• About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact
Sunday, January 18, 2026
  • Login
Bajeti
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo
No Result
View All Result
Bajeti
No Result
View All Result
Home Makala

Rais Dk.Samia alivyodhamiria kuwakomboa wakulima kupitia Mpango wa Ruzuku ya Mbolea

Wadau wapongeza

by bajeti
July 17, 2025
in Makala
0
Mafanikio ya Miaka Minne ya Uongozi wa Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan katika Tasnia ya Mbolea Tanzania

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akisikiliza kutoka kwa Waziri wa Kilimo Hussein Bashe kuhusu matumizi ya kadi janja ya mkulima aliyesajiliwa kwenye mfumo wa mbolea za ruzuku inayotolewa kwa ushirikiano baina ya benki ya CRDB na Serikali itakayomwezesha mkulima kunufaika na huduma za pembejeo za ruzuku na kifedha kabla ya kuzindua rasmi kadi hiyo.

Share on FacebookShare on Twitter

NA MWANDISHI WETU

WADAU wa tasnia ya mbolea wameipongeza Serikali kwa utekelezaji wake madhubuti wa Mpango wa Ruzuku ya Mbolea ambao katika kipindi cha miaka mitatu iliyopita umechochea matumizi ya pembejeo hiyo katika Sekta ya Kilimo na kuongeza tija kwa wakulima.

Serikali ya Awamu Sita inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, ilizindua utekelezaji wa Mpango wa Ruzuku ya mbolea katika maadhimisho ya sherehe za wakulima zilizofanyika katika viwanja vya John Mwakangale jijini Mbeya mwaka 2022/2023 ili kukubaliana na ongezeko la bei ya bidhaa hiyo katika soko la Dunia.

Akiwasilisha bajeti ya 2025/26, Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe, anasema katika miaka mitatu ya 2022/23 hadi 2024/25 serikali imesambaza mbolea ya ruzuku yenye jumla ya tani 1,454,974,721 yenye thamani ya zaidi ya shilingi Bilioni 708.6 kwa wakulima wa mazao yote nchini.

Anasema utekelezaji wa Mpango wa Ruzuku umechangia kwa kiasi kikubwa ongezeko la matumizi ya mbolea kutoka tani 363,599 mwaka 2021/22 hadi tani 848,884 mwaka 2023/24.

Hata hivyo wadau mbalimbali wa tasnia ya mbolea  ikiwemo Kampuni ya ETG Agri Input Tanzania wameunga mkono tathmini hiyo ambapo viongozi wake wamesema ruzuku ya mbolea imeleta maboresho makubwa katika upatikanaji wa mbolea kwa wakulima nchini.

“Mbolea imekuwa ikipatikana kwa bei nafuu ukilinganisha na bei ya soko, hali hii imeongeza uwezo wa wakulima kununua mbolea kwa wakati.

Tangu kuanza kwa Mpango wa Ruzuku ya Mbolea, Kampuni ya ETG imesambaza tani 300,000 za aina mbalimbali za mbolea kupitia mtandao wake wa maghala, maduka na wafanyabiashara.

“Kwa msimu ujao, tumejipanga kuendelea kushiriki kikamilifu katika kusambaza mbolea kupitia mfumo wa pembejeo za Ruzuku kwa kuongeza idadi ya vituo vya mauzo, kushirikiana na wafanyabiashara (agrodealers) na kuongeza ufanisi wa usambazaji kupitia mfumo wa Last Mile Delivery na tunaishukuru sana serikali kwa kuendelea kulipa ruzuku hii.”

“Pia tumejipanga kuwa na mbolea ya kutosha kabla ya kuanza kwa msimu ili kuepuka ucheleweshaji wa bidhaa hiyo kwa wakulima. Hivi sasa tuna meli tatu bandarini zinazosubiri kupakuliwa tayari kwa ajili ya kuwasambazia wakulima kwa ajili ya msimu mpya wa ruzuku wa 2025/26.”inaeleza taarifa ETG

Taarifa inaendelea kueleza kuwa “Mpango huu (wa ruzuku)  umeongeza wigo wa biashara kwa kampuni yetu kwa kuwafikia wakulima wadogo vijijini  pia tumepata nafasi ya kushirikiana moja kwa moja na serikali, kuongeza uaminifu wa kampuni yetu sokoni na kuchangia kwa kiasi kikubwa uzalishaji wa mazao ya chakula kwa kuwawezesha wakulima kutumia pembejeo bora kwa wakati.

Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Minjingu Mine and Fertiliser Company iliyoko mkoani Manyara, Hans Tosky, anasema kwa ujumla ulipaji wa fedha za ruzuku umekuwa wa kuridhisha kwa vile kampuni yake imekuwa ikipokea malipo wakati wote.

