunya na kuahidi kwamba atasimamia maelekezo yake ya kuona shughuli za uchimbaji katika Mto Zila zinasimama kipindi hiki cha masika mpaka pale watalaam watakapokamilisha taarifa ya tathmini na kutoa mapendekezo.

Awali, akitoa maelezo juu ya mgogoro huo, Mkuu wa Wilaya ya Chunya, Mbaraka  Batenga amesema sasa anaona mwanga ambao unakwenda kuleta suluhisho la kudumu katika mgogoro baina ya mwekezaji na wananchi wa kijiji cha Ifumbo na kuwa Serikali ngazi ya wilaya itaendelea kusimamia sheria na kanuni ili kuhakikisha eneo hilo linakuwa salama muda wote.

Mbunge wa Jimbo la Chunya,  Masache Kasaka kwa niaba ya wananchi ameishukuru Serikali kwa namna inavyoshughulikia changamoto za wananchi na kueleza kuwa ombi la wananchi ni kuona mazingira ya Mto Zila yanatunzwa kwa kuwa  ni chanzo kikubwa cha maji kwa Wilaya ya Chunya.

 

Next Post
Tanzania,Uingereza kushirikiana kuendeleza  Sekta ya Madini

Tanzania,Uingereza kushirikiana kuendeleza Sekta ya Madini

Matumizi ya baruti yafikia tani 26.5 mwaka 2024

Matumizi ya baruti yafikia tani 26.5 mwaka 2024

Rais Dkt.Samia amteua Mhandisi Lwamo kuwa Katibu Mtendaji Tume ya Madini

Rais Dkt.Samia amteua Mhandisi Lwamo kuwa Katibu Mtendaji Tume ya Madini

Discussion about this post

Contact us:

BAJETI COMMUNICATION

info@bajeti.co.tz
bajetinews@gmail.com
+255718699828
P.o.BOX 18133,
DAR ES SALAAM,
TANZANIA

Category

  • Habari
  • Magazeti
  • Makala
  • Mazingira
  • Michezo
  • Picha
  • Sayansi na Teknolojia
  • Siasa

Our Visitors

  • Today's visitors:18
  • Today's page views 18
  • Total visitors 13,277
  • Total page views 15,025

Kuhusu Tovuti Hii

Hii ni tovuti ya habari iliyojikita katika kuandika  habari za kina   zikiwemo za mazingira kwa lengo la kuelimisha na kuuhabarisha umma.

Subscribe

  • About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact

© 2025 Bajeti

No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo

© 2025 Bajeti

Welcome Back!

Login to your account below

Forgotten Password?

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In