VIENNA,AUSTRALIA
SHIRIKA la Umoja wa Mataifa la Nishati ya Atomiki, (IAEA) limesema mbegu za mazao zilizopelekwa kituo cha anga za juu mwezi Novemba mwaka 2022 zimepandwa kama sehemu ya utafiti wa kuimarisha aina mbalimbali za mbegu zinazohimili mabadiliko ya tabianchi.
Kwa mujibu wa taarifa ya IAEA iliyotolewa Januari 12,2023 imeeleza kuwa tayari mbegu hizo ikiwemo Mtama zimmepandwa eneo la ndani na nje ya kituo hicho na hivyo zinapata miali kamilifu ya anga za juu pamoja na viwango vya juu zaidi vya joto kwenye eneo hilo.
Kwa mujibu wa IAEA yenye Makao yake Makuu, Vienna nchini Australia, mbegu hizo zilipelekwa na shirika hilo pamoja na lile la Chakula na Kilimo Duniani(FAO) kwa lengo la kuchunguza athari za miali ya anga za juu kwenye mbegu kama sehemu ya utafiti wa kuimarisha aina mbalimbali za mbegu zinazohimili mabadiliko ya tabianchi na hivyo kuongeza uhakika wa chakula.
“Lengo ni kubaini iwapo mazingira magumu ya hali ya hewa anga za juu kama vile joto kali kupindukia, miale kutoka anga za juu vinaweza kuchochea mabadiliko kwenye mbegu na hatimaye mabadiliko hayo ya hali ya hewa yanaweza kusaidia mimea kuwa na mnepo zaidi pindi inapokabiliwa na changamoto za ukuaji au kumea duniani,” imesema taarifa hiyo.
Naibu Mkurugenzi Mkuu wa IAEA ambaye pia ni Mkuu wa Idara ya Sayansi ya Nyuklia na Matumizi yake, Najat Mokhtar amesema wana wajibu wa kuchunguza teknolojia za kinyuklia ambazo zinaweza kuleta tofauti chanya kwa afya ya binadamu na chakula anachokula.
“Jinsi dunia inahaha kuhimili madhara ya mabadiliko ya tabianchi, tunahitaji kuongeza kasi ya tafiti za kuboresha mimea na kupata majawabu yanayotesheleza na fanisi,” amesema Mokthar.




Discussion about this post