• About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact
Monday, May 25, 2026
  • Login
Bajeti
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo
No Result
View All Result
Bajeti
No Result
View All Result
Home Michezo

Nyota Klabu ya Simba kuibua vipaji Segerea

by BAJETI
September 8, 2021
in Michezo
0
Share on FacebookShare on Twitter

NYOTA wa zamani wa klabu ya Simba Sphere Mbwembwe pamoja na mashabiki wa klabu hiyo wameandaa   michuano ya mchezo wa mpira wa miguu katika Jimbo la Seregerea jijini Ilala Mkoa wa Dar es Salaam  lengo likiwa ni kuendeleza vipaji vya soka kwa vijana.

Michuano hiyo inayokwenda kwa jina la ‘Segerea Super Cup’ imeanza kutimua vumbi juzi ndani ya Uwanja wa Dogodogo kwa ikijumuisha timu 16 ambazo zitashiriki michuano hiyo.

Mchezo wa ufunguzi wa michuano hiyo ulichezwa kati ya Songea FC wakikabiliana na Segerea FC ambao ndio wenyeji wa michuano hiyo.

Hata hivyo katika mchezo huo timu hizo zilitoka sare ya mabao 2-2.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa michuano hiyo mkoani Dar es Salaam leo,mgeni rasmi katika uzinduzi huo Hope Kaiza, asema amevutiwa na mawazo ya wadau hao wa soka na kwamba ataunga mkono kuhakikisha Segerea inakuwa na vipaji vya kutosha.

Kaiza ambaye pia ndio Mdhamini Mkuu wa michuano hiyo amesema kwa sasa mpira ni ajira kubwa kwa vijana hivyo wanatakiwa kuwekezewa ili kutumiza ndoto zao.

“Niko kwa hapa kwa sababu nina mapenzi na mpira hivyo nitakuwa nawasapoti vijana kwa kile nilichonacho,hii itasaidia vijana wa Segerea lakini pia Tanzania kwa ujumla kwa kuwa Kijana yeyote atakae pata mafanikio ni kwa ajili ya Taifa zima.

“Jambo la msingi wazingatie malengo Kama wazazi na wadau tumeamua kujitoa kwa ajili yao nao wapambane ili kufukia ndoto zao,” amesema Kaiza.

Aidha Kaiza amefafanua kuwa  katika michuano hiyo kutakuwa na zawadi mbali  ambazo zitatolea  huku mshindi wa kwanza akichukua mbuzi na wa pili jezi na mashabiki watakao  shangilia vizuri.

Mjumbe wa Kamati ya Maandalizi  ya michuano hiyo  Shebi Machumani  amebainisha kuwa Tanzania kuzalisha wachezaji wakubwa kila siku kazi hiyo haipo kwa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) pekee bali wadau ndio wanatakiwa kuongeza  nguvu katika maeneo yao ili kuibua vipaji.

“Nashukuru Mungu kwanza maandalizi yalikuwa mazuri na wachezaji wote ambao wapo hapa wanaujua mpira naimani msimu ujao baadhi yao wataweza pata nafasi katika klabu mbalimbali,” ameongeza  Machumani

Next Post

Marekani hatarini kufilisika

Arusha kukusanya Bilioni 24 kutekeleza miradi ya maendeleo

Serikali kumaliza mgogoro Msitu wa Pugu Kazimzumbwi

Discussion about this post

Contact us:

BAJETI COMMUNICATION

info@bajeti.co.tz
bajetinews@gmail.com
+255718699828
P.o.BOX 18133,
DAR ES SALAAM,
TANZANIA

Category

  • Habari
  • Magazeti
  • Makala
  • Mazingira
  • Michezo
  • Picha
  • Sayansi na Teknolojia
  • Siasa

Our Visitors

  • Today's visitors:15
  • Today's page views 15
  • Total visitors 16,469
  • Total page views 18,680

Kuhusu Tovuti Hii

Hii ni tovuti ya habari iliyojikita katika kuandika  habari za kina   zikiwemo za mazingira kwa lengo la kuelimisha na kuuhabarisha umma.

Subscribe

  • About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact

© 2025 Bajeti

No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo

© 2025 Bajeti

Welcome Back!

Login to your account below

Forgotten Password?

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In