• About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact
Tuesday, January 13, 2026
  • Login
Bajeti
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo
No Result
View All Result
Bajeti
No Result
View All Result
Home Habari

TCRA:Uvumi ndio chanzo kikuu cha vurugu

Yawahimiza Wazalishaji wa Maudhui Mtandaoni kuepuka kusambaza taarifa zitakazosababisha taharuki

by bajeti
August 4, 2025
in Habari
0
TCRA:Uvumi ndio chanzo kikuu cha vurugu

Meneja wa Huduma za Utangazaji kutoka Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA),Mhandisi Andrew Kisaka

Share on FacebookShare on Twitter

 

NA MWANDISHI WETU

MAMLAKA ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imewatahadharisha Wazalishaji wa Maudhui Mtandaoni(Blogger), kuwa makini na taarifa zitakazochochea chuki  na kuleta machafuko nchini hasa wakati huu kuelekea katika Uchaguzi Mkuu.

Mbali na hilo lakini pia TCRA imewahimiza Wazalishaji wa Maudhui Mtandaoni kuepuka kusambaza taarifa zitakazosababisha  taharuki  na ulipizaji wa kisasi ikiwemo kutopendelea upande wowote ili kuleta amani,umoja na mshikamano kwa jamii.

Kauli ya TCRA imekuja wakati ambapo watanzania wanatarajiwa kupiga kura ya kumchagua Rais,Wabunge na Madiwani katika Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 29,2025.

Akizungumza Agosti 3, 2025 mkoani Dar es Salaam  wakati  akiwasilisha mada katika mkutano ulioandaliwa na  Tume Huru ya Uchaguzi nchini (INEC) kwa  Wazalishaji wa Maudhui Mtandaoni, Meneja wa Huduma za Utangazaji kutoka TCRA,Mhandisi Andrew Kisaka amesema ni muhimu kwa Wazalidhaji hao wa Maudhui Mtandaoni kuepuka kuchapisha taarifa ambazo zitaleta taharuki na machafuko ndani ya nchi hasa katika kipindi hiki cha kuelekea Uchaguzi Mkuu.

Mhandisi Kisaka amebainisha kuwa wakati wa uchaguzi kuna mazingira ya migawanyiko, mivutano ya kijamii, na upotoshaji wa hali ya juu hivyo ni muhimu  kwa Wazalishaji wa Maudhui Mtandaoni  kuepuka kusambaza uvumi na kutangaza kwa umakini ikiwemo kutopendelea upande wowote  na kukemea lugha za chuki.

Aidha amewataka  wazalishaji hao  nchini kote  kuimarisha maadili yao na kuchukua jukumu muhimu katika kuhakikisha uchaguzi unafanyika kwa amani kwa kupandisha maudhui yenye tija na manufaa  kwa Taifa.

“Kama unaona maudhui hayo yataleta taharuki  ni bora kuachana nayo,vyombo vya habari vinaweza kujikuta vikichangia machafuko kwa kueneza uvumi au kuchochea upendeleo wa kisiasa kutokana na mazingira magumu na yenye shinikizo la juu la uchaguzi.”ameongeza Mhandisi Kisaka

Mhandisi Kisaka ametolea mfano wa machafuko ya uchaguzi yaliyotokea nchini Nigeria mwaka 2007 na Kenya 2011.

“Katika machafuko hayo zaidi ya watu 800 walipoteza uhai nchini Nigeria wakati nchini Kenya zaidi ya watu 1,000 walipoteza uhai na wengine 600,000 kupoteza makazi.

“Ili kukabiliana na maafa wakati wa uchaguzi na baada kuna miongozo ya utoaji wa taarifa ambayo inatatua changamoto hizo.

“Uvumi ndiyo chanzo kikuu cha vurugu hivyo  Vyombo vya habari vinapaswa kuchunguza kwa umakini uvumi na kutoa taarifa sahihi na kwa haraka iwezekanavyo ili kuzuia mzunguko wa vurugu za kulipiza kisasi.” amesema Mhandisi Kisaka.

Hata hivyo Mhandisi Kisaka ameongeza kuwa vyombo vya habari havitakiwi kuchapisha taarifa ya kila kauli ya uchochezi kutoka kwa wanasiasa ,hata kama kauli hizo zinaonekana kuwa habari na zenye kuvutia msomaji ikiwemo lugha za kudhalilisha zinazoweza kuchochea wananchi kutenda vitendo vya kikatili.

Akizungumzia kuhusu urushaji wa matangazo mubashara kwa wazalishaji hao wa maudhui mtadaoni,Mhandisi Kisaka amefafanuwa kuwa katika kipindi hiki cha uchaguzi, ni  muhimu wazalishaji hao kuchukua tahadhari binafsi ya kutoa  matangazo mubashara(live)   ya mikutano ya kampeni za wagombea kwa sababu yanaweza kuleta  machafuko ikiwemo kuzuia kuonesha picha zinazochochea vurugeu  na ikiwa  ni lazima,basi pia  kusimamisha matangazo hayo mubashara ili kuzuia hali kuwa mbaya zaidi.

Next Post
Mto Msimbazi ‘waitafuna’ Vingunguti

Mto Msimbazi ‘waitafuna’ Vingunguti

Kamishna Jenerali Lyimo:Tutateketeza dawa za kulevya nchi nzima

Wapakistan vinara biashara dawa za kulevya

Spika Mstaafu Job Ndugai afariki

Spika Mstaafu Job Ndugai afariki

Discussion about this post

Contact us:

BAJETI COMMUNICATION

info@bajeti.co.tz
bajetinews@gmail.com
+255718699828
P.o.BOX 18133,
DAR ES SALAAM,
TANZANIA

Category

  • Habari
  • Magazeti
  • Makala
  • Mazingira
  • Michezo
  • Picha
  • Sayansi na Teknolojia
  • Siasa

Our Visitors

  • Today's visitors:1
  • Today's page views 1
  • Total visitors 13,057
  • Total page views 14,802

Kuhusu Tovuti Hii

Hii ni tovuti ya habari iliyojikita katika kuandika  habari za kina   zikiwemo za mazingira kwa lengo la kuelimisha na kuuhabarisha umma.

Subscribe

  • About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact

© 2025 Bajeti

No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo

© 2025 Bajeti

Welcome Back!

Login to your account below

Forgotten Password?

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In