Ameishukuru Serikali kwa jitihada hizo na kuahidi kwamba kampuni yake imehamasika kuendelea kuwahudumia wakulima nchini.

Akizungumzia kuhusu maandalizi ya msimu ujao, Tosky anasema “Tumejipanga kuwahudumia wakulima kwa kuzingatia kwamba viwanda vya ndani vina fursa nyingi ya kuweza kujitanua na kupata masoko ndani na nje ya nchi.”

“Mbolea zinazozalishwa na kiwanda chetu zimeshafahamika na kukubalika kwa wakulima na hivyo kampuni inatarajia kuzifikisha mbolea hizo kwa wakulima mapema kabla ya kuanza kwa msimu wa kilimo,” anaeleza Tosky .

Anasema, Mpango wa Ruzuku ya Mbolea umemletea mkulima wa Tanzania ahueni ya makali ya bei ya bidhaa hiyo na upatikanaji wake ikilinganishwa na siku za nyuma.

Jambo jingine la kutia moyo, kwa mujibu wa Tosky, ni kwamba mbolea zinazozalishwa nchini zimepata nafasi kubwa katika ushindani kwenye soko na zile zinazoagizwa kutoka nje.

Nayo Kampuni ya Mbolea Tanzania (TFC) imeeleza katika taarifa yake kwamba Mpango wa Ruzuku ya Mbolea umesaidia sana kuleta ustahimilivu wa bei na kuongeza matumizi yake.

Kampuni imesema upatikanaji wa mbolea kwa wakati na matumizi yake sahihi umechochea ongezeko la tija ya mazao mbalimbali nchini. “Mpango huu umewezesha utambuzi wa wakulima na maeneo yao. Umepunguza mwanya wa utoroshaji wa mbolea na matumizi mabaya ya fedha za serikali,” taarifa ya TFC imesisitiza.

Kuanzia mwaka 2022/23, TFC ilisambaza tani 4,500 za mbolea zenye thamani ya shilingi bilioni 8.9, mwaka 2023/24 tani 29,133.25 zenye thamani ya shilingi bilioni46.5 na mwaka 2024/25 tani 54,500 zenye thamani ya shilingi bilioni 81.5.

Kampuni ya Mbolea inakiri kunufaika kwa kuongeza mauzo na mtajiwa usambazaji wa mbolea kwa wakulima nchini kupitia ruzuku.

“Serikali iendelee kuweka ruzuku kwenye mbolea, ikiwezekana kwenye mbolea zote,” TFC inasisitiza katika taarifa yake.

Katika taarifa yake, Mkurugenzi Mkuu wa Itracom Nduwimana Nazaire ameeleza kuwa, kama wazalishaji wa ndani kwa msimu wa kilimo 2024/2025 Mbolea za FOMI zilipatiwa ruzuku kubwa na bei ya mkulima ikawa nafuu na hivyo kuwawezesha kumudu gharama za mbolea na kuongeza tija ya uzalishaji.

Amekiri, uwepo wa mpango wa ruzuku kumechangia sana wakulima kupata mbolea za FOMI kwa bei na kuahidi kuendelea kushiriki kwenye usambazaji wa mbolea za ruzuku kwa msimu ujao wa 2025/2026 ambapo wanatarajia kusambaza kiasi cha tani 500,000.

Next Post
DCEA:Raia wa nchi jirani wanafadhili kilimo cha bangi Mara,yakamata tani 7.8

Mkoa wa Mara kinara kilimo cha bangi 2024

TCRA:Uvumi ndio chanzo kikuu cha vurugu

TCRA:Uvumi ndio chanzo kikuu cha vurugu

Mto Msimbazi ‘waitafuna’ Vingunguti

Mto Msimbazi ‘waitafuna’ Vingunguti

Discussion about this post

Contact us:

BAJETI COMMUNICATION

info@bajeti.co.tz
bajetinews@gmail.com
+255718699828
P.o.BOX 18133,
DAR ES SALAAM,
TANZANIA

Category

  • Habari
  • Magazeti
  • Makala
  • Mazingira
  • Michezo
  • Picha
  • Sayansi na Teknolojia
  • Siasa

Our Visitors

  • Today's visitors:27
  • Today's page views 27
  • Total visitors 13,184
  • Total page views 14,930

Kuhusu Tovuti Hii

Hii ni tovuti ya habari iliyojikita katika kuandika  habari za kina   zikiwemo za mazingira kwa lengo la kuelimisha na kuuhabarisha umma.

Subscribe

  • About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact

© 2025 Bajeti

No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo

© 2025 Bajeti

Welcome Back!

Login to your account below

Forgotten Password?

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In