• About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact
Thursday, May 14, 2026
  • Login
Bajeti
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo
No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo
No Result
View All Result
Bajeti
No Result
View All Result
Home Habari

MISA-TAN yaomba marekebisho sheria huduma za habari

by bajeti
June 27, 2022
in Habari
0
MISA-TAN yataka marekebisho sharia ya habari

Makamu Mwenyekiti wa Taasisi ya Vyombo vya Habari Kusini mwa Afrika (MISA-TAN) James Marenga (Kulia) akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam juzi kuhusu mapendekezo ya marekebisho ya Sheria za Huduma ya Habari ya mwaka 2016(Picha na Mpigapicha wetu)

Share on FacebookShare on Twitter

 

WADAU wa habari nchini wamependekeza kufanyiwa mapendekezo baadhi ya vifungu vya Sheria ya Huduma ya Habari ya mwaka 2016 na ya Makosa Mtandaoni ya mwaka 2015 kutokana na kutoa uhuru mkubwa waliopewa  wasimaizi wa sheria.

Hata hivyo moja ya maeneo yanayoleta mkanganyiko katika Sheria ya Huduma ya Habari ya mwaka 2016 ni kuzuia kutoa taarifa za wawekezaji.

Akifafanua kuhusu changamoto za sheria hizo kwa waandishi wa habari mwishoni mwa wiki,Makamu Mwenyekiti wa Taasisi ya Vyombo vya Habari Kusini mwa Afrika (MISA-TAN) James Marenga amesema licha ya baadhi ya kanuni kuwa zinaleta unafuu lakini asilimia kubwa ni sheria kandamizi.

Amesema baadhi ya vipengele katika Sheria ya Huduma ya Habari ya mwaka 2016 inaunda mahakama ndogo dhidi ya taarifa za waandishi wa habari licha ya kutambua taaluma za wanahabari.

“Kwa mujibu wa Sheria hii kila mwandishi atakuwa na namba maalum lakini Kifungu cha 52(1)  kinaelezea suala la uchochezi bila kufafanuwa  jambo linaloweza kutumika vibaya na wasimamizi wa sheria”amesema Marenga

Marenga ambaye ni Wakili amefafanuwa kuwa Sheria ya Makosa Mtandaoni ya mwaka 2015 ina vifungu hatari ikiwa haitafanyiwa marekebisho.

Aidha amebainisha kuwa sheria hiyo ilitungwa kwa hati ya dharula na ilitumia siku mbili tu kupitishwa na hakukuwa na waandishi walioshirikishwa katika utungwaji wa sheria hiyo.

“Kifungu cha 50(1) (3)(a)(b)(c) kinaondoa haki ya mtu kukata rufaa hivyo sisi tunapendekeza kuwa haki ya mtu kukata rufaa  ni haki ya kikatiba”amesema Marenga.

Marenga ameongeza kuwa wao kama wadau wa habari wanapendekeza pia kuwa kuna maeneo ambayo wao wameyaanisha na kuona kuwa hayo ndiyo yanavunja Katiba na haki za msingi za kupata habari.

 

Hata hivyo Sheria hizo zimeonekana kulalamikiwa na wadau wa habari na kuitaka serikali kubadilisha baadhi ya vifungu hivyo ili kuzifanya sheria hizo kuwa za kidemokrasia zaidi kama zilivyo baadhi ya nchi barani Afrika ikiwemo Ghana.

Mwandishi:Goodluck Hongo

Next Post
Bonde la Mto Kilombero hatarini

Bonde la Mto Kilombero hatarini

Wanaume wahanga ugonjwa wa mabusha

Wanaume wahanga ugonjwa wa mabusha

TEF yaungana na wanahabari kupinga sheria kandamizi

TEF yaungana na wanahabari kupinga sheria kandamizi

Discussion about this post

Contact us:

BAJETI COMMUNICATION

info@bajeti.co.tz
bajetinews@gmail.com
+255718699828
P.o.BOX 18133,
DAR ES SALAAM,
TANZANIA

Category

  • Habari
  • Magazeti
  • Makala
  • Mazingira
  • Michezo
  • Picha
  • Sayansi na Teknolojia
  • Siasa

Our Visitors

  • Today's visitors:13
  • Today's page views 14
  • Total visitors 16,214
  • Total page views 18,386

Kuhusu Tovuti Hii

Hii ni tovuti ya habari iliyojikita katika kuandika  habari za kina   zikiwemo za mazingira kwa lengo la kuelimisha na kuuhabarisha umma.

Subscribe

  • About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact

© 2025 Bajeti

No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Siasa
  • Mazingira
  • Magazeti
  • Makala
  • Picha
  • Michezo
  • Matangazo

© 2025 Bajeti

Welcome Back!

Login to your account below

Forgotten Password?

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In