• About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact
Friday, May 8, 2026
  • Login
Bajeti
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo
No Result
View All Result
Bajeti
No Result
View All Result
Home Mazingira

Wakulima Mlimba wamuomba Rais Samia kuwasadia kuvuna mazao yao

Wasema walipanda wenyewe lakini sasa yanavunwa na watu wengine chini ya ulinzi mkali

by bajeti
July 15, 2025
in Mazingira
0
Wakulima Mlimba wamuomba Rais Samia kuwasadia kuvuna mazao yao

Mkulima wa Kitongoji cha Msondo kilichopo Halmashauri ya Mlimba mkoani Morogoro

Share on FacebookShare on Twitter

NA MWANDISHI WETU MOROGORO

WAKAZI wa Kitongoji cha Msondo kilichopo katika Kijiji cha Idondi Halmashauri ya Mlimba mkoani Morogoro wamemuomba Rais Samia Suluhu Hassan kuwasaidia kuzuia watu wanaovuna mazao yao kwa usimamizi wa polisi kwa kuwa wanateseka na familia zao.

Wananchi hao ambao wamekimbilia katika milima iliyo karibu na kijiji chao kwa hofu ya kukamatwa na Polisi wamesema kwa sasa wanaishi kwa shida kutokana na kushindwa kuvuna mazao yao ambayo waliyapanda wenyewe na kupalilia.

Akizungumza na waandishi wa habari mwishoni mwa wiki  katika kijiji hicho, mmoja wa wakulima hao Nyanda Manzabe amesema eneo hilo lilikuwa na mgogoro katika miaka ya nyuma na mtu anayedai kumiliki zaidi ya ekari 1000 kwa jina la Musa.

Amesema tangu mwaka 2021 walichukua hatua za kisheria juu ya mtu huyo anayedaiwa kuwa mwekezaji ambapo mgogoro huo ulifika katika vyombo vya kisheria na mwisho wao  waliruhusiwa kulima na kulimiliki eneo hilo.

Amesema baada ya hapo kuanzia mwezi Desemba,2024 walianza kulima na kupanda mazao yao na kuyapalilia vizuri na hakukuwa na kitu chochote lakini ilipofika mwezi Mei,2025 baada ya mazao kuiva na kutakiwa kuvunwa ndipo polisi walipofika na kuanza kuwafukuza.

“Kuna shamba moja lilianza kuiva na tulikwenda kuvuna na familia ya wenye shamba hilo lakini walikuja polisi na kutufukuza,na sisi tulikimbia maana walikuwa na mabomu lakini cha ajabu mazao yetu yakaanza kuvunwa lakini tulipokwenda kufyeka mashamba yaliyoiva sasa hivi wakajana tena polisi wengi zaidi ya wale wa mwanzo na kuvuna mazao yetu.

“Hadi sasa hivi wapo shambani wanavuna mazao yetu,tumuomba Rais samia Suluhu Hassan atusaidie kwenye tatizo hili  na sisi tunafamilia na tuko milimani tunaishi kama nyani na hatuna uhuru,sisi tumemalima kihalali lakini iweje sasa hivi tunaanza kuvuna tunavufukuzwa na kisha mazao yetu yanavunwa kwa usimamizi wa polisi”

“Tunamuomba Rais Samia Suluhu Hassan aingilie kati suala hili kwani sisi ni wakulima na tunategemea mazao hayo kulisha familia zetu sasa ikiwa mazao yetu yanavunwa wakati tumelima sisi sasa tutaishije”amesema Manzabe

Mkulima wa Kitongoji cha Msondo kilichopo Halmashauri ya Mlimba mkoani Morogoro akizungumza na waandishi wa habari mwishoni mwa wiki

Mkazi mwingine wa Kijiji hicho ambaye ameomba jina lake lihifadhiwe kwa sababu za usalama wake,amesema wao wamefanya kazi mshambani na kulima mazao yao lakini wanashangaa kuona polisi wanafika na kuwapokonya chakula chao walicholima na haki walipata kihahali kabisa

“Haki tumepata sisi wananchi lakini bado wamerudi kuwapokonya chakula chao na kilimo ndio kinawakoa ikiwemo kuwalipia ada watoto wao na shule zimeshafungua wao kama wakulina wamewekeza katika kilimo.

“Walitusubiri tulime na kupalilia sasa mazao yetu yameiva wanakuja na polisi kuyavuna hii si sawa tunaomba Rais Samia atusaidie kwani hatuna hata chakula cha kuwalisha watoto lakini kwa nini wavune mazao yetu kwani kama kulikuwa na mgogoro si wangetuzuia kabla ya kulima?tumelima,tumepanda,tumepalilia hadi mazao yamekomaa na sasa yameiva ndio wanakuja polisi kutufukuza halafu wanavuna wao hii sio halali “amesema mama huyo

Juhudi za kuwatafuta viongozi wa eneo hilo zinaendelea baada ya kutafutwa bila mafanikio ili kuzungumzia mgogoro huo.

 

Next Post
Mafanikio ya Miaka Minne ya Uongozi wa Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan katika Tasnia ya Mbolea Tanzania

Rais Dk.Samia alivyodhamiria kuwakomboa wakulima kupitia Mpango wa Ruzuku ya Mbolea

DCEA:Raia wa nchi jirani wanafadhili kilimo cha bangi Mara,yakamata tani 7.8

Mkoa wa Mara kinara kilimo cha bangi 2024

TCRA:Uvumi ndio chanzo kikuu cha vurugu

TCRA:Uvumi ndio chanzo kikuu cha vurugu

Discussion about this post

Contact us:

BAJETI COMMUNICATION

info@bajeti.co.tz
bajetinews@gmail.com
+255718699828
P.o.BOX 18133,
DAR ES SALAAM,
TANZANIA

Category

  • Habari
  • Magazeti
  • Makala
  • Mazingira
  • Michezo
  • Picha
  • Sayansi na Teknolojia
  • Siasa

Our Visitors

  • Today's visitors:12
  • Today's page views 12
  • Total visitors 16,119
  • Total page views 18,284

Kuhusu Tovuti Hii

Hii ni tovuti ya habari iliyojikita katika kuandika  habari za kina   zikiwemo za mazingira kwa lengo la kuelimisha na kuuhabarisha umma.

Subscribe

  • About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact

© 2025 Bajeti

No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo

© 2025 Bajeti

Welcome Back!

Login to your account below

Forgotten Password?

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In